Mgogoro kati ya Armenia na Azerbaijan

Mgogoro kati ya Armenia na Azerbaijan

Sijafatilia sana ila hizi systems za miaka ya 1980s uko hazikuja kipindi cha smart munitions zikitawala. Kama hizo loitering munitions zimekuwa popular kwenye mapigano haya tu.

Designers wa zamani hawakuwa na idea kwa njia za siku hizi za kushambulia. Nakumbuka ile mwanzo mwa UAE kupeleka silaha Libya walipeleka Pantsir air defence system zikapigwa na droke za Bayraktar BTB za Turkey. Nikaanza kuzichukulia poa ila kumbe zile zilikuwa ni first batch ambazo jeshi la Russia lilizikataa.

Baadae nikajiuliza mbona pale Khmeimim/Hmeimim airbase kule Latakia drones ndogo sana zaidi ya Bairaktar zilikuwa zinadondoshwa tena zikija kwa mkupuo. Nilifatilia nikaona wanatumia layered air defence. Pantsir na Strela kwa low level flight na low range. Medium to high zipo kina S-350 ni latest, long range ndo hizi S-300, S-400 na S-500 ijayo.

Systems kubwa haziwezi ona target ndogo. Unakuta inaona 300km away ila haiwezi kabisa kuona 3km away inategemea na radar imekaaje. Ndo maana kule Saudi Arabia drones zilizogungwa gundi za karatasi ziliharibu mitambo inayolindwa na Patriot. Wiki jana kuna mashambulizi kama matatu yamezuiwa na Saudi Arabia kwa vile washajua threat ilivyo.
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi murua usio na ushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kuwa na mahusiano ya kidipromasia ndio kuwa marafiki ?
Mbona Iran na Saudia wa uhusiano wa kibalozi lakini ni maadui wakubwa?
Mbona Marekani na Urusi wana uhusiano wa kibalozi lakini ni maadui? jaribu kutumia akili basi.
Erdogan anajifanya anaifokea Israel ili kuwarizisha raia wa uturuki ambao karibia wote ni waislamu, lakini nyuma ya pazia ni rafiki wa Israel.
Uturuki ilikua nchi ya kwanza kuikubali Israel tangu 1949. Wanashirikiana katika secta nyingi Sana ujasusi, uchumi, silaha, gesi na vitu mbali mbali.
Uturuki anauziwa cutting edge weapons na US +WESTERN EUROPE sababu wamemuamini kuwa sio tishio kwa Israel.
Juzi hapa aliagiza ndege nyingi Sana za F-35 na alikua aletewe kama sio kuchukua S-400.
 
Ninacho kiona hapa na bishana na mbumbu hivi unajua maana ya nchi rafiki?
Nimeshakwambia Uturuki na Israel ana uhusiano wa kawaida kama alionao kwa tz,kenya.
Ndio maana nimekutolea mfano wa urusi na marekani au Iran na saudia au Pakistan na India hizo nchi nilizo kutaja ni maadui wakubwa tena sana lakini bado Zina uhusiano wa kibiashara na kitekinorojia kati yao, kwann isiwezekane kwa Uturuki na Israel.
Uturuki sio tishio kwa Israel na pia sio rafiki wa Israel bali wana uhusiano wa kawaida wa kibiashara na kibalozi.
Nakingine umesema sijui Erdogan anapiga kelele ili kuwaridhisha raia wake, kwahiyo waislam wameingia Uturuki baada ya Erdogan kuingia madarakani?
Mbona hizo kelele hazikupingwa kipindi cha nyuma?
Uturuki kwa sasa sio tishio kwa Israel lakini inaelekea kuwa tishio kubwa kwa Israel iwapo wana siasa aina ya Erdogan wata endelea kuitawala Uturuki.
 
Kwani kuwa na mahusiano ya kidipromasia ndio kuwa marafiki ?
Mbona Iran na Saudia wa uhusiano wa kibalozi lakini ni maadui wakubwa?
Mbona Marekani na Urusi wana uhusiano wa kibalozi lakini ni maadui? jaribu kutumia akili basi.
Turkey sio tishio kwa Israel, ni partner wale Wana ushirika mkubwa Sana. Usidanganywe na kelele za erdogan pale huwa anawazubaisha raia wa uturuki tu.
 
