Mgao mkali wa umeme Morogoro mjini

XI JIN PING II

Senior Member
Mar 8, 2017
125
110
TANESCO kama kuna mgao wa umeme hapa Mkoani Morogoro basi tutangazoeni tujue ili tukanunue magenereta tu. Kwa muda wa week kadhaa sasa tanesco mmekuwa mkikata umeme karibu mitaa yote kata ya kihonda.

Mathalani kuanzia siku ya ijumaa ya tarehe 18.Dec.2020 kata nzima ya Kihonda haikuwa na umeme.

Leo tarehe 21.Dec.2020, Mazimbu yote na mjini haikuwa na umeme. Leo jioni kuanzia saa 12 kata yote ya kihonda hakuna umeme tatizo ni nini?

Tuambieni tu kama tumerudi kwenye mgao wa umeme ili tujipange kivingine na huu uchumi wa kati.
 
TANESCO kama kuna mgao wa umeme hapa Mkoani Morogoro basi tutangazoeni tujue ili tukanunue magenereta tu. Kwa muda wa week kadhaa sasa tanesco mmekua mkikata umeme karibu mitaa yote kata ya kihonda. Mathalani kuanzia siku ya ijumaa ya tarehe 18.Dec.2020 kata nzima ya Kihonda haikuwa na umeme. Leo tarehe 21.Dec.2020, Mazimbu yote na mjini haikuwa na umeme. Leo jioni kuanzia saa 12 kata yote ya kihonda hakuna umeme tatizo ni nini? Tuambieni tu kama tumerudi kwenye mgao wa umeme ili tujipange kivingine na huu uchumi wa kati.
Hili tatizo la kukatika katika umeme limerudi kmya kimya .Hata hapa Dar lipo tuu kwa baadhi ya meaneo Tabata na Gongo la mboto na Pugu
 
Nipo town huku umeme upo kama kawaida Mkuu huenda wana matengenezo line za kihonda
 
Jaribuni kuwaona tanesco kunaweza kuwa na shida sehemu..
Wewe unafikiri TANESCO hawajui?
Thubutu yake, mpaka mfagizi wa ofisi ya TANESCO kwa sasa anajua nini kinaendelea kuhusu umeme hapa Tanzania. Ni mgawo halisi kwa 100%.

Ni karibu nchi nzima kwa sasa hakuna umeme kwa mtindo wa vipande vipande.
Mvua zitakapoanza na kujaza mabwawa, hizi kelele za kukosa umeme zitapungua sana.
 
Tanesco mkoa wa Morogoro wanaboa sana.Sijui km kweli tutafika na falsafa ya Uchumi wa Kati wa Viwanda.
 
Ingekuwa vyema Tanesco wakatoa tamko rasmi..
Ukimya wa nini nyakati hizi umeme unakatika hovyo hovyo bila taarifa
 
Back
Top Bottom