Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 221
- 528
Kuanzia mwakani 2024 watumishi katika kada zote watatakiwa kuonyesha majukumu yao kwenye mfumo ambapo tathimini ya uwajibikaji wa kutekeleza majukumu hayo itafanyika kwa kutumia mfumo huo wa ki electroniki
Kwa mtazamo wa nje mfumo huo ni mzuri sana kwani baada ya tathimini kufanyika mtumishi asiporidhika na alama alizopewa mfumo unamruhusu kukata rufaa
Kwanini nasema wamekurupuka?
1. Semina elekezi kwa wasimamizi wa vituo ie, Wakuu wa shule, Mganga mkuu, Afisa kilimo nk sehemu nilipo mimi walifanyiwa kwa siku moja (Masaa matatu) ambapo walitakiwa pia na wao wakawaelekeze walioko chini yao
Tukumbuke kuwa kundi kubwa la watumishi hawana uwezo mzuri wa kumudu mifumo hii ya ki electronic. Wengi sana hizi simu janja wanaishia kusoma text kwenye watsap na kuangalia vituko vya kina Gigy money instagram
Category ya wasimamizi wa vituo ina vitu vingi ambavyo ni ngumu sana vya kufanya ambavyo ni vigumu sana mtu kuvimudu ndani ya muda mfupi wa masaa matatu hasa hasa kwa wale wasiomudu vizuri TEHAMA
Sasa hivi ukiwasikiliza wakuu wa shule, Afisa Elimu kata, Manesi, Waganga wafawadhi wa zahanati, vituo vya afya ni malalamiko ya chini chini kwamba hata hawaelewi cha kufanya
kumbuka hawa ndio wenye hatima ya kuamua performance ya mfanyakazi wanaye muongoza
2. Maeneo mengi hasa ya vijijini bado huduma za mtandao ni hafifu sana.
3. Mfumo wenyewe kuna wakati unakuwa chini kiasi cha kumkera mtumiaji
Hii itatumika kama utetezi kwa watumishi wengi
Nini kilitakiwa kifanyike
Kwanza kabisa naona utumishi walibuni mbinu ya kukwepa gharama kwani kwa eneo nililopo waliohudhuria hiyo semina elekezi hawakulipwa posho wala hapakuwa na chakula/chai
Inaonekana walikwepa gharama lakini gharama hizo hizo zimeenda kwa maofisa hao wanaozunguka kila wilaya kutoa mafunzo hayo ambayo ki ukweli hawana uhakika kama wanaopewa wanaelewa kwani hakuna session ya evaluation (nazungumzia eneo nililopo)
Kwa mtazamo wangu, haya mafunzo hasa hasa kwa wasimamizi wa vituo hayakutakiwa kuwa chini ya siku mbili (nazungumzia siku mbili za masaa rasmi ya kazi)
Unapoleta kitu kigeni hutakiwi kuogopa gharama. Ukiuangalia mfumo ulivyo una vitu vingi sana vya muhimu ambavyo hawa wasimamizi wa vituo ukiwahoji hawawezi kufafanua vinamaanisha nini
Wengi walichofanikiwa ni kuwahimiza watumishi wajisajili, kupewa role na IT pamoja na kujaza task na sub task kitu ambacho kwa kweli kwa watumishi wa chini hata wasio na ujuzi mkubwa wa mambo ya mifumo ni rahisi sana kwao
Ngazi hiyo wengi wamemaliza sasa kigugumizi kimebaki kwa wasimamizi wa vituo kuendelea na hatua zinazofuata kama ku set performance indicators, kuweka weight, dates, nk nk
Wakiulizwa "baada ya hatua hii tunafanyaje"? Hawana majibu kabisa kabisa hadi utaona huruma. Yaani jibu rahisi ni "subirini". Hii ni kuwaonea viongozi wetu huku vituoni!
Binafsi nawatetea kwasababu ya namna walivyokuwa trained kwa zimamoto kana kwamba na wao wameshiriki kuandaa huo mfumo. Shida inazidi kuwa kubwa zaidi kwasababu wao nao wanaogopa kuhoji au kuusema ukweli kwasababu ya nafasi zao. Huu nao ni udhaifu wa viongozi wengi wa kuteuliwa
Nashauri Utumishi waandae program maalum upya ambayo itakuwa na sessions za kujiridhisha kama walengwa wameelewa wanachotakiwa kwenda kufanya vituoni na kituoni watoke angalau watu wawili ili pawe na backup vinginevyo wataanza kutoa lawama na vitisho kumbe somo halikueleweka kwa kisingizio cha muda hautoshi
Jambo kubwa na muhimu kama hili halitakiwi kufanyika kwa mtindo wa zima moto, lipewe muda watu wajifunze, waelewe halafu ndipo waanze rasmi