BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,886
Posted Date::10/27/2007
Mgodi wa Bulyanhulu wafukuza wafanyakazi 700
*Watakiwa kuondoka mgodini kuanzia leo
*Wenye mafao kuyakuta katika akaunti zao
Na Julieth Kulangwa
Mwananchi
WAFANYAKAZI zaidi ya 700 wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Wilayani Kahama wamefukuzwa kazi kuanzia leo kwa kushiriki katika mgomo.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka mgodini hapo, hadi jana idadi ya wafanyakazi zaidi ya 700 walikuwa tayari katika orodha ya kuachishwa kazi baada ya jopo la ukaguzi kuhusu nani alishiriki katika mgomo kufanya kazi yake.
"Hapa tuna wafanyakazi wengi, wanafikia zaidi ya 2,000 hivyo hatuoni umuhimu wa kukaa na watu wasiofuata taratibu na sheria," kilitueleza chanzo chetu cha habari na kuongeza;
"Tumejitahidi kukaa nao na kuwataka kufuata taratibu. Awali walionyesha kukubali lakini wakabadilika baadaye. Kutokana na wao kutotaka suluhu hatuoni umuhimu wa kuwa nao tena."
Chanzo chetu kilifafanua pia kuwa, wafanyakazi watakaopata barua za kuachishwa kazi watatakiwa kuondoka mgodini na wale wanaotakiwa kulipwa mafao kwa mujibu wa taratibu watapata mafao hayo katika akaunti zao za benki.
"Kilichobakia ni hicho, wataondoka na kama kuna mafao watayachukua benki na sio vinginevyo. Tumejitahidi sana ili tusifikie hapa lakini wafanyakazi wameonyesha kutothamini hata umuhimu wa kazi zao. Kilichobakia ni kuwa tutatangaza kazi hizo ili waombaji wapya wafanye hivyo," chanzo chetu kilifafanua.
Oktoba 17, 2007 wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu walianza mgomo majira ya asubuhi kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa mgodi huo kutekeleza makubaliano baina ya uongozi na Chama cha Wafanyakazi wa Madini na Ujenzi (Tamico) tawi la Bulyanhulu.
Malalamiko hayo yalikuwa pamoja na utekelezwaji wa makubaliano ya kuondoa askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) ndani ya eneo la mgodi huo, kwa kuwa kwa kuwepo kwa kikosi hicho katika eneo hilo kunawafanya wao na familia zao kuishi kwa hofu.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na uongozi wa Barrick, mgomo huo ulianza baada ya Tamico kuueleza uongozi wa mgodi huo juu ya adhma ya kuanza rasmi kwa mgomo huo jana, baada ya kutoona utekelezaji wa makubaliano waliyofikia.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa uongozi ulilazimika kujibu barua hiyo na kuwashauri wafanyakazi hao kutogoma, kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria na utaratibu na kwa kufanya hivyo uongozi huo utalazimka kuchukua hatua kali kwa maslahi ya kampuni ya Barrick.
Hata hivyo taarifa hiyo ilieleza kuwa uongozi wa Barrick upo tayari kuendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo kwa njia ya mazungumzo hadi kuhakikisha kuwa yanamalaizika.
Lakini hili haliwezi kufanyika iwapo wafanyakazi wanaendelea na mgomo, makubaliano yetu yalikuwa wazi kuwa tutaendelea kufanya mazungumzo hatua kwa hatua hadi tutakapoyapatia ufumbuzi kwa pande zote, ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Hata taarifa hiyo ya Barick ilieleza kuwa uongozi umekuwa ukiendelea kuwaomba wafanyakazi wote kuendelea na kazi kwa mujibu wa utaratibu na kuahidi kuendelea kujali mikataba baina yake na wafanyakazi wote waliogoma.
Mgodi huo wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya Barrick Gold Tanzania limited ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini, una wafanyakazi takribani 1971 wakiwemo raia wa kigeni 178.
Kati ya hao wafanyakazi 90 wako kwenye menejimenti waliobaki wapo kwenye ufundi uendeshaji na utawala.