Mfumo "Wajumbe" ni Mbovu, CCM watakili na kuuacha

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
Wakuu heshima kwenu,

Huu mfumo wa wajumbe kwa maoni yangu nimeona unamatatizo mengi sana kuliko faida.

Ni mfumo ambao chama kitakuja kuutafakari kwa upya na kuutupilia kando.

Dhumuni la huu mfumo ilikuwa ati kupunguza rushwa lakini sivyo ilivyo,

Nina Hakika sana hakuna mwaka ambao fedha imenunua kura za watu Kama mwaka huu, Nadhani hata ripoti ya Takukuru ikitolewa itakuwa ushahidi mzuri na sababu kubwa Ni hii

Watia Nia hawakuruhusiwa kuendesha kampeni baada ya kuchukua fomu kueleza kusudio kwa wagombea, badala yake unapewa dakika mbili jukwaani kujieleza wewe Ni nani na utafanya nini.

Hii imewawia ugumu watu wenye nia ya dhati kupambanua kwa upeo namna ambavyo watawahudumia wajumbe, badala yake kumekuwa na kampeni za chini kwa chini, watia Nia wameendesha kampeni za chini kwa chini kwenye mito, miti na makaburi usiku wa manane kwa hofu ya Takukuru. Sambamba na Hilo kuwakutanisha wajumbe inahitaji mafungu, watu wametoa pesa na kupewa kwao kura kumepimwa kwa ukarimu wao.

Mfumo huu pia, unaweza kutoa kiongozi asiye chaguo la wengi, mfano panapotukia viongozi wawili wenye Nguvu sana basi kiongozi watatu anaweza kuibuka mbabe kwakuwa wale wawili watagawana kura na hii imetokea maeneo Mengi kiasi kwamba wale wajumbe wametoka ukumbini wakiwa hawaelewi walicho kifanya.

Mimi nilidhani, mfumo ule wa mwanzo uliwapa mzigo mkubwa wa kuhonga jamii nzima na hivyo wahongaji wengi walipata umaskini mkubwa, mfumo huu wasasa unawapa nafuu wahongaji.

Mimi nilidhani, mfumo ule wa zamani uliwapa nafasi wana CCM kujinadi mara mbili yaani kampeni za Chama na Zile za NEC, watanzania wakaelewa nini chama chao kina kusudia kuwafanyia, mfumo huu wa sasa unatoa dakika 2 za kuonesha sura yako!

Mimi nilidhani, mfumo wa mwanzo ulisababisha watu kuchagua kiongozi wao kwa sauti ya wengi "voix populii"
Mfumo wa sasa hauwapi wanachama uhuru wa kuchagua, badala yake kikundi Cha wajumbe wachache wanachagu, wakitumia matumbo yao kutoa kilio Cha wengi.

Nakipenda Chama Cha Mapinduzi lakini siupendi mfumo wa watu hawa
IMG-20200726-WA0058.jpg
 
Mkuu,

Huu mfumo ni mzuri sana endapo kura za maelekezo hazitakuwepo. Kura za maelekezo ndizo zinazofanya wajumbe tuwaone wabaya hapa.

Tatizo liko kwenye kata, endapo kama KATA kuna makundi basi tarajia haya na hata kama yasipokuwepo yatarajie pia.

Watia nia wengi wamedili na wajumbe ambao wako chini ya M/kiti wa tawi huska wakasahau kwamba M/kit wa kata pamoja na katibu wake wanacontroll haya matawi.

Viongozi wengi waliopitishwa na wajumbe ni wale ambao wako ndani ya chama kwa muda mrefu hivyo wanafahamiana na washakubaliana kwamba tunaenda na mtu gani.

Lakini pia mtia nia mwenye pesa akifanikiwa kuwanunua Kata basi kamaliza kila kitu kwa sababu wale wanakura zao zilizosimama.

Kuna diwani kapita kata fulani hapo mjini kwa dau la 80,000 kwa kila mjumbe. Sasa unajiuliza huyu mtu mshahara wake ni 350,000 na akiingia ofisini anakopeshwa 10mil. Hizi pesa zinarudi vp?!


Shukrani sana
 
Back
Top Bottom