Mgawanyo viti maalum Bunge la 11

Mgawanyo viti maalum Bunge la 11

mchambuzixx

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
1,292
Reaction score
946
Mgawanyo viti maalumu kwa kila chama

CCM 62
CHADEMA 43
CUF 7
ACT 0
NCCR 0

Hii ni kwa mujibu wa NEC... Kila chama kimevuna mavuno yake...

Ubunge Viti Maalum kaa la moto

Rama-03Nov2015.png

Mkurugenzi wa Nec, Ramadhani Kailima
​

Viti Maalum vya ubunge vimekuwa kaa la moto kwa vyama vya siasa nchini, kutokana na kusubiri kwa hamu uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuhusu idadi ya wabunge hao, idadi ya kura za wabunge na sifa za kupata viti hivyo.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Nec, ilitenga viti 102 kwa ajili ya Wabunge Wanawake, ikiwa ni sawa na asilimia 40 ya Wabunge 256 waliokuwapo (majimbo 239 na 17 wengineo).

Katika uchaguzi huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipata wabunge 69 na vyama vingine CUF na Chadema viti 33.

Katika mchakato huo, idadi ya Viti Maalum kwa CCM itapungua huku ya vyama vya upinzani ikizidi kuongezeka kutokana na uwapo wa wagombea wake kila jimbo.

Ili chama kipate viti maalum ndani ya Bunge la 11, ni lazima kiwe na asilimia tano ya kura za ubunge nchini nzima.

Kwa kutimiza sifa hiyo, ni dhahiri kuwa vyama vitakavyopata Viti Maalum ni CCM, Chadema na CUF kutokana na idadi ya kura za ubunge kwa kila jimbo.

Idadi ya Viti Maalum kwa CCM itapungua tofauti na vipindi vilivyopita kutokana na vyama vya upinzani kama Chadema, CUF na ACT kusimamisha wagombea katika majimbo yote nchini na hivyo kupunguza kura ambazo chama hicho tawala kingezipata katika majimbo.

Katika uchaguzi wa mwaka huu uliohusisha majimbo 258 kati ya 264, CCM imeshinda ubunge katika majimbo 182, ikifuatiwa na CUF iliyoshinda katika majimbo 39 na Chadema 35, huku vyama vya ACT-Wazalendo na NCCR- Mageuzi vikipata kiti kimoja kimoja.

Majimbo nane hayajafanya uchaguzi wa wabunge kutokana na sababu za vifo vya wagombea katika majimbo sita na kasoro mbalimbali katika majimbo mawili.

Majimbo ambayo wagombea walifariki dunia ni Ludewa, Lushoto, Ulanga Mashariki, Arusha Mjini, Handeni Mjini na Masasi. Majimbo yenye kasoro ni Lulindi na Kijitoupele.

Bunge la 10 kulikuwa na wabunge wa majimbo 254, kati yake CCM ilikuwa na viti 186, CUF 23 na Chadema 24, NCCR-Mageuzi vinne huku UDP kiti kimoja na TLP kimoja. Wa kuteuliwa na rais kumi, Baraza la Wawakilishi watano.

Licha ya Chadema kuwa na wabunge wachache wa majimbo ikilinganishwa na CUF, lakini itakuwa na wabunge wengi wa Viti Maalum kutokana na wingi wa wapiga kura wa majimbo ya bara ambayo Chadema imeshinda katika nafasi hiyo.

HESABU ZINAVYOPIGWA
Ili kupata viti maalum kwa kila chama ni lazima ijulikane idadi ya viti hivyo kwa kipindi hiki ambacho ni sawa na asilimia 30 ya wabunge 281 ambayo ndiyo wabunge wa Bunge lijalo.

Kwa hesabu hizo, viti vya Wabunge Maalum vitakuwa kati ya 84 au 85 ikilinganishwa na vya Bunge lililopita ambalo vilikuwa 102.

Chanzo kimoja kimeieleza Nipashe kuwa kwa hesabu hizo, CCM itapata viti 46. Bunge lililopita chama hicho kilikuwa na Viti Maalum 69.

Kwa mujibu wa Katiba idadi ya wabunge wanawake (Viti Maalum) isipungue asilimia 30 ya wabunge wote waliotajwa katika Katiba.

Kwa mujibu wa kilichoandikwa katika ukurasa wa ‘Facebook' wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu, wabunge wanaohesabiwa ni wa majimbo 264, Baraza la Wawakilishi watano, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mmoja, uteuzi wa Rais 10 na Spika kama sio mbunge mmoja na kufanya jumla ya 281.

"Hivyo katika Bunge hili, Wabunge V/Maalum wanatakiwa wasipungue asilimia 30 ya Wabunge 281," alieleza.

