Mfanyakazi wa Ubalozi wa Canada adaiwa kumtemea mate Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyakazi wa Ubalozi wa Canada adaiwa kumtemea mate Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Bongolander, Dec 10, 2009.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mzungu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mfanyakazi wa ofisi ya ubalozi wa Canada nchini hapa, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumtemea mate askari wa usalama barabarani (Trafiki) aliyekuwa akiongoza magari, Jijini Dar es Salaam.

  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema tukio hilo la aina yake lilitokea jana saa 8:15 mchana eneo la Ukonga Banana, barabara ya Nyerere Jijini.

  Kamanda amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Gean Touchatte, 48, ambaye imeelezwa kuwa ni Katibu Mhitasi wa ubalozi huo.

  Akisimulia tukio zima, Kamanda Shilogile amesema kabla ya tukio hilo, trafiki mwenye namba NCO E1653 Koplo Samson, alikuwa kazini akiongoza magari katika barabara ya Nyerere pale Ukonga Banana.

  Akasema wakati huo mtuhumiwa huyo alipita akiendesha gari lenye namba za usajili T 17 DC 178 aina ya Toyota Land Cruiser, akitokea Ukonga kwenda Uwanja wa Ndege.

  Kamanda Shilogile amefafanua kuwa mtuhumiwa huyo alipomkaribia trafiki, alipunguza mwendo, akashusha kioo cha gari, kisha akamtemea mate askari kabla ya kuongeza mwendo na kuondoka.

  Kwa mujibu wa Kamanda Shigolile, trafiki alitoa taarifa za tukio hilo kwa wenzake kupitia `redio callÂ’ za polisi, juhudi zilizosababisha gari hilo kufuatiliwa.

  Amesema gari lilipofika maeneo ya Kamata, lilikamatwa na askari na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

  Kamanda amesema wakati mtuhumiwa huyo akiendelea kuhojiwa kituoni hapo, alifika mwandishi wa habari wa TBC, Jerry Muro akiwa na nia ya kumhoji lakini naye inadaiwa aliishia kutemewa mate yaliyompata chini ya kidevu na kuenea upande wa mbele wa fulana aliyokuwa amevaa.

  Amefafanua kuwa kutokana na kitendo hicho, mwandishi huyo alifungua jalada la mashtaka ya shambulio kituoni hapo na kufunguliwa jalada namba CD/102/4818/2009.

  Kwa mujibu wa Kamanda Shilogile, mtuhumiwa huyo hakuwa tayari kutoa maelezo yoyote, kwa madai kuwa atafanya hivyo pindi akiwepo balozi wa nchi yake.

  Aidha, akasema fulana ya mwandishi Jerry Muro iliyotemewa mate, imehifadhiwa katika Kituo cha Polisi Kati kwa ajili ya ushahidi na mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa na Polisi.


  CHANZO:
  ALASIRI /ippmedia.com

  WanaJF, sasa tumefikia wakati hata idara zetu za usalama zinadharauliwa mbele ya macho yetu. Nafautilia kuona ni vipi serikali yetu inafuatilia hili. Najua nini kingenipata kama ningefanya hilo hilo Canada.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii ni aibu kwa ubalozi wa Canada nchini na pia ni fedheha kwa serikali yetu.
  Inapofikia mgeni kuitukana crown basi tujue kuna tatizo.
  Hili ni fundisho ifuatavyo:
  1. Wakati wageni wanaendelea kudharau watanzania kila siku, tumekuwa tukiwatukuza na kuwachekea.Ukimchekea nyani utavuna mabua.
  2. Traffic nao wamezidi kuwa kero japo hii haitoi sababu kufanyiwa dharau kama hivi
  Wito:
  Watanzania tuamke, tuache kuwaabudu wageni - hata kama wanatupa misaada. Bora utu kuliko mali!
   
 3. Einstein

  Einstein Senior Member

  #3
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni aibu sana..

  Pole bwana Jerry Mulo na Trafiki... This not fair. Huyo jamaa inabidi wamweke jela kwa muda fulani. Sitaki wampe adhabu ya kulipa fidia na kumfukuza nchini. Inabidi wamtandike na virungu, ili tuheshimiwe. Kama wakimwambia alipe tu,,, aaaaaah jamaa litacheeeeeeeka maana pesa linazo...
   
 4. I

  Inviolata Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wewe mtoa mada na mimi nadubiri sana nione serikali itafanya nini. Hawa watu wana dharau sana kwa kweli. Jaribu kufanya hivyo ukiwa kwao ndio utajua ngozi nyeupe ilivyo.

