Yoyo Zhou
Member
- Jun 16, 2020
- 68
- 110
China Jumanne ilirusha satilaiti ya mwisho ya Mfumo wa kuongozea wa BeiDou(BDS), ambapo inaonesha kukamilika kwa uendelezaji wa mfumo huo nchini, miaka 26 baada ya ujenzi wa BeiDou-1 kuanza rasmi mwaka 1994, na kuwa mmoja kati ya mifumo minne ya mtandao wa uongozaji duniani, ikiwa sambamba na GPS wa Marekani, GLONASS wa Russia na Galileo wa Umoja wa Ualaya.
Hivi sasa duniani kuna nchi 130 ambazo kila siku idadi ya satilaiti za Beidou zinazozunguka katika anga zake za juu nikubwa zaidi kuliko GPS, na 100 kati ya hizo ni nchi za Asia na Afrika. Satilaiti nyingine zinamaanisha usahihi na utegemezi. Basi Beidou ina uhusiano gani na mwafrika wa kawaida, na ni jinsi gani itahudumia maisha yako katika pande mbalimbali?
Kila siku baada ya kuamka, tunakunywa chai. Beidou inatumiwa sana katika mfumo wa kilimo cha kisasa. Na inawezekana kuwa mikate unayokula inatengenezwa kwa ngano iliyovunwa na magari ya kuvunia yasiyo na dereva yakiongozwa na Beidou.
Baada ya kula chakula, unapanga kwenda kazini. Kabla ya kutoka nyumbani, unaangalia utabiri wa hali ya hewa kwenye simu, na BeiDou inaweza kukupatia huduma hiyo yenye usahihi mkubwa halafu utajua leo unalazimika kubeba mwavuli au la, na hata BeiDou inaweza kutoa tahadhari ya kutokea kwa maafa na kulinda usalama na maisha yako.
Baada ya kutoka, ukipanda Daladala au Matatu, BeiDou inaweza kujua mahali pa kila gari, na ukiona kibao cha kidijitali chenye vituo, utaweza kujua basi lijalo litafika baada ya dakika ngapi. Huduma hizo tayari zimetumiwa katika miji ya Shanghai na Beijing nchini China na kiwango chake cha usahihi ni asilimia 95.
Kama ukiendesha gari binafsi, programu za kuongoza safari zinazotumia huduma za Beidou zinaweza kutusaidia kukwepa msongamano wa magari. Hali halisi ni kuwa program nyingi za ramani zilizopo katika simu zetu zinatumia mfumo wa BeiDou. Habari zinasema duniani simu milioni 700 za aina ya Android zinatumia huduma za BeiDou.
Sasa unatoka kazini na kurudi nyumbani. Baada ya kula chakula, unataka kutazama televisheni, na unapata habari moja inayohusu kulinda wanyamapori. Kwa kutumia mfumo wa BeiDou, kila mnyama pori anaweza kupandikizwa kifaa mwilini mwake cha kujua mahali pake alipo, halafu walinzi wanaweza kujua mienendo yao ili kuzuia vitendo vya ujangili.
Mbali na kutoa huduma za uongozaji safari, BeiDou pia inaweza kutoa huduma nyingine nyingi. Kwa mfano, BeiDou ina vitu maalumu ambavyo havipo kwenye GPS. Kile kinachoonekana waziwazi ni ujumbe. Watejawanaweza kutumiana ujumbe mfupi kwa satilite. Bila kujali wewe upo katika jangwa lisilo na kivuli cha mti au bahari isiyo na mpaka, BeiDou inaweza kutoa huduma za uokoaji wa maisha yako.
Kama alivyosema msanifu mkuu wa mfumo wa BeiDou Bw. Sun Jiadong, “mipaka ya matumizi ya BeiDou ni kufikiria tu.”