KERO Mfumo wa Ajira Portal upo kama Roboti, hauwezi ku-synchronize sifa katika qualifications za elimu

KERO Mfumo wa Ajira Portal upo kama Roboti, hauwezi ku-synchronize sifa katika qualifications za elimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

NBica

Member
Joined
Sep 13, 2010
Posts
44
Reaction score
40
Ajira portal na serikali yetu mfumo wa ajira ni mgumu sana kuutumia, yaani upo kama roboti hakuna integration na una kinda of conservative mind imagine.

Kwa mfano
1.
Mtu amesoma kuanzia Form 1 hadi 6 masomo ya biashara let say form 1 hadi 4 (business studies) then 5 na 6 (ECA) yaan Economics Commerce na Accountancy halafu sasa huyu Mtu akaamua asiende chuo ila akaenda NBAA kujisajili akaanza level za chini za CPA mpaka akamaliza na kuwa Certified Public Accountant (CPA).

Imagine huyu mtu hawezi pata kazi Serikalini kupitia mfumo wa Ajira Portal na hata akipata siku atakayoenda ku-report watamkataa watasema kwamba hana degree au diploma ya accounting ya chuo wakati hiyo Diploma au Degree haifiki hata kidogo CPA na mambo ya kwenye degree ni machache mnayosoma kuliko CPA pia ni level ya juu kabisa ya uhasibu kuliko Shahada yoyote ya uhasibu.

2. Mtu Huyu wa pili unakuta amesoma Science au Art hadi form 6 then chuo akaamua asome course ya accounting yaani bachelor, huyu Mtu ajira portal anakubalika chapu sanaa na haraka bila shaka.

Sasa mwisho wa siku huwa tunajiuliza kuna haja gani ya CPA au hii professional kusoma na pia kama mfumo wetu wa ajira hauwezi ku-synchronize sifa mbalimbali katika qualifications zetu huo mfumo hautufahi maana unakuta labda sometimes jina tu la course linamkosesha Mtu Kazi na kipindi hiko anakuwa ashareport kama hiyo issue mlio address hiyo ya UDOM.

Serikali yetu wala haina habari wakati vijana wengi wanateseka na inashindwa kuelewa kuwa sio kila mtu lazima apitie chuo maana kuna professional board kibao ambazo zinatoa quality education kuliko chuo ambapo unaweza kuchonga na lecturer na ukafaulu.

Nashukuru Sana na hongereni kwa Kazi nzuri mnayofanya Wana jamii.

Pia soma ~ Mfumo wa Ajira Portal unatutesa, mamlaka husika ifanyie kazi changamoto hii
 
Back
Top Bottom