Mara: Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu CATA MINING warejesha mgomo, walala ofisini wakisubiri mshahara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,998
12,351
4464f1dd-8ca3-4a4d-a896-ace0b4d62648.jpeg

d8994a3a-f77d-4042-8f98-757836ddc6ae.jpeg

bec7a849-7902-4ffa-8649-caf699dfaaee.jpeg

Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu CATA MINING ulioko Kijiji Katalyo, Wilaya ya Butiama wamerejea kwenye mgomo na wakulala ofisini wakishinikiza Mwekezaji wa Mgosi kulipwa mshahara na malimbikizo, ikiwa ni wiki moja tu tangu walipositisha mgomo baada ya kuahidiwa kuwa watalipwa Januari 11, 2024.

Awali wapogoma Afisa Rasilimali Watu (HR) wa Mgodi wa Cata Mining, Richard Bendera aliiambia JamiiForums kuwa “Wanadai mishahara ya miezi miwili, tumewaahidi kuwalipa Januari 11 (2024), kulitokea changamoto kadhaa ikiwemo mvua na hivyo uzalishaji kupungua pia kulikuwa na marekebisho ya kiufundi.”

Inadaiwa mbali na Mishahara Wafanyakazi hao wanadai mishahara yao imekuwa ikikatwa makato kwa ajili ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) lakini makato hayo hajayawasilishwa NSSF kwa miaka saba na kila wakifuatilia NSSF Mara.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Wafanyakazi wa Mgodi huo, kuingia mgogoro na mwajiri wao, Mwaka 2023, walianzisha mgomo kama huu kushinikiza walipwe madeni ya mishahara ya miezi mitatu Julai, Agosti na Mwezi Septemba.

Pia soma
- Wafanyakazi mgodi wa CATA Mining Mara, waanza mgomo kushinikiza kulipwa mishahara, michango NSSF

- Mara: Uongozi Mgodi wa Cata Mining wasema utawalipa Wafanyakazi wake waliogoma kwa kutolipwa mishahara
 
Inauma sana kukosa haki yako ...Kama nyaraka umeshawasilisha za maombi ila wapi...Mbaya wafanyakazi wengine wamepewa haswa watu wa juu ila hawa wenye mishahara ya chini ni changamoto.
 
Back
Top Bottom