Nina wasiwasi na umri wako au huenda labda hauna familia, lakini kama ungekuwa na familia inayokutegemea sidhani kama ungekuwa na muda wa kufanya hayo unayoyafanya. Watu sasa hivi kila sehemu wanalia na mgawo wa umeme kiasi kwamba shughuli zao zote zimesimama watoto wao wameshindwa hata kurudi shuleni kwa kukosa ada hapo unafikiri huo muda wa kwenda kukesha bar atautoa wapi? Sasa hivi unaambiwa huo mgawo wa umeme utachukua zaidi ya miezi 6, ina mana hiyo miezi yote utaisubiria ukiwa huko bar? Siku hizi Wastani wa bia 1 inauzwa Tsh 1,500 huo muda unaosubiria umeme ukiwa huko bar lazima utatumia bia 4 je kwa muda wa hiyo miezi 6 utakuwa umetumia sh ngapi? Kama shida yako ni umeme hiyo hela kwanini usiende kununua Genereta? NDIO MANA KILA SIKU WA TZ WANIZIDI KUWA MASIKINI. Rafiki yangu kifupi tu ni kwamba huo uamuzi uliouchukua hauwezi kutatua hilo tatizo la umeme matokeo yake ndo unazidi kujimaliza kabisaaaaaaa!! TAFAKARI KISHA CHUKUA HATUA.