Mkuu, naona umeandika kiufuasi wa urusi sana, lakini ukweli ni kwamba baada ya kuanguka kwa Soviet (USSR), mataifa ya mashariki ya ulaya yaliyokuwa wanachama wa soviet chini ya urusi yalikuwa fukara sana, mengi yalitamani na bado yanatamani kujiunga na kambi ya magharibi ili kupata hafueni ya kiuchumi, labda kama hujui jinsi majeshi ya Russia yalivyojiondoa haraka ujerumani mashariki baada ya wananchi wakule kuanza kuwapiga kwa mawe urusi,
Baada ya kuanguka kwa USSR hakuna nchi ya ulaya mashariki iliyokuwa inawataka warusi, warusi walionekana kama mabeberu na wakoloni, mataifa kama Poland (haikuwa USSR) ,Estonia, Latvia, Romania, Slovakia, Ukraine, Bulgaria, Yugoslavia, Georgia, nk yalianza kutaka uhusiano na magharibi kwasababu ya misaada ya kiuchumi, wakati huo Russia ilikuwa mufilisi na kumbuka madeni yote ya USSR yalibebeshwa Russia pekeyake kuyalipa! Na kama unakumbuka chanzo cha kuanguka na kusambaratika kwa USSR ni umaskini na madeni, ilifikia mahali urusi ilishindwa tena kui manage kiuchumi USSR, na kuiacha ianguke!
Sasa basi iweje urusi izuie mataifa huru ya ulaya mashariki kuchagua mustakabali wao?!
Kwanini Russia itumie jeshi kuumiza mataifa yanayojiamulia upande wanaoutaka?!
Jibu ni kwamba Russia pia ni beberu kama Marekani na western Europe countries!
Maana kiuhalisia ni kwamba wananchi wengi wa nchi za ulaya mashariki hawaitaki Russia maana haiwezi kuwasaidia kiuchumi, ndio maana wanakimbila magharibi angalia Yugoslavia ilivyosambaratika member wote wako magharibi Slovenia, Kosovo, Croatia, Bosnia Herzegovina, Macedonia hata Serbia itself, angalia Romania tayari ni mshirika wa NATO, sijasema kuhusu kina Estonia, Latvia, Georgia ambao Russia inajaribu kuwahujumu na Ukraine,
Ukweli ni kwamba wananchi wa nchi za former Soviet, hawaitaki Russia maana haina msaada kiuchumi, ndio maana wengi wanaandamana kupinga viongozi wenye milengo ya Russia angalia Belarus kwasasa, na nini kinatokea Kyrgyzstan,
Kuhusu klemia si kweli, huwezi kutoa ardhi yako kama zawadi kwa rafiki yako mkuu, klemia ni sehemu halali ya Ukraine tuwe serious kidogo! Ndio maana imesababisha iwekewe vikwazo na magharibi, Russia inatabia ya kunyakua ardhi ya mataifa madogo angalia kinachotokea Georgia wale waasi wa Ossetia wanataka kujiunga na Russia unalijua hilo?! Wale waasi wa Donetsk Ukraine mashariki wanaoongea kirusi walitishia kujiunga na Russia, bado kunamzozo Latvia kati ya wanaozungumza kirusi na wa Latvian halisi, achilia mbali mzozo wa Chechnya! Tabia ya Russia ni divided and isolated! (Wagawanye uwatenge).
Kwangu Russia ni Beberu tu kama Marekani na washirika wake hakuna tofauti kabisa!
Kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema:
" The west wing and Right wing belongs to Same Bird"