Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,361
- 2,734
Hivi sasa mbunge wa Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili......anawahutubia wananchi wa Bukoba Mjini na inaonekana kuna mgogoro mkubwa kati yake na Meya wa Manispaa na Mbunge huyo maana amenza kuhutubia kwa kupinga maneno yaliyozagaa kuwa Mbunge huyo anamuogopa Meya kwa kuwa anataka kuchukua nafasi yake.
Kagasheki anafunguka kwa kusema kuwa alimsaidia meya huyo kuomba Uraia na kwa sasa ni raia.....alafu anamzushia kuwa kagasheki ni mpinga maendeleo.Kagasheki analalamika hadi hivi sasa kwenye hotuba yake kuwa Halmashauri imemdhihaki kwa kudai kuwa wamesema wapange chohcote wanachotaka na kukitekeleza kwa maana mbunge si chochote. Anasema Halmashauri imekopa zaidi ya Bilioni 2.5 kwa ajili ya maendeleo lakini mikataba haionekani.
Anasema haieleweki fedha hiyo italipwa na nani kwa maana mkataba wa mkopo huo hauonekani.
Katika kuelezea hayo kila mara anataja kuwa Dr. Slaa atakuja kuwaumbua baadae. Anasema wafanye kwa umakini vinginevyo Dr. Slaa akishutuka na kusema kuwa mkataba umejaa ufisadi wataumbuka. Anasema CHADEMA watatumia nafasi hiyokuwaumbua hasa Dr. Slaa akishtukia mikataba hiyo.Anasema yeye kama mbunge hajaiona mikataba ya mikopo na ujenzi wa soko jipya, madiwani wameiona wapi ? anahoji Kagasheki, wasiwasi wake Dr. Slaa akiiona mikataba hiyo na ikawa na mapungufu itakuwa tabu.
Mwingine aliyepo na anayesikiliza aendelee kutupia