Mgogoro kati ya Armenia na Azerbaijan

Mgogoro kati ya Armenia na Azerbaijan

'Mtambo wa kujikinga na makombora ya Russia ya Masafa marefu ICBM (Inter-continental Ballistic Missile) unaoitwa Iron Dom.'

Nadhani Iron dome ni ya Israel kama sijakosea.
Iron dome ni short range air defence,hauwezi kupangua makombora,una deal na marocket yenye range ya kilomita 40 kurudi chini,
David sling ni long range air defence ila bado iko kwenye testing stage...
 
Ni mshirika wa kuaminika,sema hanaga papara kwenye maamuzi,,mpaka sasa kishawaita foreign ministers wa armenia na Azebenjain kule moscow na wanaelekea wanaweza kusitisha mapigano,means russia huwa hakurupuki
Mara nyingi Russia hua sio mshirika wa kuaminika sana.
 
Turkey anaunda hizo F-16 under license,
Turkey alikuwepo kstika project ya F-35,na wanaunda lile body la F-35 na sehemu zingine muhimu,
Turkey bado anaitesa ugiriki licha ya kuwa member mwenzake wa NATo na anakamata visima vya gase vya greece

Kwanza kuunda body ya F 35 bila engined ni bure, ni sawa Na kuunda body Toyota bila enginee. Hata India anaunda Ndege za urusi by licensed, marekani wakimpiga tanji uturuki hawezi kuunda tena kumbuka huu ni mkataba unaweza kuvunjwa any time! (Maana yake kuna masharti ya mkataba kwa maslahi ya marekani).

Pili Uturuki hajakamata visima vyovyote vya Gesi vya ugiriki wala kiukweli hawezi kuthubutu kufanya hivyo hasilani, anachofanya Uturuki ni kupeleka meli za kufanya utafiti wa Gesi kwenye bahari hiyo eneo ambalo linazozaniwa na Ugiriki pia hapo ndio mzozo unapoanzia (kama ulivyo mzozo wa Tanzania na malawi ziwani Nyasa), lakini Uturuki hawezi kuthubutu kushikiria kisima cha Gesi cha Ugiriki itakuwa inajitakia balaa kubwa kimataifa, kumbuka Ugiriki ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Uturuki sio mwanachama. Na anaungwa mkono sana kijeshi na Ufaransa. Pia wote Greece na Turkey ni member wa NATO. hivyo kuvamia assets za member mwenzako sidhani kama watamvumilia Uturuki.
 
Ni mshirika wa kuaminika,sema hanaga papara kwenye maamuzi,,mpaka sasa kishawaita foreign ministers wa armenia na Azebenjain kule moscow na wanaelekea wanaweza kusitisha mapigano,means russia huwa hakurupuki
Huko unakosema kukosa papara ndiko kumemfanya apoteze washirika wake, kapoteza Latvia, Estonia, Romania, Georgia na sasa kampoteza Ukraine anang'ang'ania kumforce abaki nae kwa kuunga mkono waasi wa mashariki ya Ukraine kule Donetsk na kuvamia Rasi ya Klemia eneo la Ukraine kwenye black sea na kulikalia kwa nguvu. Achilia mbali kinachotokea Belarus!

Russia kapoteza sana mkuu, hasa wakati wa Boris Yeltsin, iko wazi sana Urussi tatizo alikosa strategic plans za kufanya kuwa na ushawishi eneo hilo, kidogo ujio wa Vladimir Putin umerudisha heshima ya Russia walau kidogo hadi kuwekewa vikwazo na magharibi.
 
Russia hawezi ruhusu nchi jirani yake ikaliwe na majeshi ya US au NATO. Ndio maana baada ya Yanukovich kuondolewa na Wamarekani Russia alianzisha vita ili kuifanya Dinbass iwe free hata kama Ukraine itakarihisha majeshi ya Marekani. Marekani anajua hili ndio maana hayupo kule na rais wa sasa wa Ukraine ameamua kutambua hili.

