Mfumuko wa bei waongezeka kutokana na Bei ya Nyama, Gesi, Ngano na Maziwa ya unga

Kusema it will never happen hapo ndio ujinga wako ulipojidhihirisha bila kificho.

Kwenye uchumi anything can happen. Kusema it will never happen inaonyesha kabisa jinsi ulivyo mweupe kichwani.
Uchumi wa nchi kama hii ndio jamaa anasema it will never happen. Marekani ilitokea GED miaka ya 1920s na mdororo wa uchumi mwaka 2008 wakati inaongoza uchumi wa dunia. Ujerumani iliwahi fikia inflation ya 29,500% (sijakosea kuandika) yani walikuwa wanakaa siku tatu na masaa kadhaa bei zinakuwa twice. Jumatatu saa 1 ukinunua kilo kwa 200, Alhamisi jioni hiyo kilo inauzwa 400. Kwa siku walikuwa na inflation ya over 20%

Nchi yenyewe ina uchumi wa hotuba na matamko. Uchumi wa kisiasa
 
Ameadjust lini tupe walaka wa EWURA aseee???
Nilichosikia wanakwenda kurekebisha sheria ya kupunguza tozo. Yaan baada ya mvua ya tozo kuwa nzito tena ya mawe na upepo walau watatupa mwamvuli kupunguza makali lakini kuloana kupo pale pale.
 
Kawaida tu ipande ishuke tutaishi

Kuna watu wananunua nyama kg 1 ,zaidi ya hiyo

I pande ishukke ipande tutaishi

Ova
Na ndio maisha siku zote,Mfuko wa simenti ulikuwa 4500 2010 leo 20,000 ..

Nchi iko Uchumi wa Kati gharama za maisha kupanda ni kawaida.
 
Ameadjust lini tupe walaka wa EWURA aseee???
Nilichosikia wanakwenda kurekebisha sheria ya kupunguza tozo. Yaan baada ya mvua ya tozo kuwa nzito tena ya mawe na upepo walau watatupa mwamvuli kupunguza makali lakini kuloana kupo pale pale.
Tozo zote ziliwekwa kwa sheria ya Bunge na Kati ya hizo ziko ambazo zinaweza kuwa adjustable lakini huwezi futa lazima zirudi Bungeni na zingine huwezi hata kuzibadilisha ndio maana Ili kuzifuta lazima warudishe mswaada wa sheria Bungeni.
 
Bidhaa za nyama, gesi ya kupikia, mkaa na viazi mviringo zimetajwa kuongeza mfumuko wa bei kutoka asilimia 3.8 Agosti hadi asilimia 4.0 kwa Septemba mwaka huu.

Taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Oktoba 8 jijini Dodoma, imetaja bidhaa nyingine zilizoongeza mfumuko wa bei ni ngano na maziwa ya unga.

Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja alisema sababu za kuongeza mfumuko ni kutokana na kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma.

Minja alisema mabadiliko hayo ni kwa mwaka ulioishia Septemba ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Agosti 2021.

Amesema badiliko hilo la asilimia 0.2 limechangiwa na kasi ya mabadiliko ya bidhaa za vyakula kama unga wa ngano kwa asilimia 6.8, nyama ya ng’ombe kwa asilimia 3.4, maziwa ya unga kwa asilimia 9.2, mayai kwa asilimia 5.0 na viazi mviringo kwa asilimia 4.7 na kufanya kuongezeka kwa asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.6 mwezi Agosti.

Amesema pia bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko ni gesi ya kupikia kwa asilimia 2.7, mkaa kwa asilimia 3.5, na huduma ya malazi katika nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7na kufanya bidhaa hizo kuongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.0 mwezi Agosti.

Mwananchi
Tutasikia mengi kwa hali tunayoenda nayo.
 
Hii inawahusu under 35 years umri wa kupigana , kilimo cha mahindi kimetupiga, tugeukie ufugaji wa ng'ombe , ikiandaliwa inatoa kitu inaitwa nyama, kilo ni kumi elfu ~mtaalam wa math adadavue hii ng'ombe inatoa kiasi gani cha faranga za tz
 
Back
Top Bottom