Mwalimu alifafanua kuwa upatikanaji wake wanachaguliwa na vyama vya siasa kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa Wabunge na siyo idadi ya wabunge. "Kila kura moja inachangia kupatikana kwa wabunge Viti Maalum. Wataalamu wa mifumo ya uchaguzi wanautambua mfumo huu kama ‘proportional representation'. Tofauti na mfumo wa uchaguzi wa wabunge wa majimbo ambao ni ‘Aliyepata kapata na aliyekosa kakosa," alifafanua katika ukurasa huo.

Mwalimu ambaye ni mshindi wa Viti Maalum mkoani Tanga, amefafanua kuwa kama chama kimepata kura halali za Wabunge asilimia 60 basi kitapata asilimia 60 ya viti vilivyotengwa.

Akizungumza na Nipashe, Mkurugenzi wa Nec, Ramadhani Kailima, alisema mwishoni mwa wiki hii kazi ya kutambua Viti Maalum itakuwa imekamilika na vitatangazwa baada ya kukamilisha hesabu.

CHANZO: NIPASHE(03/11/2015)
 
so far I reserve my comment until some times
 
Mama regina lowassa ndani. Wakati huohuo lowassa speaker wa bunge.
 
Mgawanyo viti maalumu kwa kila chama

CCM 63
CHADEMA 43
CUF 7
ACT 0
NCCR 0

Hii ni kwa mujibu wa NEC... Kila chama kimevuna mavuno yake...heko lowasa kura za urais zimetuongezea viti wapinzani

Viti maalum hutokana na kura za wabunge na siyo kura za urais. Kama ingekuwa kura za urais CUF wasingepata viti vyovyote kwani hawakuweka mgombea. Kura za urais hutumiwa kwenye mahesabu ya ruzuku.
 
Mama regina lowassa ndani. Wakati huohuo lowassa speaker wa bunge.

Mlianza Kumtabiria Atapita Kuwa Mgombea Urais Ndani Ya CCM Akakosa, Mkamtia Ndimu Baba Wa Watu Ahamie CHADEMA Kwa Kumpa Matumaini Kuwa Anakubalika Na " Wapumbavu Na Malofa " Wengi Akakubali Na Kuingia Kichwa Kichwa Ameukosa Urais Sasa Tena Bila Hata Haya au Aibu Mnataka Mumtie Tena AIBU Ya Kufungia Mwaka Agombee Uspika Ambapo Hata Huko Napenyewe Atakosa. Hivi Lowassa Huwa Hana WASHAURI WANAOJITAMBUA? Kama Kawaida Yangu Nimekuwa Nikisema Mambo Na Yanatimia. Nilianza Na Kusema Dr. Magufuli Atapita CCM Na Nikasema Tena Atakuwa Rais Na Juzi Nikasema Waziri Mkuu Atakuwa Kati Ya Dr. Mwakyembe au Prof. Muhongo Na Sasa Nasema Kuwa Piga UA Spika Wa Bunge La JMT Ni Kati Ya Mussa Zungu au Job Ndugai au Samwel Sitta Na kupitia Wewe POPOMA Wa UKAWA Mwambie Kabisa Lowassa Kuwa ASIJISUMBUE Na Aende Sasa AKACHUNGE Ng'ombe Zake Kule MONDULI Huku Akilea Tu Wajukuu Zake Na Atuache Sasa CCM Na Serikali Yetu Ijayo Tufanye Kazi Ya Kuwaletea MAENDELEO Ya HAPA KAZI TU Watanzania.
 
Duh! siku Mh. Lowassa anakaribishwa Rasmi na kukabidhiwa Kadi ya Chadema Mh. Mbowe aliuhakikishia Umma wa Wa tanzania kuwa Bunge la 11 hakutakuwa na Chama kitakacho hodhi Bunge Binafsi niliamini hilo na nikajiaminisha kuwa Lowassa hawezi kushinda ila Amsha amsha zake zitatuwezesha kuwa na Bunge litakalokuwa walau na theluthi moja ya wabunge kutoka kambi ya Upinzani, Ukawa msikate Tamaa kawia Ufike ila pia Mzingatie ule Uamuzi wa Mbowe alioutangaza 2014 kuwa Hawatochukua tena MAKAPI toka CCM na akisahau msikhofu kumkumbusha.
 
Viti maalum hutokana na kura za wabunge na siyo kura za urais. Kama ingekuwa kura za urais CUF wasingepata viti vyovyote kwani hawakuweka mgombea. Kura za urais hutumiwa kwenye mahesabu ya ruzuku.

Hebu dadavua kidogooo
 
Viti maalum hutokana na kura za wabunge na siyo kura za urais. Kama ingekuwa kura za urais CUF wasingepata viti vyovyote kwani hawakuweka mgombea. Kura za urais hutumiwa kwenye mahesabu ya ruzuku.


Kitufe cha like sijui kwanini wamekiondoa, hili ni jibu murua, kuna watu hutiririka bila kujua wanadanganya.
 
Back
Top Bottom