Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 572
- 356
Mfumo wa Elimu ya Afrika tulioachiwa na Wazungu ni mfumo unaoharibu Akili na Saikolojia ya Wanafunzi.
Wazungu wao wanasoma Elimu ya Maarifa na Wanasoma Future, sisi Afrika tunasoma vitu visivyo na msaada katika Maisha ya kawaida na vingi ni Past. Elimu inakufanya utegemee kuajiriwa usipoajiriwa unapata Tabu kujikomboa kiuchumi.
Wazungu wanasoma vitu vilivyopo na vijavyo kwa hiyo Mwanafunzi anapata maarifa ya kuweza kuelewa Mambo yaliyopo na yajayo ili muda ukifika aweze kuishi na Mazingira anayoyakuta kwa wakati huo.
Mara nyingi Elimu ya Afrika tunafundishwa Vitu ambavyo ukihitimu Shule basi ulivyovisoma hautovikuta Mtaani, unafundishwa Maji Maji war sijui Vasco Da Gama alikuja mwaka gani, ukirudi Mtaani hautokutana na mambo hayo.
Njaa ikikuuma Mama Ntilie hatokuambia Taja mwaka ambao Maji maji war vilipiganwa ili tukupe Chakula.
Afrika tunajifunza vitu vilivyopita ambavyo haviendani na Mazingira ya sasa na havitokusaidia Chochote, Ulaya Wanafunzi hawafundishwi jinsi Wazungu alivyotutawala Waafrika, vitabu vya aina hiyo utavikuta Library ambapo mtu yeyote ataamua akasome au asisome.
Viongozi tulionao wametokana na Mfumo wa Elimu hii hii ndio maana wengi hawana Maarifa. Kauli yao ni Vijana mjiajiri wakati wao walishindwa kujiajiri.
Kijana amefundishwa Mambo ya Vasco Da Gama, amefundishwa kipeuo cha 2, amefundishwa Sehemu ya Kike ya ua inaitwa Sepali, amefundishwa jinsi kipepeo anavyozaliwa halafu unamwambia ajiajiri, atajiajirije wakati kichwani mwake kumejaa Matakataka hayo.
Mwanafunzi anakaririshwa mambo ya Zama za mawe, Kinjekitile, Vyura wanavyozalina halafu anaambiwa ajiajiri!
Source: FB, Romanticx Aloyce's post