The same case na Southern Ossetia na Abkhazia ambazo Russia alizifanya zijiondoe Georgia pale ilipotaka kujiweka karibu na US wakati inapakana na Russia. Russia alitenganisha maeneo yanayopakana nae.
Ndio maana Sweden haiwezi kabisa kujiunga na NATO wala kukaribisha majeshi au silaha za US kama meli na subs.

Kuhusu Crimea bado mwenye haki nayo ni Russia, ilikuwa ni matter of time waichukue. Kilichofanya waichukue 2014 ni pale vibaraka wa US walipoingia madarakani ambapo nao walishindwa uongozi mpaka sasa nchi inaongozwa na mchekeshaji wa zamani ambaye hakuwahi kuwa hata katibu wa mtaa. Miaka ya zamani Josef Stalin aliifanya Crimea iwe chini ya uongozi wa Ukrainian Socialist Republic ili kuraihisha maendeleo na usimamizi, baada ya dissolution ya USSR Crimea ikabaki Ukraine. Pia Russia hakuwa na warm naval base yeyote kwa vile bases zake zinaganda kwa kipindi fulani kwa mwaka ndio maana aliitaka sana Crimea ambayo haijai barafu.

Ni sawa na sasa hivi kisiwa cha Mafia kiwekwe chini ya Zanzibar ili kurahisisha usimamizi na miaka ijayo muungano uvunjike Mafia ibaki Zanzibar alafu maadui wa Tanganyika walete base yao pale na majeshi.
Hii kesi ya Crimea ni sawa na hii ya Nagorno-Kabarakh na Stalin mwenyewe aliizidisha badala ya kuitatua.
 
Ila kwenye hili naona kama Russia amemsaliti sana Armenia, na nahisi huenda hata Armenia akawaza kuachana kumtegemea Russia kama alivyofanya Georgia (T'blis), na kujiunga na kambi ya magharibi, pamoja na Ukraine (Kiev), Estonia na Latvia, bila kusahau Romania ambayo wote ni washirika wa NATO.

Maana naona Armenia (Yerevan) ataona hakuna Maana kuwa na mkataba wa ulinzi pamoja na kuwa na kambi ya Russia nchini mwake wakati Russia hampi msaada wowote wa maana kama afanyavyo Turkey (Ankara) kwa Azerbaijan (Baku).

Kwakweli Mrussi asipoangalia atajikuta anapoteza washirika wake karibia wote na kujikuta amezungukwa na kambi za magharibi (NATO) kwenye mipaka yake!
Russia hajamsaliti Armenia. Anacholenga ni kuonesha washirika wake kwamba ukikengeuka utaonja joto la jiwe kwani huyo Armenia alijikuta amekua akaanza kuondoa influence ya Russia ambaye alikuwa protector wake na kujiweka kwa US. Russia wakishirikiana na nchi hawaachi kizembe hivi.

Hapa Russia ana mahusiano na nchi zote na wala hataki mgogoro uendelee ila inaonekana hatafuti suluhisho la Nagorno-Kabarakh yeye akiwapa ceasefire anatosheka.

US mwenyewe hana cha kufaidika nacho kwa Armenia anataka mafuta ya Azeri. US hawezi mchukua Armenia akamwacha Azeri kwenye vita hii.

Turkey alianza akionekana anataka kuinua ushawishi wa ndani kama Putin alivyopata kukubalika baada ya kuichukua Crimea. Nchi zinazoongozwa na utawala wa muda mrefu hufanya hivi na viongozi wake hujuana kwa hili, ndio maana Turkey na Russia wanapinzana kule Libya ila hawana uadui.
Issue ya Syria inatambulika kuwa Turkey anataka Wakurdi wawe mbali nae hivo Russia anaelewa hili.

Tatizo linalokuja Turkey anaonekana anaitaka gesi ya Azerbaijan na anataka kuichimba kuuza Europe. Russia anamuuzia Turkey gesi ila miaka hii ununuzi umepungua ndio tunaona pale Libya na Greece kuna migogoro chanzo kikiwa ni gesi.
Turkey anataka kuwa independent kwenye energy na defence sector ila Russia haijawahi kukubali upinzani kwenye biashara ya energy. Ikijulikana hii case ya pili ndo lengo la Turkey, Russia atambadilikia mpaka tushangae.
 
