Mkuu hakuna kitu cha bure hiyo huduma ya Beiduo lazima ilipiwe ili upate ile huduma standard.
Miaka ya nyuma kwenye navigation hali ikikuwa ngumu kwa kutumia nyota,jua,mwezi(Celestial Bodies). Baada ya GPS kuja watu walijua wamepata ahueni kubwa ilibidi walipie huduma.
Na baada ya tukio la ugaidi mwaka 2001 USA ilibidi aweke vizuizi kwenye matumizi ya GPS ambapo waliweka daraja la Military na Civilians use.Walifanya hivyo kujilinda na wabaya ambapo ukitumia civilian GPS kuna error kama mita kadhaa hivyo uwezi kupata target sahihi.
Hili utumie GPS halisi ambayo ni military purpose inakubidi ulipie huduma na hii waliuziwa nchi,makampuni na taasisi.
GPS ipo chini ya department of defense ya USA, jamaa walipoweka barrier hii ikawafanya jumuiya ya Ulaya na wao waanzishe Galileo, Urusi wakaja na Glonass, China wakaleta Beidou.
GPS mpaka kukava dunia nzima walitumia miaka mingi, mwanzo ilikuwa unapata GPS kwa maeneo ukiwa baharini.
Kwa sasa GPS na Glonass ndio zina cover worldwide.
Ngoja tuone Beidou kama itacover dunia nzima,ufanisi wake utakuwa vipi?