Mkuu unaposema (unapoandika) "mvamizi hawezi kuwa mmiliki kamwe" ...unazungumziaje kisiwa cha Mayotte ambacho bado kipo chini ya himaya ya Ufaransa, je utasema Ufaransa sio mmiliki halali? (Kumbuka wakazi wa huko wanajiona wao ni Wafaransa zaidi kuliko Wacomoro)
Vipi kisiwa cha Samoa ambacho kipo chini ya Marekani ina maana Marekani sio mmiliki halali?...Usisahau hichi kisiwa kina mwakilishi kwenye bunge la Marekani japo haruhusiwi kupiga kura (kama nimekosea nirekebishwe).
Ukiangalia hiyo mifano hapo juu na ukiangalia kadhia ya Crimea ambapo raia wa eneo husika kwa hiyari yao wameamua kujiunga na Urusi (kupitia kura ya maoni) kwanini umuone Urusi kama mvamizi?
>Tukiweka ubishi pembeni usio hata mantiki yoyote kama jamaa hapo juu mshabiki wa Russia, lakini kashindwa kunijibu swali rahisi sana. Kwanini umoja wa mataifa hawatambui klemia kuwa ni sehemu ya Russia?!
* Ina maana umoja wa mataifa wanadiplomasia wote wale hawajui historia ya klemia isipokuwa yeye?! Swali hili najua limemzidi umri, amelikwepa sana!
*Mayote , Samoa , Marshall island , Falklands islands islands na Caledonia (ya ufaransa) ambayo juzi hapa imepiga kura kwa mara ya tatu ya kujitenga na ufaransa, lakini walowezi wa ufaransa wazungu (settlers) wamepiga kura kubaki kuwa milki (koloni) la ufaransa. Dhidi ya wazawa wenye asili ya nchi hiyo (natives) ambao wanapigania Uhuru wao!
*Kiuhalisia hakuna hasiyejua kuwa Mayote ni sehemu ya Comoro pamoja na Ngazija na Nzuani, hakuna asiyejua jinsi ufaransa inavyohujumu makoloni yake kwa kusupport mapinduzi ya kijeshi na civil war ili kulinda maslahi yake (kumbuka Mapinduzi ya mara kwa Mara ya Comoro), yaliyokuwa makoloni karibu yote ya ufaransa hayana amani ukilinganisha na yaliyokuwa makoloni ya mwingereza: kwanini?!
Angalia kuanzia ivory coast, central Africa Republic, Congo Brazzaville, Cameroon, Niger, Mali, Burkina Faso, T'Chad, Algeria, Mauritania, Gabon hata Comoro yenyewe!
Sera ya ufaransa ya kuwalinda madikteta kama wakina Omar bongo wa Gabon, Franciour Bozize wa afrika ya kati, sise wa Mali, Denis Swaso Ngweso wa Congo Brazzaville, Canary Azari Athuman wa Comoro, hata wakina Mobutu Seseseko kukubenga wa Zabanga wa Zaire ya zamani (DRC) japo ilitawaliwa na Belgium.
Na dikteta (Imla) au kibaraka huyo (puppet) akienda kinyume na maslahi ya ufaransa basi utolewa haraka sana! Mayotte ni eneo halali la Comoro ambalo beberu wa kifaransa kwa kufanya hila wamelimega na kuendesha kura ya kishenzi kama kule Caledonia (Pacific) , ndio maana umoja wa afrika (AU) bado unatambua eneo hilo kama sehemu ya halali ya Comoro. Kama ilivyofanywa Klemia na Russia aliivamia kijeshi na yeye mwenyewe akaendesha kura ya danganya toto na kudai wakazi wa klemia wameamua kujitenga, yaani unavamia eneo kijeshi kisha wewe mwenyewe mvamizi ndio unapanga na kusimamia uchaguzi hapo unategemea mshindi atakuwa nani?! Mchezaji wewe, Referee wewe mshindi atakuwa nani?! Wanasema Mbuzi wa bwana Heri amekula shambani kwa bwana Heri, Hakimu bwana Heri, basi yote Heri,,,,,
>Ni kama Mayote!
Hivi ufaransa au marekani inaweza kukubali eneo lake lijitenge na nchi yake?! Tuseme ukweli bila unafiki wala ushabiki?! Kwasheria za marekani kujaribu tu kujitenga ni uhaini, na adhabu ya uhaini ni kifo! Ndio kunyongwa hadi kufa! Marekani walipiga wao kwa wao vita vya wenyewe kwa wenyewe wakizuia eneo la kusini lisijitenge na Marekani. Russia alipigana na Chechnya na Grozny kufa na kupona kuzuia eneo hilo lisijitenge kutoka kwake.
Lakini sisi mataifa maskini wanatufanyia mizengwe na hujuma nyingi kutugawanya na kututawala kwaajili ya maslahi yao! Mayotte ni eneo halali la Comoro (Moroni), pamoja na visiwa vya Mwali na Zwani. Lililonyakuliwa kama klemia.
Maeneo kama haya ukifuatilia kwa undani utagundua ni ubeberu tu, fuatilia visiwa vya Diego Garsia, vilivyopo bahari ya Hindi ambavyo vilitwaliwa kwa mabavu na Uingereza na kuweka kambi zake za kijeshi pale ambapo kwasasa wakazi wake wanapigania Uhuru wake!
Fuatilia visiwa kama Marshall islands kule pasific, visiwa kama Caledonia kule karibu na Australia, visiwa kama Samoa, visiwa vya Falkland kule Argentina (islas malvinas), hata kisiwa cha Marekani cha Puerto Rico kule bahari ya Caribbean (kwasasa wakazi wake wengi wenye asili ya uhispain wanataka kujitenga na marekani na kujipatia Uhuru wao!
Bado narudia mkuu,,, mvamizi ni beberu tu hawezi kamwe kuwa mmiliki hata akae miaka mia nane!