MFICHA UCHI HAZAI..👐

MFICHA UCHI HAZAI..👐

Jack Ma ana utajiri hivi sasa unafikia usd dola bilioni 41.5...

Huyu jamaa aliomba kazi KFC ,imagine KFC ni kazi ya chini kabisa inayo dharaulika huko ughaibuni ni kama tu McDonalds, katika watu 24 yeye akiwemo , 23 walipita na kupata kazi yeye akakataliwa...

Akaenda ku apply kwenye kazi ya polisi China, walikuwa wanne, watatu(3) wakapata yeye akakosa...

Akaomba kazi yeye na cousin wake kwenye Hoteli ya nyota nne, licha ya cousin wake kupata alama ndogo kwenye evaluation kuliko yeye kwenye hio kazi , Jack Ma akakosa kazi na cousin wake akaajiriwa...
Licha ya hayo yote, Jack Ma alikosa hata nafasi kwenye college entrance exams pale China..

Badala yake akaajiriwa kwenye college ambayo ni local , baadae aka apply Havard kama mwalimu wa Kiingereza kama mara 10 na bado alikosa ajira..

Ma akaendelea na kazi kwenye kazi yake kama mwalimu wa Kiingereza kwenye local college akalipwa dola 12 kwa mwezi..
1995 alipokwenda US ndipo anafahamu kuhusu internet , ndipo akaanzisha Alibaba mwaka 1999 kwemye apartment yake..

Ndipo akawa tajiri hadi leo..
Ingekuwa Bongo ndipo unahisi umerogwa...

Mungu anapofunga mlango elewa tu hio njia haikuwa inakufaa kwa potential uliyonayo , ama ulipaswa kuwa na mafanikio zaidi...

Imagine Jack Ma angekubaliwa kuwa police, mwalimu ama mfanya kazi wa hoteli asingekuwa hapo alipo.... Mungu huwa ana makusudi yake...

Sisi tunaona sehemu ndogo sana ya maisha yetu ila Mungu anaona ramani nzima ya maisha yetu..

Nikutie moyo endelea kupambana, labda kuna kitu kizuri mbeleni...

Lakini mimi sio motivational speaker 😁😁...
Mungu akubariki Motivationall speaker.Umetutia moyo jobless.
 
Back
Top Bottom