Ondoeni Chama Cha Mafisadi madarakani ndipo mtakapo kipatia CHADEMA na DK Slaa uongozi wa nchi mtaweza kutatuliwa tatizo lenu, ila kwa sasa vumilia maana mliyataka wenyewe mlipomchagua huyu muanguka majukwaani kuongoza nchi. Nyerere si aliwaonya kuwa kama mnamtaka mkanywe naye chai ninyi mkapitiliza mkampatia uongozi wa nchi?Wakuu, Tanzania ni nchi nzuri na watu wake wana heshima ya ajabu... inasikitisha sana kuona mgeni anakuja, anatukana watoa huduma wetu na mengine mengi, lakini mara nyingi sisi kama watanzania hukaa kimya na kufunika kombe
nimesoma habari moja ya Mpakistani kuchana noti ya Tanzania nikasikitika sana na cha kwanza nilipata hisia kwamba huyu mtu ni sawa na aliyechana bendera au hata mwenye dharau ya kupindukia... hakufanya hivyo akiwa amelewa wala amekuwa provoked
Nakumbuka miezi kadhaa iliyopita raia mmoja wa kigeni alimtemea mate polisi wwetu na hatukukaa kimya, rai yangu ni kwamba tulaani kitendo hiki lakini tusiishie hapo
Kiburi hiki kinaletwa na watu wetu wa idara ya uhamiaji kutoa hivi vibali kwa njia mbadala hivyo kujishusha na kushusha hadhi ya nchi, wageni wanaona sisi sasa ni wa kununuliwa kwa dola chache hivyo sawa tu hata kutudhalilisha
Mgeni huyu ni wa NGO ya kimarekani, si ajabu dharau hizi zinatokana na mitazamo au hata mazoea ya wageni hawa nchini (dharau)... shirika lililomwajiri tayari lina wageni wengine, na inawezekana kabisa dharau hizi zimo ndani ya shirika na hasa kwa wageni waliobaki
tulaani kitendo hiki
tumulike haya na-NGO
Somo la uraia lifundishwa kwa wageni ili waelewe watanzania tuna culture yetu
source Habari leoHabari za Kitaifa
Mgeni aliyechana noti adakwa
Imeandikwa na Nashon Kennedy, Mwanza; Tarehe: 7th September 2010 @ 22:25 Imesomwa na watu: 204; Jumla ya maoni: 2
POLISI mkoani Mwanza imemkamata Attique Ahmad Swatt (35) ambaye ni raia wa Pakistan kwa kosa la kuchana hadharani noti ya Sh 5,000 mali halali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Nonosius Komba aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa Swatt alichana noti hiyo jana saa 6.30 mchana, wakati alipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza akiwa safarini kwenda Dar es Salaam.
" Wakati akiwa ‘board room' pale uwanja wa ndege, wananchi walimuona akiitoa noti hiyo ya Sh 5,000 na kuichana, walichukizwa na kitendo hicho na walipotoa taarifa kwenye kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege alikamatwa," alisema Komba.
Alifafanua kwamba kitendo hicho ni kudharau mali halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Komba alisema vielelezo vikiwemo vipande vya noti hiyo viko Polisi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kesho mara baada ya utaratibu mwingine wa uchunguzi kukamilika
kwakweli itakua aibu kama huyu jamaa ataachiwa aendelee kuishi nchini
kwakweli itakua aibu kama huyu jamaa ataachiwa aendelee kuishi nchini
Hii ni dharau kubwa na kosa la jinai kwa nchi. Baadhi ya national symbols kwa nchi yeyoet ni pamoja na
;
1. National Currency
2. National Flag
3. National Anthem
4.etc, etc
Sasa basi kama ilithibitiska hivyo, mhusika alitakiwa akamatwe mara moja na kufikishwa vyomo vya dola na hatimaye kufunguliwa mashtaka. Tatizo tanzania civic education haipo na mambo yanayofundishwa hata kwa wale wachache hayatilii msimamo na mkazo kwa baadhi ya mambo. Nchi hii bwana, nachoka kabisa.
4. kadhalilisha inchi
mhusika kakamatwa, lakini nahofia asije akawa kama akina chenge tu, maana tanzania ni zaidi ya uijuavyo
naskia amelipishwa faini ya shilingi elfu tano tu:mad2:,,,, kuna wakubwa wametetea hapoTunahitaji kuona mtu anafungwa hapa hapa hakuna kumrudisha NYUMBANI. Anyee debe kwanza hata mwaka mmoja, na viboko kumi nambili. Siku hizi watu wanachezea sana taifa letu, hata Watanzania hatujali kabisa tena viongozi ni jina tu, "Viongozi".
Ukienda nchi zingine, cha kwanza ni DO's and DON"Ts pamoja na culture kama namna ya kusalimiana na wenyeji. hiyo inahitajika pia kwetu, kama mtu amekuja kwetu lazima afuate sheria zetu huo ujinga uishie kwenye ndege. So sad to see someone from another country do something like that.
AFUNGWE, Wala hakuna kesi hapo. :A S-coffee:.
............hii sasa dharau faini ya elfu tano!!!naskia amelipishwa faini ya shilingi elfu tano tu:mad2:,,,, kuna wakubwa wametetea hapo