Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kichangani Morogoro Apongezwa kwa ubunifu wake wa kuboresha Zahanati hiyo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, CDE Fikiri Juma, amempongeza Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kichangani kwa ubunifu wake wa kuboresha Zahanati hiyo.

Pongezi hizo amezitoa hivi karibuni Oktoba 2023 katika ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini ya kukagua miradi ya Maendeleo inayotekekezwa na Manispaa ya Morogoro.

Aidha, Fikiri pamoja na Kamati yake ya Siasa wamefurahishwa na ubunifu wa uboreshaji huduma na majengo Zahanati ya Kichangani na kumwagia sifa kedekede Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kichangani Dkt. Magdalena Kongera.

Fikiri, amesema sifa hizo ni kutokana na kufurahishwa na Mganga huyo kwa kushirikiana na timu yake kwa kuitumia vizuri makusanyo ya fedha kwa kusimamia uboreshaji wa Kituo hicho.

"Hapa Kichangani mmeupiga mwingi, wenzenu wanashindwa kufanya haya, wao kila kitu wanategemea Mapato ya Manispaa lakini kwa upande wenu mmeweza hongereni sana endeleeni na ubunifu wenu na kuendelea kuwahudumia Wananchi wetu ambao wanaimani kubwa na Serikali yao chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa akipeleka fedha nyingi kwenye miradi hususani katika huduma za Afya" Amesema Fikiri.

Kufuatia sifa alizomwagiwa na Mwenyekiti wa CCM, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, alimtaka Dr. huyo kwa kushirikiana na timu yake wachape kazi na kuendelea kuwa wabunifu katika uboreshaji wa Kituo na utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.

Akiwa Mganga Mfawidhi fawidhi kituo Cha Afya Kingolwira, Dkt. Kongera, alipelekea Kituo Cha Afya Kingolwira kuibuka kinara katika zoezi la kitaifa la Big Result Now Brn mwaka 2018 Mkoani Morogoro na kuleta ngao ya pongezi Manispaa ya Morogoro iliyotolewa na Waziri wa Afya.

WhatsApp Image 2023-10-18 at 15.57.49.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-18 at 15.57.50.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-18 at 15.57.53.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-18 at 15.57.54.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-18 at 15.57.54.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-18 at 15.57.55.jpeg
 
Back
Top Bottom