MGIMWA: Kodi ya simu kutobadilika

MGIMWA: Kodi ya simu kutobadilika

mawenge

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2012
Posts
286
Reaction score
71
WAZIRI wa Fedha, William Mgimwa,amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.

Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko.

Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.

"Wananchi wenyewe wanalalamikia ukosefu wa huduma na baada ya Serikali kupitia na kufanyia kazi changamoto hizo, imeridhia kodi hizo… wanakuja watu wanalalamika," alisema.

Alisisitiza kuwa ongezeko la kodi kwa huduma za intaneti, ni kwa ajili ya kuboresha mfumo wa elimu ambao unalalamikiwa mara kwa mara.

Mgimwa alisema ulipaji kodi unatokana na aina ya biashara na mapato na kutaka kampuni zinazokatwa kodi, kutojilinganisha na kampuni zingine. Wabunge wahusika Alishangaa wabunge wanaolalamikia ulipaji Sh 1,000 za simu,kwa maelezo kwamba kodi hiyo haikupendekezwa na Serikali,bali Bunge kupitia Kamati ya Bunge lilitaka wananchi wakatwe Sh 1,450.

Baada ya mapendekezo, Mgimwa alisema Serikali ilifanya uchambuzi na kuamua kupunguza hadi Sh 1,000. Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, jana alisema msimamo wa Serikali ndio wake pia.

Kauli ya Mgimwa inajibu malalamiko ya baadhi ya kampuni,wabunge na vyama vya siasa, kwamba ongezeko hilo linaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.

Hivi karibuni kampuni za simu na Mbunge wa Ubungo,John Mnyika (Chadema), walilalamikia kodi hiyo kwamba inaongeza gharama za maisha kwa wananchi.

Mbali na Mnyika,hata CCM kupitia taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ilitaka kodi hiyo iondolewe na Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato.

Pia Chama cha Watoa Huduma za Mitandao ya Intaneti Tanzania (TISPA), walilalamikia sheria mpya ya kodi na ushuru wa bidhaa katika intaneti,kwamba itachangia ongezeko la gharama za huduma ya intaneti kwa watumiaji wa kawaida.

Source: Habari Leo
 
Final withholding tax maana yake nini? yaani kampuni lilipe kodi na mtumiaji alipe kodi?
 
Big up, msimamo ni kitu muhimu sana katika serikali yoyote ile duniani. Habari ya kuwasikiliza wanasiasa ni kupoteza muda wa kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Big up, msimamo ni kitu muhimu sana katika serikali yoyote ile duniani. Habari ya kuwasikiliza wanasiasa ni kupoteza muda wa kuwaletea wananchi maendeleo.


Hatuwezi kuwa wajinga na wanyonge kias cha kuweza kuliruhusu hili...
Kama mnabisha wewe na mafisadi wenzako subirini mtaona mwisho wake,tumeshachoka na kwa hili litakuwa kama sehemu ya kuanzia.,serikali ya kipumbavu kabisa hii...
 
Hatukatai kulipa kodi tatizo hakuna outcome nzuri, isitoshe kuna sehemu nyingi tu za kukusanya kodi serikali imezifumbia macho wangeni wanapewa misamaha..serikali ianze huko kabla ya kuja kwa wananchi
 
Ana haki kujiropokea atakavyo maana yeye ametengewa bajeti ya mawasiliano hivyo haitamdhuru!
 
Natamani kula ban ila mods nikitupia neno nakuta vidoti why? Haya bwana cha maana hana mgimwa mjinga
 
Nafikiri lile wazo la kuzima simu wananchi wote linatakiwa lifanyiwe kazi vizuri......hii serikali imekuwa na njaa kiasi imeamua kutafuna watoto wake.
 
Muziki sio lazima uzimwe ndo mchezaji achukie,hata kila mpiga ala akipiga atakavyo hapo ndo mwisho wa dansi..

