MGIMWA: Kodi ya simu kutobadilika

MGIMWA: Kodi ya simu kutobadilika

Nafikiri lile wazo la kuzima simu wananchi wote linatakiwa lifanyiwe kazi vizuri......hii serikali imekuwa na njaa kiasi imeamua kutafuna watoto wake.

Wanatafuta za mwaka 2015
 
Kumbukeni mgimwa ni waziri wa viti maalumu pamoja na muhongo,hawa hawana hofu na ulaji wao,kwa hali hii ccm inazikwa rasmi 2015.Hii inatia hasira na uchungu...hapa jamvini tunaogopa ban..otherwise cjui ningetumia lugha gani kuonesha hasira na uchungu nilionao.Mawaziri wao hawatozwi kodi wao na watoto wao.
 
Huyu mzee akili zake siyo nzuri nahisi kwahiyo yeye anaona fahari kupingana na mawazo ya wanaotengeneza fedha na ajira katika Nchi hii kwa manufaa ya Serikali yenyewe na Watanzania wote.Hili ndio tatizo la Serikali za Kikomunisti duniani kwote.Wakomunisti siku zote huamini Serikali ndio suluhisho la kitu,Wanapenda kuwapangia watu namna ya kuishi,namna ya kufikiri kwa ujumla Wakomunisti wanapenda kumiliki maisha ya watu.Sekta binafsi ambayo ndio injini ya Uchumi,Ajira na maendeleo ya sayansi na kiteknolojia haina uhuru wala haithaminiwi na serikali ya kikomunisti.Kitendo cha Serikali ya CCM ya kuitoishirikisha Sekta binafsi katika maamuzi yake ya kisera kwa mfano kuviburuza Vituo vya Television kuingia katika Digital Technology bila ya kusikiliza maoni yao na hiki kitendo cha Serikali kupuuza wito wa Makampuni ya Simu juu ya hii Kodi mpya inaonyesha dalili zote za Serikali kufuata itikadi za kikomunisti.Sifa kubwa ya Serikali ya Kikomunisti ni kukosa ubunifu katika kukuza fursa za shughuli za Kiuchumi
 
Hivi jaman kwa nini tusiwaige Waarabu? Manake mm nahisi hawa ccm wametuchosha. Tumedharaulika sana!! Nmekasirika sana.
 
Hapa hakuna fedha ya maendeleo inayokusanywa fedha hizi ni maandalizi ya CCM kwa ajili ya uchaguzi 2015 na ndo maana wanalazimisha.


Umenikumbusha wimbo wa Masanja wa TOT, Mchimba kaburi aingia mwenyewe. Uamuzi huu wa ccm ni kitanzi chao wenyewe. Nape alishituka lakini nadhani waziri haja fore see impact yake kwenye siasa. Waziri kashindwa kutambua kuwa policy za uchumi zina muingiliano mkubwa na siasa za nchi. Atakuja shuhudia matokeo yake!
 
“Wananchi wenyewe wanalalamikia ukosefu wa huduma na baada ya Serikali kupitia na kufanyia kazi changamoto hizo, imeridhia kodi hizo… wanakuja watu wanalalamika,“ alisema.

Source: Habari Leo

Bogus Kabisa..., huyu jamaa anataka kuleta siasa na ku-insult intelligence ya watu..

Of course wananchi tunataka maendeleo ila kwanini hizo kodi zisitoke kwenye madini yetu au categories ambazo hazimbani mlaji direct ?, hivi hajui kwamba watu kwa sasa simu ndio ofisi zao na zinawafanya wapate mkate wa kila siku..., sasa na wakishindwa hata kutumia hizo simu wakale wapi.. ?, Ajira hakuna na wanaojitahidi kujipatia ajira wanabanwa huyu jamaa bure kabisa, na hao / hio kamati walioleta hio suggestion ndio wapo out of touch
 
Yaani kodi wanazotukata kila kukicha hazitoshi kutoa hizo huduma tunazozidai mpaka waanzishe kodi nyingine? Kama ni kodi zilizopo kutokukidhi kwa nini wasipendekeze kuongeza viwango vya hizo kodi badala ya kuanzisha kodi nyingine> Na hiyo kodi ya line za simu, mwananchi anatozwa kwa sababu gani? Kwla nini wasitoze makampuni ya simu?
 
Sawa mstari umechorwa...

Tanzania haihitaji nguvu kubwa kama za Arab Spring .................. CCM wanatusaidia kujitoa wao wenyewe madarakani kwa speed nzuri tu!! Issue hii inawaaffect karibu wapiga kura wote nchini!! Kwa hiyo ujumbe umefikishwa kisawasawa ...... Mgimwa anadai ni wazo la Chenge ..............Asante zangu kwa waheshimiwa Mgimwa na Chenge!!
 
Umenikumbusha wimbo wa Masanja wa TOT, Mchimba kaburi aingia mwenyewe. Uamuzi huu wa ccm ni kitanzi chao wenyewe. Nape alishituka lakini nadhani waziri haja fore see impact yake kwenye siasa. Waziri kashindwa kutambua kuwa policy za uchumi zina muingiliano mkubwa na siasa za nchi. Atakuja shuhudia matokeo yake!

Nchi hii mapumbavu bado mengi mno, angalia uchaguzi wa Arusha, CCM bado inapata kura zaidi ya 1000! Ilitakiwa wapate zisizo zidi 5, yaani za viongozi wa CCM ambao wanasomesha watoto wao nje ya nchi! Utakuta lilala-hoi linaipigia kura CCM halafu lina lalamikia kodi za laini ya simu!!!!!
 
mgimwa hana tofauti na dikteta kama saddam au hitler, anachoamua yeye kiwe ndo hichohicho kiwe, hajui mdororo wa kipato cha wanajamii kilivyo. hawa mawaziri wa viti maalum na wengineo dizaini ya kina muhongo hawatakiwi dunia hii...
 
Back
Top Bottom