Mgeni siku ya kwanza - kula na kubakisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeni siku ya kwanza - kula na kubakisha?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 26, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Kwa mbwembwe nimeingia, salamu nawatakia
  Za watoto nawaitikia, wakubwa naamkia,
  Swali nawaulizia, natumai mtajibia,
  Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

  Mgeni akikujia, kutoka maili mamia,
  Hata jirani na njia, hodi akakupigia,
  Nawe ukamlakia, huku ukimkumbatia,
  Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

  Ndipo ukamwandikia, chakula cha kunukia,
  Kumbe njaa kazuia, chakula kakipania,
  Akala akigunia, utamu ukimwingia
  Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

  Mwisho alipofikia, sahani akaachia,
  Chakula kikabakia, ni wali na mboga pia,
  Ndipo ukaulizia, 'vipi hujafurahia'
  Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

  Mgeni kakuambia, siku ya kwanza nabakishia,
  Ya pili ikiingia, ntakula utakimbia,
  Ndipo swali kuingia, ni mila ya kuachilia,
  Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia!

  Tamati nimefikia, na miye nawakimbia,
  Ugeni umenijia, chakula naandalia,
  Kesho nitawaambia, kama alibakishia,
  Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia!

  Na. M. M.Mwanakiiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ngoja kwanza nijaribu kumjibu Mzee Mwanakijiji...

  Kila mgeni akila, lazima kubakishia
  Ikiwa kamalizia, Aaonekana kapupia
  Shangazi yangu Aisha, somoni alinambia:
  Bila kula mara mia, Usile ukamalizia

  Ugenini waingia, kwa njaa waumia
  Mwiko na safuria kulamba watamania
  Mwanangu wewe tulia, jaribu kuvumilia
  Bila kula mara mia, Usile ukamalizia

  Kuna wanawake pia wanashindwa kuangalia
  Mlo wa kumalizia na ule wa kubakishia
  Kwa mlo wa kukaribia, wanasafisha sinia
  Bila kula mara mia, Usile ukamalizia

  Ila hili lakumalizia, au tena kubakishia
  Manyingi hutegemea umri pia jinsia
  Kijana akimalizia anaonekana Kadhamiria
  Kijana akibakishia, huonekana hana afia

  Wengi wao hutumia sifa hiyokama Njia,
  ya kutafuta pa kufikia, au hata kuhamia
  wenyeji hufurahia vijana wakimalizia
  Kijana akibakishia, huonekana hana afia
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  ajilie awezavyo, bila umiza mwenyeji.
  Asifanye atakavyo, bora aanzie maji
  yatatuliza alavyo, huku akisoma mji
  mgeni siku ya kwanza, ajilie kwa akili
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha story ya my late bro!
  Aliksribishwa lunch, na mdada alikuwa anamfukuzia (lsevya Tbr); kaenda na mshkaji wake. My bro was starving n the food was mmwah! Kwa wanaowajua wadada wa kinyamwezi wa enzi zile (sio kina sisi) watakuwa wanaelewa nikisema the food was mmwah!

  So, mdada wa watu (sijui ndio mila) akawaacha wale; yeye kaenda uani kuendelea na shughuli zake. My bro kafukumia lile punga na kuku wa kienyeji, akafuta. His buddy, hakuwa mlaji sana, alibakisha chakula. So my brother baada ya kusikia movement sign ya mshori kuja; akanadilisha plate. Yake iliyo clean kaisogeza kwa mshikaji na ya mshikaji yenye mabaki akaiweka kwake!

  Mdada alivyoanza kutoa vyombo; akamuuliza buddy wa bro "shemeji nikuongeze chakula?".
  You can imagine nini kilichotokea baada ya my bro na buddy wake kurudi ufisini!
   
 5. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  mh! Dada Ngorongoro a
  ni wapi hiyo?
   
 6. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mbona umestuka kaka? au ndio wewe, wavamia ugenini? lol
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  sidhani chakula kiongelewacho ni cha kwenye masinia, someni kati kati, chini na juu ya mistari.
   
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Sijaiuelewa; Ngorongoro? Mimi nimema Tabora!
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Kongosho nishaelewa siku nyingi! Lkn nimeikumbuka tu hiyo story!

  Na kwangu mimi, mgeni akimaliza chakula Siku ya kwanza nafurahi; kwani inaonesha kafurahia! Na ni kwa maana zote!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Kumbe ama kuna wapishi wazuri humu au wapo walaji wazuri....
   
 11. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mawazo yangu yote ni kwenye Pilau Kuku, kumbe kuna chakula ingine inayozungumziwa...
   
 12. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Siku ya kwanza ina everlasting impression!
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Pilau ziko za aina nyingi. Kuna pilau maua, pilau maharagwe, pilau samaki, pilau ng'ombe, pilau bata, pilau soseji,pilau mbuzi, na hiyo pilau kuku.
   
 14. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kula ni kula jamani,mbaya kukomba mboga utaonekana hujatulia,mlafi nk. Ni vizuri siku ya kwanza ukala chakula chote na mchuzi ukanywa wote ili mwenyeji apange bajeti nzuri siku nyingine!
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,394
  Trophy Points: 280
  Mgeni kafakamia, aibu kajipatia,
  Tonge lamkwamia, kooni kujipitia,
  Style hakuitumia, kuanza maji pitia,
  Sasa anaumia, pia anajutia
   
 16. B

  Bagram Army Member

  #16
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba mwenye mji vipi mbona huna kauli?
  Kula ale mgeni akila mwenyeji mwasema kafakamia.
   
 17. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  You guys are the best mmenifanya nifurahi asubuhi na mapema kwa ushairi..dah!
   
 18. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  King'asti, pia kuna pilaw za vegetarians
  Pilau njegere, pilau maharage, pilau soja nk
  Kuna pilau for all tastes, hata pilau kavu ipo.
   
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mgeni siku ya kwanza???????????usijifanye mjuaji......
  Pembeni kuangalia, kila dakika macho chini.....
  Tabasamu tupilia.lakini liwe la mbali.....
  Mgeni siku ya kwanza...usijifanye mjuaji.....
  Nina ugeni mahali leo
  thax kwa tips..........
   
 20. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mwali naona upo bussy na ugeni
   
Loading...