SoC02 Mfumo utakaosaidia uendeshaji na usimamizi wa taarifa muhimu kwa Serikali za Mitaa katika kila Kata ndani ya Wilaya

Stories of Change - 2022 Competition

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,208
1,755
UTANGULIZI.

Upatikanaji wa taarifa mbalimbali kwa haraka ni suala muhimu sana kwa nchi zinazoendelea na zilizoendelea, njia nyingi zimekuwa zikitumika katika utatuzi wa changamoto hii ya upatikanaji wa taarifa muhimu .

Mfano wa njia hizi ni kama uundwaji wa mifumo ya hifadhi taarifa ya kidijitali. Mifumo hii imesaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka kwa kuwa taarifa zote huifadhiwa katika eneo moja ambalo ni rahisi kulifikia mara baada ya taarifa kuchakatwa.

Mfano wa taarifa hizi muhimu ambazo huweza saidia serikali za mitaa katika maendeleo na mikakati mingineyo ni kama vile idadi ya wakazi, wakazi wenye ajira na wasio na ajira, vifo vya mara kwa mara na taarifa zinginezo muhimu.

Mambo muhimu yaliyonichochea kuweka wazo hili hapa kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza nililiweka katika jukwaa la sayansi bila maelezo yanayojitosheleza ni kama ifuatavyo.

  • Kukosa taarifa muhimu zinzoendelea katika mitaa tunayoishi kwa kuwa unaweza safiri kwa muda au sababu nyinginezo.
  • Kutopata nyaraka toka kwa mkuu wa mtaa(mtendaji au mwenyekiti) wako kwa haraka hasa unapokuwa mbali, mfano wa nyaraka hizi ni kama vile barua za ushahidi na makazi.
  • Kupata shida juu ya taarifa za nida na usajili.

Mara nyingi serikali za mitaa na viongozi wake bado wanatumia njia hafifu za uwasilishaji wa taarifa mfano matumizi ya vipaza sauti ambayo ni utamaduni wa kizamani kwa kuwa vipaza sauti vinaishia eneo moja lenye mikusanyiko na wakati huo kuna walemavu wasiosikia na watu wengine wako bize na kazi zinazowafanya wasipate sauti kutoka kwenye vipaz sauti vya watendaji wa mitaa. Hii upelekea watu kutoshiriki matukio muhimu ya mitaa yao.

Vile vile Kukosa nyaraka muhimu zinatakiwa na taasisi flani kwa ajili ya uthibitisho flani kwa kuwa muhusika yuko mbali hivyo kupelekea kutumia gharama nyingi katika utatuzi wa jambo hili.

Na mwisho ni ufuatiliaji wa taarifa za NIDA ambapo ni mpaka uende NIDA au ofisi ya serikali ya mtaa wako ambapo wakati mwingine mnakuwa wengi eneo moja au kuwa na mizunguko mingi mfano unaweza kwenda ofisi ya serikali ya mtaa wako na ukaambiwa uende NIDA na unapofika NIDA unaambiwa urudi tena serikali ya mtaa wako(huko Kata).

Hivyo kwa kuona changamoto hizi basi niliweza kuandaa mfumo huu utakaokuwa ukifanya kazi ya kutatua changamoto hizi tatu,

Mbali na utatuzi wa changamoto hizi, mfumo utaweza kusaidia hasa nyakati za SENSA zifikapo hakutakuwa na haja ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa kuwa taarifa zote muhimu za wakazi na makazi zitakuwa hapo Kata, hivyo wataalamu wa SENSA watapata taarfia muhimu kutoka kila mtaa ndani ya kata kwa kuwa kila mtaa na wakazi wa mtaa husika watakuwa humo ndani ya mfumo na taarifa zote muhimu bila muingiliano wowote kwanzia wadogo mpaka wakubwa. Pia usajili wa wakazi kwajili ya kutuma taarifa kwenda NIDA utafanyika hapo hapo ofisi ya serkikali ya mtaa(Mara nyingi Kata).

UTENDAJI KAZI WA MFUMO

Wasimamizi wa mfumo huu wenye taarifa za wakazi wa mtaa husika ni Mtendaji wa mtaa(uwezo wa kusimamia kila aina ya taarifa nitaweka baadae), mwenyekiti(uwezo wa kusimamia taarifa kadhaa), balozi(yuko chini ya mwenyekiti) na wajumbe.

Kabla ya kuelezea kazi zao kiufupi niweke namna mfumo unavyofanya kazi.

Ukiwa kwenye kurasa ya kuingilia utaweka jina la kuingilia na nywila, endapo utakosea mara tatu basi itabidi usubiri baada ya dk 30 hii hata uzime na kuwasha computer hautaweza labda ubadili ip address au saa ya computer. Hii inasidia kiulinzi.

Endapo utasahau nywila basi itabidi ufanye marejesho ya akaunti. HII ni kwa wasimamizi niliowataja hapo juu.