Huko unakosema kukosa papara ndiko kumemfanya apoteze washirika wake, kapoteza Latvia, Estonia, Romania, Georgia na sasa kampoteza Ukraine anang'ang'ania kumforce abaki nae kwa kuunga mkono waasi wa mashariki ya Ukraine kule Donetsk na kuvamia Rasi ya Klemia eneo la Ukraine kwenye black sea na kulikalia kwa nguvu. Achilia mbali kinachotokea Belarus!

Russia kapoteza sana mkuu, hasa wakati wa Boris Yeltsin, iko wazi sana Urussi tatizo alikosa strategic plans za kufanya kuwa na ushawishi eneo hilo, kidogo ujio wa Vladimir Putin umerudisha heshima ya Russia walau kidogo hadi kuwekewa vikwazo na magharibi.
Ujue US walikuwa wanafanya kampeini kali sana kuziwini nchi ambazo zilibreak away kutoka Russia,kwa case ya Ukraine utaona marekani ndo waliorganise ile colour revolution,,na ilupofanikiwa,,mrusi akaona aichukue crimea kabla marekani hawajakita mizizi na ile sehemu ya kaskazini mwa ukraine,,ukraine akataka kujiunga na NATO lakini NATO wakaanza kumchenga baada ya warusi kuingia crimea kwani walijua watanasa katika mtego wa vita na russia,
Moaka sasa ukraine haitakaa ikubaliwe NATO
 
Russia hawezi ruhusu nchi jirani yake ikaliwe na majeshi ya US au NATO. Ndio maana baada ya Yanukovich kuondolewa na Wamarekani Russia alianzisha vita ili kuifanya Dinbass iwe free hata kama Ukraine itakarihisha majeshi ya Marekani. Marekani anajua hili ndio maana hayupo kule na rais wa sasa wa Ukraine ameamua kutambua hili.

The same case na Southern Ossetia na Abkhazia ambazo Russia alizifanya zijiondoe Georgia pale ilipotaka kujiweka karibu na US wakati inapakana na Russia. Russia alitenganisha maeneo yanayopakana nae.
Ndio maana Sweden haiwezi kabisa kujiunga na NATO wala kukaribisha majeshi au silaha za US kama meli na subs.

Kuhusu Crimea bado mwenye haki nayo ni Russia, ilikuwa ni matter of time waichukue. Kilichofanya waichukue 2014 ni pale vibaraka wa US walipoingia madarakani ambapo nao walishindwa uongozi mpaka sasa nchi inaongozwa na mchekeshaji wa zamani ambaye hakuwahi kuwa hata katibu wa mtaa. Miaka ya zamani Josef Stalin aliifanya Crimea iwe chini ya uongozi wa Ukrainian Socialist Republic ili kuraihisha maendeleo na usimamizi, baada ya dissolution ya USSR Crimea ikabaki Ukraine. Pia Russia hakuwa na warm naval base yeyote kwa vile bases zake zinaganda kwa kipindi fulani kwa mwaka ndio maana aliitaka sana Crimea ambayo haijai barafu.

Ni sawa na sasa hivi kisiwa cha Mafia kiwekwe chini ya Zanzibar ili kurahisisha usimamizi na miaka ijayo muungano uvunjike Mafia ibaki Zanzibar alafu maadui wa Tanganyika walete base yao pale na majeshi.
Hii kesi ya Crimea ni sawa na hii ya Nagorno-Kabarakh na Stalin mwenyewe aliizidisha badala ya kuitatua.
Mkuu, naona umeandika kiufuasi wa urusi sana, lakini ukweli ni kwamba baada ya kuanguka kwa Soviet (USSR), mataifa ya mashariki ya ulaya yaliyokuwa wanachama wa soviet chini ya urusi yalikuwa fukara sana, mengi yalitamani na bado yanatamani kujiunga na kambi ya magharibi ili kupata hafueni ya kiuchumi, labda kama hujui jinsi majeshi ya Russia yalivyojiondoa haraka ujerumani mashariki baada ya wananchi wakule kuanza kuwapiga kwa mawe urusi,

