Mgogoro kati ya Waziri Kagasheki na H.shauri ya Manispaa ya Bukoba.....kila mara Dr. Slaa anatajwa

Kagasheki: Mwosha, Huoshwa! Amani, Tulia kwa Amani

Naomba kuwapasha Wana-JF ukweli ninaoujua kwa haraka haraka sana.

  • Kagasheki hakuna anachokipigania dhidi ya Dr. Amani zaidi ya wasiwasi wa Ubunge wake hapo 2015

  • Kasi ya miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa na kufanikiwa chini ya Uongozi wa Dr. Amani ni pigo sana kwa mbwembwe za Kagasheki kisiasa.

  • Siyo kweli hata kidogo kuwa wananchi wanahofu au wanapinga mradi wa viwanja. Mafanikio ya mradi huu yamemuinua sana Mayor Amani. Na fahamuni, baada ya matusi ya mkutano wa Kagasheki wananchi wametaka kujua ukweli na walio wengi sasa wanamuona Kagasheki kama mtu aliyechanganyikiwa wakati Dr. Amani anazidi kung'aa.

  • Ubunifu kwa Dr. amani haukuanza leo. Mradi wa kuendesha baiskeli maarufu kama ASECDO uliotoa ajira na kuwafumbua macho vijana kujua kuwa kumbe usafirishaji ni ajira ulibuniwa na Dr. Amani. Katika hatua za juu zaidi wengine walianza kuendesha pikipiki maarufu kama bodaboda. Muulizeni Kagasheki kwa nini alizipinga bodaboda 2005 na kuwafirisi vijana na leo hii anajifanya anawajari kinafiki?

  • Siyo kweli hata kidogo kuwa wananchi au wafanyabiashara wanahofu au wanapinga mradi wa ujenzi wa soko. Na kwa taarifa ya wasiojua, wafanyabiashara wengi wamekwisha tafuta vibanda na maeneo ya kuhamia kwa muda ili kuendeleza shughuli zao wakati wa kipindi cha ujenzi. Wataondoka kama 1000, watakaporudi zitakuwepo nafasi 2000!

  • Kagasheki kwa nini hasemi kuwa 2010, alipomaliza kumuonga aliyekuwa Meneja wa KCU, alimuonga pia Dr. Amani naye asigombee Ubunge ili yeye apite bila kupingwa ndani ya ccm? Mbona pia hasemi juu ya ahadi ya kuachiana kijiti kati yake na Dr. Amani?

  • Kagasheki ni mnafiki wa hali ya juu. Wakati Ukoo wa Rwangisa na Masabara ndiyo waliochangia sana 2005 kumuingiza kwenye siasa baada ya kuusaliti ukoo wa Rwakatare, 2010 Kagasheki ndiye ali-engineer fitna ya kumng'oa Rwangisa kwenye Umeya. Siwezi kusahau alfajiri ile ya kuhesabu kura, Kagasheki akiwa Walk Guard Hotel. Wakati hesabu zilikwisha onyesha Rwakatare ameshinda; ni maboksi ya kura za Nshambya tu ndizo zilikuwa hazijafika Manispaa. Kagasheki akawa anamwambia Mzee Rwangisa anaomba iletwe ndege ya kukodiwa ili atoroke. Na Mzee Rwangisa akamujibu kuwa ni bora hayo masanduku ya Nshambya yapelekwe yakatupwe Kisiwani Musira iwe kesi lakini Kagasheki atangazwe mshindi.

  • Kagasheki ni mtu asiyeweza kumudu majibizano ya hoja kwa hoja; ni mbabe. Na akipandwa na temper hubwabwaja kama mtoto mchanga. Siyo mara ya kwanza Kagasheki kubwabwaja siri za kiofisi hasa za iliyokuwa Wizara yake-Mambo ya Ndani. Mfano 2010 alibwabwaja siri yake na Rwangisa juu ya Rwangisa kuwa na Uraia wa Marekani. Alivyomshenzi Kagasheki ndiye aliyehakikisha kina Muhingo wanaingiza habari hii kwenye local national newspapers

  • Bukoba ccm na Manispaa inapaswa kugeuka haraka sana kutoka inakoelekea kutawaliwa na ukoo mmoja tu –Kagasheki

  • Kagasheki ana tabia za Kiswahili za kupenda kulea na kuamini majungu. Si kweli kwamba Kagasheki ni mtu wa maadili kivile. Mfano Kagasheki yuko tayari kufanya kazi na wahuni (Amin-Uswahilini, Enock-jambazi-Kashai), kutetea wezi (Mutensa na Ujambazi wa Kutumia silaha) maadamu tu ni maarufu na wanampamba, wanamwabudu na kufanya kama yeye atakavyo.
 
siasa za bukoba ni ngumu mno,kuna vita vya koo mpaka udini.nilishuhudia uchaguzi wa udiwani wakristo walikuwa na slogan msalaba kwanza! kuna vijiji vya bukoba balaa tupu,siasa zimepitiliza
 
Dk Slaa ni tishio sana kwa viongozi wa CCM,ukitaka kujua huyu jamaa ni hatari kwa uhai wa chama cha mapinduzi angalia hata hapa jamvini anavyopakwa matope na Makada uchwara wa CCM.
 
Back
Top Bottom