Acha chuki wewe, Kagasheki na Catherine Magige wao walikuwa wanafanya nini?
Baadhi ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.
Akichangia muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011, Assumpter Mshama (Nkenge ? CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA, ?Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi,? alihoji.
Aliongeza: ?Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo. ?CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni Kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje.?
Kwa upande wake, Livingstone Lusinde (Mtera - CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.
Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku, ?Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme,? alisema. Ingawa Lusinde hakuwataka kwa majina ndugu hao wa viongozi wa juu wa CHADEMA, lakini inafahamika kwamba, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, mtoto wake ni Lucy Owenya na mkwewe ni Grace Kiwelu ambao ni wabunge wa viti maalumu.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa mkewe Rose Kamili naye ni mbunge wa viti maalumu, kama kwamba haitoshi Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu naye ana dada yake, Christina Mughwai ambaye ni mbunge wa viti maalumu.
Kigogo mwingine wa CHADEMA, ambaye ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar, naye ana mtoto wa dada yake bungeni kupitia nafasi hizo. Mjomba wake kigogo huyo ni Raya Ibrahim Khamis.
Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo, kwani wa kuzuia fujo wapo, ?Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu,? alisema.
Lusinde alihoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.
Soma zaidi:
"Ukoo wa CHADEMA Bungeni" Hizi ndizo siasa za Tanzania za kumwokoa raia karne ya 21 (pathetic) - wavuti.weebly.com