Baada ya kuanguka kwa USSR hakuna nchi ya ulaya mashariki iliyokuwa inawataka warusi, warusi walionekana kama mabeberu na wakoloni, mataifa kama Poland (haikuwa USSR) ,Estonia, Latvia, Romania, Slovakia, Ukraine, Bulgaria, Yugoslavia, Georgia, nk yalianza kutaka uhusiano na magharibi kwasababu ya misaada ya kiuchumi, wakati huo Russia ilikuwa mufilisi na kumbuka madeni yote ya USSR yalibebeshwa Russia pekeyake kuyalipa! Na kama unakumbuka chanzo cha kuanguka na kusambaratika kwa USSR ni umaskini na madeni, ilifikia mahali urusi ilishindwa tena kui manage kiuchumi USSR, na kuiacha ianguke!

Sasa basi iweje urusi izuie mataifa huru ya ulaya mashariki kuchagua mustakabali wao?!

Kwanini Russia itumie jeshi kuumiza mataifa yanayojiamulia upande wanaoutaka?!

Jibu ni kwamba Russia pia ni beberu kama Marekani na western Europe countries!

Maana kiuhalisia ni kwamba wananchi wengi wa nchi za ulaya mashariki hawaitaki Russia maana haiwezi kuwasaidia kiuchumi, ndio maana wanakimbila magharibi angalia Yugoslavia ilivyosambaratika member wote wako magharibi Slovenia, Kosovo, Croatia, Bosnia Herzegovina, Macedonia hata Serbia itself, angalia Romania tayari ni mshirika wa NATO, sijasema kuhusu kina Estonia, Latvia, Georgia ambao Russia inajaribu kuwahujumu na Ukraine,

Ukweli ni kwamba wananchi wa nchi za former Soviet, hawaitaki Russia maana haina msaada kiuchumi, ndio maana wengi wanaandamana kupinga viongozi wenye milengo ya Russia angalia Belarus kwasasa, na nini kinatokea Kyrgyzstan,

Kuhusu klemia si kweli, huwezi kutoa ardhi yako kama zawadi kwa rafiki yako mkuu, klemia ni sehemu halali ya Ukraine tuwe serious kidogo! Ndio maana imesababisha iwekewe vikwazo na magharibi, Russia inatabia ya kunyakua ardhi ya mataifa madogo angalia kinachotokea Georgia wale waasi wa Ossetia wanataka kujiunga na Russia unalijua hilo?! Wale waasi wa Donetsk Ukraine mashariki wanaoongea kirusi walitishia kujiunga na Russia, bado kunamzozo Latvia kati ya wanaozungumza kirusi na wa Latvian halisi, achilia mbali mzozo wa Chechnya! Tabia ya Russia ni divided and isolated! (Wagawanye uwatenge).

Kwangu Russia ni Beberu tu kama Marekani na washirika wake hakuna tofauti kabisa!

Kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema:

" The west wing and Right wing belongs to Same Bird"
 
Ujue US walikuwa wanafanya kampeini kali sana kuziwini nchi ambazo zilibreak away kutoka Russia,kwa case ya Ukraine utaona marekani ndo waliorganise ile colour revolution,,na ilupofanikiwa,,mrusi akaona aichukue crimea kabla marekani hawajakita mizizi na ile sehemu ya kaskazini mwa ukraine,,ukraine akataka kujiunga na NATO lakini NATO wakaanza kumchenga baada ya warusi kuingia crimea kwani walijua watanasa katika mtego wa vita na russia,
Moaka sasa ukraine haitakaa ikubaliwe NATO

Kwahili ni kweli kabisa nakubaliana na wewe mkuu,,, kwenye kikao kimoja kati ya magharibi na Russia, mrusi aliwaambia marekani mkataba wowote kati ya magharibi na Ukraine lazima uangalie maslahi ya Russia (yaani urusi lazima awepo) lakin marekani ilikataa ikasema Ukraine ni nchi huru haiitaji kuamuliwa na mwingine, ndio chanzo cha mzozo maana mrusi aliona maslahi yake yako hatarini. Kilichotokea ndio tunachokiona leo!

