Mgawanyo wa majukumu katika utendaji wa Wizara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
MGAWANYO WA MAJUKUMU KATIKA UTENDAJI WA WIZARA

Watanzania kwa Muda mrefu tulikuwa na hamu kubwa ya kuona Mgawanyo wa madaraka na Majukumu katika utendaji Kazi katika Serikali. Kuna Jambo kubwa sana la kujifunza na kujivunia kwa Rais wetu Mpendwa @SuluhuSamia jinsi anavyoongoza na alivyowapa majukumu Mawaziri wake katika kutimiza majukumu yao pasipo kuwaingilia.

Mfano mdogo juzi tumeshuhudia Rais wetu akimtengua mwenyekiti wa Bodi ya TPA lakini pasipo kumuingilia majukumu Waziri wake akamuomba Waziri akatimize majukumu yake kwa wajumbe wa Bodi hizo maana ni majukumu yake kama Waziri.

Nani asiyejua kuwa Mamlaka ya Rais ndio ya Mwisho. Lakini kwa kuheshimu SHERIA,Kanuni na Miongozo Rais @SuluhuSamia kwa nyakati tofauti ameacha Mawaziri wake watimize majukumu yao pasipo kuwa ingilia. Hakika Tanzania tunahaja ya kumpongeza na kumshukuru Rais wetu kwa utendaji Kazi wake.

#MgawanyoWaMadarakaChachuYaKulindaDemokrasia

#MamaYukoKazini
#KaziIendelee

Screenshot_20211206-093741.jpg
 
Back
Top Bottom