Ninacho kiona hapa na bishana na mbumbu hivi unajua maana ya nchi rafiki?
Nimeshakwambia Uturuki na Israel ana uhusiano wa kawaida kama alionao kwa tz,kenya.
Ndio maana nimekutolea mfano wa urusi na marekani au Iran na saudia au Pakistan na India hizo nchi nilizo kutaja ni maadui wakubwa tena sana lakini bado Zina uhusiano wa kibiashara na kitekinorojia kati yao, kwann isiwezekane kwa Uturuki na Israel.
Uturuki sio tishio kwa Israel na pia sio rafiki wa Israel bali wana uhusiano wa kawaida wa kibiashara na kibalozi.
Nakingine umesema sijui Erdogan anapiga kelele ili kuwaridhisha raia wake, kwahiyo waislam wameingia Uturuki baada ya Erdogan kuingia madarakani?
Mbona hizo kelele hazikupingwa kipindi cha nyuma?
Uturuki kwa sasa sio tishio kwa Israel lakini inaelekea kuwa tishio kubwa kwa Israel iwapo wana siasa aina ya Erdogan wata endelea kuitawala Uturuki.
Acha ubishi fuatilia usharika wa turkey na Israel utagundua ukweli.

Turkey hajawai kua adui wa Israel tangu 1949 na ndo nchi ya kwanza kuikubali Israel.
 
Hapana mkuu mwaka 2018 walifanya mazungumzo ya kurudisha ubarozi lakini walikubalia kufungua kwanza barozi ndogo.
Can you prove this claim??
Kuwa Saudi Arabia wamekubaliana na Iran wafungue balozi ndogo mwaka 2018.
 
Mkuu hizi taarifa ni za kweli?
Ndio ni za kweli na nilizisikiliza kwenye moja wapo ya taarifa ya habari ya DW Swahili mwaka 2018 kwenye mwezi wa 3 kama sikosei na hayo ndio yalikuwa makubaliano yao baada ya mazungumzo na sababu ya kufungua kwanza ubalozi mdogo ilikuwa ni Saudia kuufanyia ukarabati jengo lake la ubalozi wake lililo chomwa moto na waandamanaji.
 
Israel na Turkey sio marafiki.fatilia operation waliyoifanya Jeshi la Israel (Gaza flotilla raid) mwaka 2010 ndo utajua Israel wala hana na urafiki na Mturuki
 
Israel na Turkey sio marafiki.fatilia operation waliyoifanya Jeshi la Israel (Gaza flotilla raid) mwaka 2010 ndo utajua Israel wala hana na urafiki na Mturuki
Tatizo watu wana fananisha ushirika wa kawaida wa kibiashara na kibalozi na Urafiki
Uturuki na Israeli uhusiano wao kwa sasa hauko sawa hata kidogo kama ni mfatiriaji wa siasa za ulimwengu kuna mambo mengi mno wanatofautina.
 
Ni "grey" area hii lakini taarifa zilizopo za kijasusi ni kwamba waasi wa Syria na hata kutoka Libya ambao wanaungwa mkono na CIA wapo wakipigana mjini Karabah.

Kijiografia Armenia imesimama kati ya bara ya Ulaya, Bahari Nyeusi na mashariki ya kati.

Pia eneo hilo ipo sehemu ijulikanayo kama Caucasus ambayo ni sehemu ilosheheni mafuta na hapo ndipo mataifa makubwa ya kibeberu ndipo yanapopazingira na kumezea mate.

Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron amethibitisha kuwa wanajeshi wa kukodi kutoka Syria na Libya ambao ni wanamgambo wa kiislam wanakodiwa kuipigania Azerbaijan.

Huenda Ufaransa akaingia kuwasaidia Armenia ambao kiukweli hawana nguvu sana kwenye hii.

Hawa wanapitia Uturuki na moja ya stratejia na Marekani katika vita kwenye eneo la mashariki ya kati ni kutoa mafunzo na silaha kwa waasi wa Syria.

Taarifa zingine za kijasusi ni kwamba Azerbaijan ni sehemu ya maandalizi ya kivita yanayofanywa na Marekani na Israeli.

Russia tayari kagundua kwamba makombora ambayo yametupwa kule Armenia kutokea Azeri yametengenezwa na kampuni ya Azad System ambayo ni ya Azerbaijan.

Kampuni hiyo inashirikiana na kampuni ya Israeli ya Aeronautics ambayo inasaidia kiteknolojia.

Hivyo hii vita mlengwa hapo ni Russia kwa sababu alikwishawafyekelea mbali waasi kule Syria lakini akasahau kwamba wataingia Urutuki na kuhifanyiwa.
Unavyosema mlengwa ni Russia inamaanisha hiyo vita ni mbinu ya kuivamia Urusi kupitia Armenia?