Nikweli mkuu.
 
Russia hajamsaliti Armenia. Anacholenga ni kuonesha washirika wake kwamba ukikengeuka utaonja joto la jiwe kwani huyo Armenia alijikuta amekua akaanza kuondoa influence ya Russia ambaye alikuwa protector wake na kujiweka kwa US. Russia wakishirikiana na nchi hawaachi kizembe hivi.

Mkuu hapa Armenia amekengeuka vipi?! Unajua kuwa Armenia ana mkataba wa ulinzi na Russia?!

Unajua kuwa Russia ana kambi ya Jeshi Armenia?! sasa Armenia amejiweka vipi na U.S wakati anamkataba na Russia na ana kambi ya Russia nchini kwake?!
Hapa Russia ana mahusiano na nchi zote na wala hataki mgogoro uendelee ila inaonekana hatafuti suluhisho la Nagorno-Kabarakh yeye akiwapa ceasefire anatosheka.

Ni kweli kuwa Russia ana maslahi na wote Azerbaijan na Armenia. Kwakuwa zote zilikuwa kwenye USSR pia Russia ana biashara kubwa na Azerbaijan. Lakini sidhani kama Azerbaijan itakubali kutopata eneo lao linalokaliwa na Armenia kimabavu, wala sidhani kama Armenia atakubali watu wake wachache walioko Nagorno karbakh wawe sehemu ya azer. Hapa bado kuna mtiti.
 
Mkuu hapa Armenia amekengeuka vipi?! Unajua kuwa Armenia ana mkataba wa ulinzi na Russia?!

Unajua kuwa Russia ana kambi ya Jeshi Armenia?! sasa Armenia amejiweka vipi na U.S wakati anamkataba na Russia na ana kambi ya Russia nchini kwake?!

Ni kweli kuwa Russia ana maslahi na wote Azerbaijan na Armenia. Kwakuwa zote zilikuwa kwenye USSR pia Russia ana biashara kubwa na Azerbaijan. Lakini sidhani kama Azerbaijan itakubali kutopata eneo lao linalokaliwa na Armenia kimabavu, wala sidhani kama Armenia atakubali watu wake wachache walioko Nagorno karbakh wawe sehemu ya azer. Hapa bado kuna mtiti.
Mkuu hii vita itaisha siku Nagorno-Kabarakh ikiwa chini ya Azerbaijan.

Hiyo Armenia tangu mwaka 2018 inajitenga na Russia kidogokidogo. Unasema Russia wana base kama kigezo lakini mbona US wapo Incirlik airbase na walideploy mabomu ya nuclear pale, pia wana radar station nchini umo ila bado Turkey anawageuka.

Kitu kingine huu mgogoro unafatiliwa sana kimyakimya. India walikuwa wawazi kuwa wanafatilia each and everything
 
Mkuu, naona umeandika kiufuasi wa urusi sana, lakini ukweli ni kwamba baada ya kuanguka kwa Soviet (USSR), mataifa ya mashariki ya ulaya yaliyokuwa wanachama wa soviet chini ya urusi yalikuwa fukara sana, mengi yalitamani na bado yanatamani kujiunga na kambi ya magharibi ili kupata hafueni ya kiuchumi, labda kama hujui jinsi majeshi ya Russia yalivyojiondoa haraka ujerumani mashariki baada ya wananchi wakule kuanza kuwapiga kwa mawe urusi,

Baada ya kuanguka kwa USSR hakuna nchi ya ulaya mashariki iliyokuwa inawataka warusi, warusi walionekana kama mabeberu na wakoloni, mataifa kama Poland (haikuwa USSR) ,Estonia, Latvia, Romania, Slovakia, Ukraine, Bulgaria, Yugoslavia, Georgia, nk yalianza kutaka uhusiano na magharibi kwasababu ya misaada ya kiuchumi, wakati huo Russia ilikuwa mufilisi na kumbuka madeni yote ya USSR yalibebeshwa Russia pekeyake kuyalipa! Na kama unakumbuka chanzo cha kuanguka na kusambaratika kwa USSR ni umaskini na madeni, ilifikia mahali urusi ilishindwa tena kui manage kiuchumi USSR, na kuiacha ianguke!

