Mfanyibiashara............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyibiashara.............

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by WomanOfSubstance, May 9, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Katika jamii, mtu hutambuliwa kwa shughuli aifanyayo inayompatia namna halali ya kuishi.Tanzania tuna wakulima, wafanyakazi,wafanyabiashara, wajasiriamali na wale wasiokuwa na shughuli zinazoeleweka.

  Tatizo kubwa liko kwenye hili kundi la mwisho.Ni kawaida kuona au kusikia mtu akitambulishwa au akijitambuslisha kama mfanyabiashara hata kama hana shughuli maalum inayoeleweka.Je Mfanyabiashara hasa ni nani? Kwanini watu hawajitambulishi kama wakulima au wafanyikazi.

  Jana kuna mtu mmoja alisemekana kuingia Ikulu na kuiba ua la shilingi 5,000/- Katika mashtaka yake particulars zake zinaonyesha kuwa yeye ni mfanyabiashara .... hii inafanya mtu ajiulize: Kama huyu ni mfanyabiashara kweli, huo muda wa kwenda kuzurura hadi akashawishika kuiba ua, nani alikuwa anasimamia biashara zake?

  Je hakuna kundi tunaloweza kuwaweka hawa watu wasiokuwa na shughuli maalum badala ya kuwabatiza " wafanyabiashara"? Angalau nchi za wenzetu kuna watu wanajulikana kabisa wako kwenye " welfare". Je Tanzania hawa tuwaweke wapi maana hatuna utaratibu kama huu?

  NB: TAFSIRI YA MFANYABIASHARA KUFUATANA NA KAMUSI:
  businessman - a person engaged in commercial or industrial business (especially an owner or executive)
  man of affairs
  amalgamator - a businessman who arranges an amalgamation of two or more commercial companies

  arb, arbitrager, arbitrageur - someone who engages in arbitrage (who purchases securities in one market for immediate resale in another in the hope of profiting from the price differential)

  big businessman, business leader, magnate, top executive, tycoon, baron, mogul, king, power - a very wealthy or powerful businessman; "an oil baron"

  bourgeois, businessperson - a capitalist who engages in industrial commercial enterprise

  industrialist - someone who manages or has significant financial interest in an industrial enterprise

  oilman - a person who owns or operates oil wells

  operator - someone who owns or operates a business; "who is the operator of this franchise?"

  owner, proprietor - (law) someone who owns (is legal possessor of) a business; "he is the owner of a chain of restaurants"

  small businessman - a businessman who runs a business employing less than 100 people

  suit - (slang) a businessman dressed in a business suit; "all the suits care about is the bottom line"

  syndicator - a businessman who forms a syndicate

  transactor - someone who conducts or carries on business or negotiations

  Hawa ma jobless wetu wana fit kwenye tafsiri gani hapo juu?

  Naomba maoni yenu.
   
  Last edited: May 9, 2009
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  womenofsubstanc,
  Umenikumbusha awamu fulani ya uogozi kulikuwa na MAWAZIRI WASIO NA WIZARA MAALUM!

  sasa unaonaje kama tukawaita WAFANYABIASHARA DOGO DOGO WASIO NA BIASHARA MAALUM?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  UMENICHEKESHA SANA NDUGU YANGU....
  HUJAKOSEA.... hebu tusikie na wengine wanasemaje.
   
 4. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hawafiti kokote Wos......ndio maana kuna makosa ya uzururuji...yule anaweza itwa mzururuji....na anatumia jina la mfanya biashara kwa kuwa bongo...ni ngumu ku track mtu anafanya biashara...gani...kama vile nikisema mie ni mkulima..siku nikinunua mcheke kisesa nikauza pasiansi..hata bila TIN number basi nshakuwa mfanya biashara..so hata polisi wakikukamta ukawaambia wewe ni mfanya biashara hawana muda wa ku track ni nini bishara wafanya....so ndio maana watu wanaona easy tu kusema mkulima au mfanya biashara.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Utashangaa hata wanaokamatwa kwa kosa la uzembe na uzururaji, charge sheet inasomeka
  Jina:-------
  Kabila:-------
  Umri:------
  Kazi: Mfanyabiashara!

  Hao ni polisi waliomkamata kwa kuzurura na kukosa makazi maalum( rogues, vagabonds, no fixed abode) wanaomwita
  " mfanyabiashara".Kumbe wangeweza wakaandika hana kazi maalum
  Wanadhalilisha wafanyabiashara wa kweli.
   
 6. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Regardless ya hizo definitions za wazungu hapo juu, ukifikiria sana utagundua kuwa almost kila mtu ni mfanyabiashara kwa kuwa somehow, somewhere kila mtu atajikuta 'anauza' kitu fulani. Mkulima anapovuna mazao yake huishia kuyauza. Hata mfanyakazi naye ni mfanyabiashara kwa kuwa anauza skills zake kwa muajiri na pia imekuwa ni common kwa waajiriwa kujihusisha na shughuli za kibiashara- hata ukiwa na kihiace unaingia kundini! Changuduo naye anauza mwili wake, vibaka wakiiba vitu huwa wanaviuza, etc. Ufanyabiashara hauepukiki.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  "........... Sisi twaelewa, anafanya biashara. Na hiyo biashara, anajua mwenyewe......"

  Anzia dakika ya 2:00

  [ame=http://www.youtube.com/watch?v=5JbwXlTnTGg]YouTube - SWAHILI SONG-sigalame issa juma[/ame]
   
 8. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Enzi za Mwalimu watu ambao walikuwa hawana shughuli maalum a kufanya waliitwa "wakulima". Kuna jamaa yangu mmoja aliomba pass ya mchele aende nchi jirani, pale panapo kazi alijaza mkulima
   
 9. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Kwa maana hiyo ukiwa unauza chochote kile automatically unakuwa mfanyabiashara?
  Je kuna tofauti gani kati ya mjasiriamali na mfanyabishara?
   
 10. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  WoS,
  Nadhani tungewaweka katika kundi la watu wasio na shughuli maalumu.
   
 11. Mathayo Christopher

  Mathayo Christopher Verified User

  #11
  Mar 7, 2015
  Joined: Dec 15, 2013
  Messages: 336
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Tuwaite madalali
   
Loading...