Au wanataka kuanzisha vita mpya mpakani mwa Urusi (itakayoihusisha pia Urusi hapo mbeleni) baada ya Urusi kuwashinda kule Syria?
 
Wakifanikiwa kuigia maeneo hayo watataka kuwa na mitambo yao ambayo itawachunguza Russia mpaka sebuleni.

Hivyo kuondoa kadhia hiyo Russia hapendi ujinga huo.
 
Tatizo turkey iko very strategically located na ndo maana kina Russia,iran,marekani wanamwendea kwa tahadhari sana,
Mfano Russia anauza mafuta ,gase turkey via pipelines,vilevile turkey ni lango la manowari za russia kutoka black sea via istabull kuja Medditerania ocean,,Turkey akiwafungia,Russia anapoteza Navy port zake za warm water zilizoko black sea maana zitakuwa useless,
Kwa upande wa marekani,turkey ni ya pili kwa ukubwa wa jeshi ndani ya NATO baada ya US,,marekani anahofia akimuudhi turkey,atahamia kambi ya russia na ulaya yote itakuwa at the mess of Russians,
Ukija kwa iran,,biashara nyingi zinapitia turkey,inshort turkey haheshimu vikwazo vya marekani dhidi ya iran,kwani uturuki wanafanya biashara na iran ya mabilion,
Wote hao Turkey kawashika,hawafurukuti,ndo naana anafanya anavyotaka syria,libya na huko armenia
Aisee hatari sana
 
Nadhani unaweza kujibu kwa uelewa wako, ndivyo unavyoelewa wewe, sasa usilazimishe nami nifikiri kwa kiwango cha uelewa wako mkuu, na kudai ni "ubishi" ingekuwa wote tunauelewa mmoja hata Maendeleo yangechelewa kufika.

Hoja yako unasema ni eneo la Russia sababu mwaka 1954 walilikabidhi kwa Ukraine kutokana na urahisi Wa utawala, hutaki kuona kuwa Russia walilivamia (occupied) wakalimega (segregated) na kulitenga (annexed)) na Ukraine baada ya kulivamia eneo hilo! Upeo huo hujafikiria bali umeanzia hapo kwenye sababu ya kulikabidhi kwa Ukraine! Kwahiyo ndugu South Africa kuivamia Namibia na kuja kuipa Uhuru 1990 inahalalisha kuwa eneo la south Africa?! Uingereza kuitawala Zanzibar na kuipa Uhuru 1963 kisha ikirudi na kuivamia ni halali? Klimea ilitawaliwa na nchi nyingi kuanzia Roma, ugiriki, Ufaransa enzi za Napoleon, Uturuki enzi za Ottoman, ujerumani enzi za Adolf Hitler, ikaja kukombolewa na Russia aliyekuwa mvamizi wake toka miaka ya 1700 kisha Mwaka huo 1954 ilirudishwa kwa Ukraine kama eneo lake halali.

Na ndio maana dunia nzima inatambua Klimea ni eneo la Ukraine halali, mpaka Leo hii hakuna nchi iliyotangaza kutambua unyakuzi huo Wa Russia klimea, hata Umoja Wa Mataifa umekataa kutambua hilo, Ramani zote Mpya zinazotoka sasa bado zinaonyesha kuwa klimea ni eneo la Ukraine.

Nimewauliza ina maana UN na wanadiplomasia wote hawajui kuwa klimea lilikuwa eneo la Russia isipokuwa nyie humu Jamiiforum?!

Tuache ushabiki na mapenzi binafsi tusome historia, mvamizi hawezi kuwa mmiliki kamwe.
Mkuu unaposema (unapoandika) "mvamizi hawezi kuwa mmiliki kamwe" ...unazungumziaje kisiwa cha Mayotte ambacho bado kipo chini ya himaya ya Ufaransa, je utasema Ufaransa sio mmiliki halali? (Kumbuka wakazi wa huko wanajiona wao ni Wafaransa zaidi kuliko Wacomoro)

Vipi kisiwa cha Samoa ambacho kipo chini ya Marekani ina maana Marekani sio mmiliki halali?...Usisahau hichi kisiwa kina mwakilishi kwenye bunge la Marekani japo haruhusiwi kupiga kura (kama nimekosea nirekebishwe).

Ukiangalia hiyo mifano hapo juu na ukiangalia kadhia ya Crimea ambapo raia wa eneo husika kwa hiyari yao wameamua kujiunga na Urusi (kupitia kura ya maoni) kwanini umuone Urusi kama mvamizi?
 
Back
Top Bottom