Sasa basi iweje urusi izuie mataifa huru ya ulaya mashariki kuchagua mustakabali wao?!

Kwanini Russia itumie jeshi kuumiza mataifa yanayojiamulia upande wanaoutaka?!

Jibu ni kwamba Russia pia ni beberu kama Marekani na western Europe countries!

Maana kiuhalisia ni kwamba wananchi wengi wa nchi za ulaya mashariki hawaitaki Russia maana haiwezi kuwasaidia kiuchumi, ndio maana wanakimbila magharibi angalia Yugoslavia ilivyosambaratika member wote wako magharibi Slovenia, Kosovo, Croatia, Bosnia Herzegovina, Macedonia hata Serbia itself, angalia Romania tayari ni mshirika wa NATO, sijasema kuhusu kina Estonia, Latvia, Georgia ambao Russia inajaribu kuwahujumu na Ukraine,

Ukweli ni kwamba wananchi wa nchi za former Soviet, hawaitaki Russia maana haina msaada kiuchumi, ndio maana wengi wanaandamana kupinga viongozi wenye milengo ya Russia angalia Belarus kwasasa, na nini kinatokea Kyrgyzstan,

Kuhusu klemia si kweli, huwezi kutoa ardhi yako kama zawadi kwa rafiki yako mkuu, klemia ni sehemu halali ya Ukraine tuwe serious kidogo! Ndio maana imesababisha iwekewe vikwazo na magharibi, Russia inatabia ya kunyakua ardhi ya mataifa madogo angalia kinachotokea Georgia wale waasi wa Ossetia wanataka kujiunga na Russia unalijua hilo?! Wale waasi wa Donetsk Ukraine mashariki wanaoongea kirusi walitishia kujiunga na Russia, bado kunamzozo Latvia kati ya wanaozungumza kirusi na wa Latvian halisi, achilia mbali mzozo wa Chechnya! Tabia ya Russia ni divided and isolated! (Wagawanye uwatenge).

Kwangu Russia ni Beberu tu kama Marekani na washirika wake hakuna tofauti kabisa!

Kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema:

" The west wing and Right wing belongs to Same Bird"
Kuhusu Crimea nilichosema siongezi ni jukumu lako kukubali au kukataa. Ungerejea mifumo ya uongozi wa USSR ilivyokuwa usingepinga. Nchi zilizokuwa USSR na Yugoslavia zilipigana baada ya kuvunjika muungano kwa sababu zilezile.
Leo hii huwezi chukua kisiwa cha Mafia ukakiweka chini ya Zanzibar ukiamini muungano utadumu, kisha muungano uvunjike Zanzibar ikatalie kisiwa hicho.
Kwa mfano huu: Mafia- Crimea, Zanzibar- Ukraine, Tanganyika- Russia. Badae Tanganyika ikitwaa kisiwa chake uiite beberu.

Russia si kuwa analazimisha mahusiano na nchi za zamani za Soviet block. Yeye asichopenda ni kuweka base za NATO na US kwenye nchi hizo. Huwezi kuweka base ya Russia nchini Mexico US wakakubali. US hawezi kubali Russia kuivamia Canada hata kama isingekuwa NATO. US huyuhuyu ndiye aliweka naval blockade pale Cuba ilipohifadhi makombora ya USSR wakati huo USSR ikataka makombora yaliyoko mpakani naye yaondolewe.

Kitendo cha majirani za Russia kuwa puppets wa NATO au US hakikubaliki kwake. Huu sio msimamo wangu wa kuitetea Russia bali ni sera zao zinavyosomeka hivo. Na sikubaliani na occupation ya Donbass, kuna mahala ulisema Russia hawaaminiki wakati NATO hii hapa ilishindwa kuitetea Ukraine member wao.
 
Ujue US walikuwa wanafanya kampeini kali sana kuziwini nchi ambazo zilibreak away kutoka Russia,kwa case ya Ukraine utaona marekani ndo waliorganise ile colour revolution,,na ilupofanikiwa,,mrusi akaona aichukue crimea kabla marekani hawajakita mizizi na ile sehemu ya kaskazini mwa ukraine,,ukraine akataka kujiunga na NATO lakini NATO wakaanza kumchenga baada ya warusi kuingia crimea kwani walijua watanasa katika mtego wa vita na russia,
Moaka sasa ukraine haitakaa ikubaliwe NATO
Akili zangu ni kama zimekopi kwako. Nakubali 93%
 
Russia angeumaliza mgogoro haraka kama Turkey asingejihusisha,,,hivi sasa inabidi aende taratibu maana hataki kumuudhi Turkey,
Azbenjain wanasaidiwa na Turkey na israel,
Armenia angeweza kusaidiwa na Russia na pengine iran,ila sasa Russia na iran hawataki kumuudhi Turkey,
Armenia ni nchi ya ordhox christian,Azebenjain ni secular shia country,
Turkey aliwahi kuwa mtawala maeneo hayo enzi za ottoman empire,,hivyo anataka kurudisha influence yake huko
Ndo Putin kasema kwamba hataki kumuudhi turkey?!
 
Russia angeumaliza mgogoro haraka kama Turkey asingejihusisha,,,hivi sasa inabidi aende taratibu maana hataki kumuudhi Turkey,
Azbenjain wanasaidiwa na Turkey na israel,
Armenia angeweza kusaidiwa na Russia na pengine iran,ila sasa Russia na iran hawataki kumuudhi Turkey,
Armenia ni nchi ya ordhox christian,Azebenjain ni secular shia country,
Turkey aliwahi kuwa mtawala maeneo hayo enzi za ottoman empire,,hivyo anataka kurudisha influence yake huko
Kwa hiyo Iran anasimama dhidi ya shia wenzake!
 
Iran akisimama na Azerbaijan maana yake anaungana mkono na makundi ya Kissuni ya upiganaji yaliyoletwa na Turkey ila yanapigana na vikosi trained na Iran na yako anti-Assad.

Israel hashiriki vita hii ila alitokea kuwa kawauzia Azerbaijan silaha kama ambavyo Russia iliwauzia.
Iran hana tatizo kushirikiana na Wakristo ila huwezi kumuweka pamoja na Wassuni. Pia halazimiki kushiriki vita hii
 
Kuhusu Crimea nilichosema siongezi ni jukumu lako kukubali au kukataa. Ungerejea mifumo ya uongozi wa USSR ilivyokuwa usingepinga. Nchi zilizokuwa USSR na Yugoslavia zilipigana baada ya kuvunjika muungano kwa sababu zilezile.
Leo hii huwezi chukua kisiwa cha Mafia ukakiweka chini ya Zanzibar ukiamini muungano utadumu, kisha muungano uvunjike Zanzibar ikatalie kisiwa hicho.
Kwa mfano huu: Mafia- Crimea, Zanzibar- Ukraine, Tanganyika- Russia. Badae Tanganyika ikitwaa kisiwa chake uiite beberu.

Russia si kuwa analazimisha mahusiano na nchi za zamani za Soviet block. Yeye asichopenda ni kuweka base za NATO na US kwenye nchi hizo. Huwezi kuweka base ya Russia nchini Mexico US wakakubali. US hawezi kubali Russia kuivamia Canada hata kama isingekuwa NATO. US huyuhuyu ndiye aliweka naval blockade pale Cuba ilipohifadhi makombora ya USSR wakati huo USSR ikataka makombora yaliyoko mpakani naye yaondolewe.

Kitendo cha majirani za Russia kuwa puppets wa NATO au US hakikubaliki kwake. Huu sio msimamo wangu wa kuitetea Russia bali ni sera zao zinavyosomeka hivo. Na sikubaliani na occupation ya Donbass, kuna mahala ulisema Russia hawaaminiki wakati NATO hii hapa ilishindwa kuitetea Ukraine member wao.
Ukraine ni member wa NATO Sikh hizi!?
Nilikuwa sins habari!
 
Back
Top Bottom