Mradi umegawanywa katika sehemu tatu,

Eneo la wakazi(haihitaji kuingia ndani ya mfumo bali utaweza ingiza namba ya simu au nida na kuweka maombi au maoni yako na mfumo utajua unakupeleka mtaa gani kulingana na ulikosajiliwa),

Eneo la viongozi wa mitaa na msimamizi mkuu
mfano iwapo kata ina mitaa 25, mfumo utawatambua viongozi, wakazi , nyaraka, matukio, maombi, matangazo na mengineyo kulingana na mitaa yao bila kuchanganya taarifa.

Wakazi wanaweza kuomba Barua za utambulisho kwa taasisi fulani, Kuomba/kuulizia kitambulisho cha nida ikiwa kiko tayari, Kutoa malalamiko na mapendekezo katika mitaa yao.

Viongozi wanaweza kusajili mwanachama mpya wa mtaani, na uwezo wa kuunganisha taarifa za mwananchi kwa NIDA api kwa MAOMBI YA KITAMBULISHO CHA NIDA(Hakuna haja ya mwananchi kwenda kujiandikisha NIDA katika ofisi ya NIDA) kipengele hiki kinapatikana katika hali ya test kwa sasa.

MAONGEZEKO
Anachoweza kuona kiongozi wa mtaa

Anaweza kuona idadi ya raia, kaya, viongozi, hati rasmi, kutuma tangazo kwa raia wote kupitia nambari za simu za raia zilizosajiliwa, kipengele hiki kinafanya kazi kwa sms api.

Vipi kwa mkazi

Anaweza tuma aina yoyote ya ombi au pendekezo kwa viongozi wake wa mtaa

Anaweza pokea taarifa na arifa muhimu kupitia ujumbe wakati ombi lako limechakatwa

NB: MNSIMAMIZI MKUU WA MFUMO NI MTENDAJI KATA NAYE ANAW3EZA KUONA TAARIFA ZA MITAA YOTE NDANI YA KATA BILA KUFANYA EDITING ISIPOKUWA KWA MAMBO MUHIMU TU.

Mambo hayo ni kama kuona idadi ya wakazi na viongozi wa kata nzima, waliokufa na waliopo na kubadili uongozi kwa watendaji.

FAIDA ZA MFUMO

Mfumo husaidia kwenye swala la upatikanaji wa taarifa na nyaraka muhimu kutoka kwenye mtaa unaoshi hata kama umesafiri kwa muda.

Mfumo unarahisisha usajili wa wakazi na utumaji wa taarifa zao kwenda NIDA ili kupata vitambulisho na NIN zao kwa haraka.

Mfumo unasaidia wakazi kutoa taarifa kwa vongozi wao juu ya matukio yanayoendelea mtaani na mapendekezo ya kimaendeleo.

CHANGAMOTO ZA MFUMO

Ofisi nyingi za mitaa ni nyumbani kwa kiongozi na mara nyingi zinategemea ofisi ya Kata ambapo miundo mbinu ya ICT ni hafifu kwani zingine hazina umeme.

Viongozi wengi wa serikali za mitaa ni watu local ambao hawana elimu ya mjuu angalau diploma.

Hii upelekea kuona suala kaa hili ni jipya na ni gumu.

HITIMISHO

Kutokana na kukosa taarifa muhimu na kupelekea kutokea kwa changamoto mbalimbali kama nilizozitaja hapo awali, Basi kupitia mfumo huu itakuwa ni rahisi kwetu kwenda na wakati na kuukomboa muda. kwani kupata taarifa, kutoa maoni na kuomba nyaraka muhimu kwa kumerahisihwa kwa mustakabali wa maendelo ya uchumi wetu.

kiungo rejea
 
Hii upelekea kuona swala kaa hili ni jipya na ni gumu.

HITIMISHO

Kutokana na kukosa taarifa muhimu na kupelekea kutokea kwa changamoto mbalimbali kama nilizozitaja hapo awali, Basi kupitia mfumo huu itakuwa ni rahisi kwetu kwenda na wakati na kuukomboa muda. kwani kupata taarifa, kutoa maoni na kuomba nyaraka muhimu kwa kumerahisihwa kwa mustakabali wa maendelo ya uchumi wetu.

kiungo rejea
I like the Idea, Lakini una kazi kubwa ya kufanya kuendesha huu Mradi, kwa sababu unaelenga kumpa huo mfumo ni Mwenyekiti au Mtendaji (Mtu huyu Ni Duni katika utambuzi wa masuala ya Tehama, hana lolote analolijua katika Sayansi ya Technologia.

Mfano, Wizara ya Afya kupitia Wahisani wameanzisha Technologia ya VISHIKWAMBI kutuma taarifa lakini nahisi Ni Mradi ambao haufanyi kazi kwa 96%. Ukifatilia Kuna changamoto kubwa sana katika Matumizi ya App kwenye level ya vijiji na mitaa.

Fikiria Tena nàmna Bora ya kutegeneza mfumo huo uwe rafiki kuendana na Mazingira ya Vijijini na Aina ya Watumiaji.

But it's a good idea
 
Back
Top Bottom