Endeleeni kupiga tena kwa sauti ya juu..wachezaji pia tuna maamuzi na kumbi zipo nyingi pia.,tutaenda ukumbi unaopiga muziki tunaouhitaji
 
Hii haikubaliki. Kuna maeneo mengi ya vyanzo vya kodi lakini inaonekana wanaangalia vyanzo rahisi kwa sababu wanajua ni lazima watu watatumia simu. Isitoshe kampuni zinalipa kodi sasa ni kwa nini tena watumiaji wa huduma wanadaiwa.Bei ya operator tayari imejumuisha extra costs?? Ni sawa na muuzaji na msafirishaji wa mkaa analipa kodi na tena mwananchi anayenunua anadaiwa extra kodi?????

Au Muagizaji wa spea anadaiwa kodi na anapofikisha dukani anapanga bei itakayojumuisha additional tax. Sasa mnunuaji wa spea in addition hawezi tena kudaiwa kodi - Please think of other source of tax.
 
Hapa hakuna fedha ya maendeleo inayokusanywa fedha hizi ni maandalizi ya CCM kwa ajili ya uchaguzi 2015 na ndo maana wanalazimisha.
 
Hatuwezi kuwa wajinga na wanyonge kias cha kuweza kuliruhusu hili...
Kama mnabisha wewe na mafisadi wenzako subirini mtaona mwisho wake,tumeshachoka na kwa hili litakuwa kama sehemu ya kuanzia.,serikali ya kipumbavu kabisa hii...

Mkuu ulisema piga ua gesi haitoki Mtwara naona mabomba yameshafika huko jana
 
Mkuu ulisema piga ua gesi haitoki Mtwara naona mabomba yameshafika huko jana


So what?imeshatoka??
Na issue sio tuh kusema gesi haitoki bila ya reason,hoja ni kwamba haitoki hadi serikali ieleze umma wa watanzania uhalisia wa mikataba,manufaa kwa wananchi kwa ujumla wa taifa zima,hasa kwa kuanzia na huku ilipogundulika rasilimali hii na serikali kueleza short tem & long term plans and benefits za uwekezaji katika rasilimali hii kwa taifa,
Watu wa Mtwara si wapumbavu kwamba washikilie kitu bila kuwa na hoja,we unadhani sisi tunajihesabu kuwa tumefeli??
Si wanallinda na JWTZ hapa.,why walinde?why waingie gharama kama hizi?
Si,wameunda kamati ya bunge ije kuzungumza na wadau ili taifa lijue uhalisia,nani kapoteza?besides kama ikiwa na ishu ya ufisadi wa CCM katika hili watakaoloose si wana mtwara pekee,litakaoloose ni taifa zima,sisi tulikuwa na bado tupo kulipigania taifa letu dhidi ya walafi na wahujumu uchumi wa taifa hili...
 
Big up, msimamo ni kitu muhimu sana katika serikali yoyote ile duniani. Habari ya kuwasikiliza wanasiasa ni kupoteza muda wa kuwaletea wananchi maendeleo.

Namna hii ndio bado mnalalamika kuwa mnapoteza umaarufu kwa wananchi wenu kisha mnawatafuta CDM kama mchawi wenu!!
 
Tuko radhi hata wananchi wale nyasi ila ndege ya mkulu wa kaya inunuliwe... mimi kwa mtizamo wangu ninahisi "kuna mpunga unatafutwa kwajili ya kambi fulani kipindi fulani kwa tukio fulani " xaxa njia rahisi ya kupata chao bila jasho ni kupitia hili tozo la kadi za simu kwani kwa mwezi mmoja wanauhakika wa kukusanya zaidi ya 2 billions Kkwa kima cha chini sasa sipati picha kwa hii miezi zaidi ya 50 iliyobaki ili kufika kwenye tukio la kuupiga mpunga, sasa watakuwa na shiling ngapi kwapani mpaka "muda mwafaka wa lile tukio kuu " ukifika . wa TZ tuamke muda kulala kwani kushakucha mapeeema. Dalili za mvua ni ...
 
Back
Top Bottom