Mgogoro kati ya Waziri Kagasheki na H.shauri ya Manispaa ya Bukoba.....kila mara Dr. Slaa anatajwa

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,732
Hivi sasa mbunge wa Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili......anawahutubia wananchi wa Bukoba Mjini na inaonekana kuna mgogoro mkubwa kati yake na Meya wa Manispaa na Mbunge huyo maana amenza kuhutubia kwa kupinga maneno yaliyozagaa kuwa Mbunge huyo anamuogopa Meya kwa kuwa anataka kuchukua nafasi yake.

Kagasheki anafunguka kwa kusema kuwa alimsaidia meya huyo kuomba Uraia na kwa sasa ni raia.....alafu anamzushia kuwa kagasheki ni mpinga maendeleo.Kagasheki analalamika hadi hivi sasa kwenye hotuba yake kuwa Halmashauri imemdhihaki kwa kudai kuwa wamesema wapange chohcote wanachotaka na kukitekeleza kwa maana mbunge si chochote. Anasema Halmashauri imekopa zaidi ya Bilioni 2.5 kwa ajili ya maendeleo lakini mikataba haionekani.

Anasema haieleweki fedha hiyo italipwa na nani kwa maana mkataba wa mkopo huo hauonekani.

Katika kuelezea hayo kila mara anataja kuwa Dr. Slaa atakuja kuwaumbua baadae. Anasema wafanye kwa umakini vinginevyo Dr. Slaa akishutuka na kusema kuwa mkataba umejaa ufisadi wataumbuka. Anasema CHADEMA watatumia nafasi hiyokuwaumbua hasa Dr. Slaa akishtukia mikataba hiyo.Anasema yeye kama mbunge hajaiona mikataba ya mikopo na ujenzi wa soko jipya, madiwani wameiona wapi ? anahoji Kagasheki, wasiwasi wake Dr. Slaa akiiona mikataba hiyo na ikawa na mapungufu itakuwa tabu.

Mwingine aliyepo na anayesikiliza aendelee kutupia
 
Amepingana na utaratibu wa Manispaa wa kuvunja soko tarehe 15/01/2013 na amewatamkia wananchi kuwa soko halivunjwi
 
Dr Slaa ndio nuru inayowamulika watanzania wote bila kujali kanda, dini wala kabila. Mungu akubariki Dr Slaa.
 
Aiseeeeee! Kumbe wanashindwa kufisadi kwa 7bu ya dr.wetu wa ukweli slaa! Ahsante!
 
Na bado 2015 tunamkabidhi usukani wa hii nchi ili mtafutane na ufisadi wenu muanze namna ya kutubu,kwanza umesema maliasili na biashara ya meno ya ndovu inahusisha vigogo so utadeal nao,sasa kigogo wa kwanza ni katibu mkuu wa magamba anza nae ili wengine wafuatie.....
 
nimefurahi sana kumbe dr anaogopeka hivi na magamba..ati hofu kubwa ni dr akijua mikataba hiyo, watamueleza imekuaje ahaaha...dr ukitoka karagwe pitia bukoba mjini ushughulikie hilo swala mara moja...
 
Daaaaa dr akijua tuu wamekwishaa bora awambie mapema maana watalipuliwa si muda mrefu!
 
Nina uhakika Dr Slaa W. hizi taarifa anazo tayari na kikosi kazi kipo kazini kuchimbua ukweli halisi. Stay tuned.
 
Ni kweli Dk, Slaa ametajwa sana katika mkutano wa Mh. Kagasheki. Nimegundua kwamba Dk Slaa ni tishio na anarekebisha uozo. Ushauri wangu kwa Wanakagera, wasawazishe tofauti hizi kati ya Mbunge na Meya kwani hazileti tija yeyote kwa maendeleo ya Bukoba na wananchi wake.

Kwa mwenye taarifa eti ni kweli Dk Slaa kesho atawasha moto katika viunga hivi vya Bukoba? Kwa mwenye taarifa atujuze jamani.
 
kagasheki amehisi anafunikwa bukoba. kaamua kuwaeleza wananchi kuwa wasikubali mambo harakaharaka inawezekana kuna ufisadi. DR SLAA akifuatilia akajua itakuwa balaa
 
Anasema hofu yake kubwa ni Wilbroad Slaa endapo atajua kuwa mikataba hiyo ina matatizo
Ajabu wanamuogopa slaa badala yakumuogopa MUNGU na wanainchi wenye hela zao zakodi?kwahiyo mpaka Slaa awashtukie so irritating
 
Kama hayo ni ya kweli basi CCM wanamwogoa Dr Slaa kama ukoma. Ila kama aliweza kuwataja wakubwa kwenye ufisadi....
 
Na huo ndio ukweli!! Ccm wanamuogopa Dr kuliko jehanamu!! Ndo maana mnaona wanaongeza wachumia tumbo humu ili kumchafua Dr!!

Watu wakisema Dr anaongoza nchi indirect wana maana kubwa!!

Asante Kagasheki kwa kutuonyesha mtu anaetufaa!! Yaani CCM wanamuogopa Dr kuliko hata mwenyekiti!!?

MUNGU AKUJAALIE NGUVU DR. SLAA!!
 
Uozo mtupu, kwani Slaa akitoweka nchi haiendi?

Acheni kumpandisha hadi nafasi ya Mwenye enzi,walikuja wakapita nchi itaendelea, tunahitaji watu wenye INNER FEELING

from Purkinje fibers si CCM wala CDM!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom