Kama eneo ni La Azerbaijan si UN Itoe tamko kuwa Armenia waache Hilo eneo mara moja.
Kwanini kigugumizi wakati jambo liko wazi.
Trump anajifanya anapenda Amani kwann asiweke vikwazo kwa Armenia mpaka waache eneo la Azeri.
##DOUBLE STANDARDS ##
Mkuu msemayo ni kweli kabisa , eneo ni la Azerbaijan tangu enzi na enzi, lakini huu mzozo una utata sana mkuu sio rahisi hivyo,
Kwanini?!
Kwasababu jamii ya Armenians wamepitia mateso makubwa sana, waliuawa kinyama sana enzi za Ottoman empire ya Uturuki, pia wakauawa tena na Uturuki katika vita kuu ya kwanza ya dunia ambapo Uturuki iliiunga mkono ujerumani.
Uturuki walifanya mauaji ya kimbari na kuwaua wa Armenia wengi sana na kukwapua eneo lao, kama wafanyavyo Leo kwa Wakurds (pia Iraq, Iran na Syria zinawafanyia hivyo) kama kabila la Yazid linavyo shambuliwa na kuangamizwa huko Iraq, kama Watutsi walivyouawa kinyama katika mauaji ya kimbari ( Genocide) miaka ya 1994.
Najua unafahamu mzozo wa ufaransa na Uturuki baada ya bunge la ufaransa kupiga kura ya kutambua mauaji ya waarmenia miaka ya 1922 kama mauaji ya halaiki.
Sasa kwamfano unadhani watutsi watakubali kuona jamii yao (kabila lao linaangamizwa au kunyanyaswa iwe mashariki ya Kongo, Burundi au penginepo alafu wakakaa kimyaa na kuangalia tu mkuu?!
Unaona jinsi Kagame anavyounga mkono watutsi kupindua serikali ya wahutu kule Burundi, na kuwaunga mkono watutsi kule goma, Kivu ya kaskazini na uvira,
Vivyo hivyo Armenia ina waunga mkono ndugu zao au jamaa zao wa kabila lao walioko Nagorno- Karbakh ambao ni wachache (minority) dhidi ya wa Azeri (majority) usisahau pia kuhusu dini hapa!
Na dunia inatambua manyanyaso waliyopitia wa Armenians dhidi ya Waturuki kwa kuuawa kikabila karibu watokomee mbali na kufutika katika uso wa dunia, hivyo nadhani dunia inawaangalia wa Armenians kama victims zaidi na kuwaonea huruma dhidi ya wa Azeri, kama ilivyo kwa Watutsi na wahutu.
Mzozo huu una historia ndefu sana kaka, sio wa juzi au Jana tangu enzi za Ottoman empire mpaka Leo! Unaonekana pia una sura ya kikabila na kidini, na hapo ndio tatizo linapoanza!