  Serikali sijui bado inasubiri nini, Huyo mtu alitakiwa kuwa kuondolewa nchini na hakuna kukanyaga tena ardhi yetu, na hii ni baada ya yeye kutemewa mate na askari yule yule, then he will feel what they felt (askari na J.Muro).
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kiutaratibu, hakupaswa hata kupelekwa polisi, badala yake alipaswa kupewa 24 hours notice ya kuondoka nchini kama ambavyo wao wanatufanyia tukiwa nchini kwao. Nitaishangaa serikali kama itamchekea, au itaanza kumfungulia mashitaka mahakamani yasiyokuwa na mwelekeo. Afukuzwe!
   
 6. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kudadadeki..............!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wanadhani diplomatic immunity ni leseni ya kufanya kila watakacho bila woga wala wasi!
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa nini huyo trafiki asingelamba angalau ngumi mbili....
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ngumi isingekuwa nzuri, flog would be better
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ushahidi wa mate kwenye fulana na Jerry utakuwepo kweli baada ya masaa machache!?
   
 11. Visible

  Visible Senior Member

  #11
  Dec 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Masanilo<>NIPENI RUHUSA TUMPOTEZEE HUYU:
  fUNGUA MABANO funga mabano unavotaka;
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Dec 10, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimi mtu akinitemea mate wala hatutafikishana mahakamani. Judge, jury, executioner ntakuwa mwenyewe. Lazima aondoke na nundu..
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama kweli hili limetokea huyu mtu hata credentials zake za ubalozi zinatia shaka, tutaanza kufikiri kwamba kwa kuwa mtu wa ubalozi yuko hivi basi ni representative wa wa-Canada, which is not fair.

  Huyu anaweza ku-invoke diplomatic immunity kirahisi, lakini ubalozi wa Canada kama unajua whats good for them na hautaki kuonekana unafuga watu washenzi ni bora wangemrudisha kwao.

  Unfortunately watu wa ubalozi kuwashitaki ni tabu sana, hasa kwa kesi kama hii.
   
 14. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  safi sana sa ingine unakua kama sio miafrika,mi alishawai kufanya ivyo kaburu mmoja hapo bongo kibonge cha mtu,ngumi iliyochomoka hapo ilikua kama bomu la atomiki maana alipaa kama kishada na kaenda kudondokea kwenye jiko la moto,mpaka hapo yeye ndo alipiga simu polisi kudadadeki
  na polisi kwenyewe tukamtengeneza tena vizuriii,si unajua polisi wetu ukiwachongea dili la uhakika wakamgeuzia kibao,mpaka ilibidi aombe samahani akadai alikua anaongea na mimi ndo mate yakanirukia,aah alinilipa fidia ni kama kamshahara ka mwaka mzima nilikua homu nakula bata tu,sema kibarua kiliota mbawa.sometime inabidi tuwe wakali hii yes yes itatumaliza ndio mana wakenya wanatuona mafaaala.
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Dada yangu, leo wakati narejea, kitu cha kwanza dereva wa teksi pale airport alichoniambia ni hiyo habari... kusema kweli nilichukia sana maana wanatudharau, ila sikutegemea kwamba itafikia hatua hii ya kututemea mate tena siyo mara moja!!!

  Mawazo yangu

  1. That guy, ni vyema wanaharakati na wanasheria wangetusaidia kusema hatumtaki
  2. Pia nadhani kuna namna ya petition kwenye mitandao ambayo tunaweza ku-narate hbari na kusambaza email ya kila mtu kutia saini kulaani kitendo hicho
  3. Wataalam tusadieni tupate japo picha yake, ili popote takapoonekana hapa bongo azomewe hata kama ni kwa pesa!!
  4. If he was good enough, asingekuwa anahangaika na jua la bongo, angebaki kwao akipunga upepo

  He came, he saw, he spat!!!
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  That was my question too... traffic angeleta drama kiswaziswazi bila hata ya yeye kumgusa halafu mzungu apewe na watoto wa kitaa... yaani nimesikitika sana jinsi mzungu alivyoamua kututusi namna hiyo
   
 17. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajua Tanzania ni nchi ambayo haina utawala wa kisheria , Na kama zipo ni kwa walala hoi . kwahiyo hawa wazungu au wenye uwezo wanaweza fanya lolote pasipo kuwa na hofu..!

  Wazungu wakishagundua kwamba sheria za nchi hazifuatwi waweza kukufanyia jambo lolote baya au lenye maudhi wakijua kwamba hata ukishtaki watakushinda bila shida wala pingamizi..!!!

  Balozi wao akija anamtetea bila shaka..Si wajua Tanzania wapata misaada mingi toka kwao !!!! SHAME US !! Mkuu akachukue tu Tshirt yake akafue...Au anasubiri kipande cha Sabuni ??
   
 18. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Haiyumki
  niki mijitu inayojinadi kuwa ni waasisi wa ustarabu kufanya upuuzi kama huu. Polisi nanyi vipi mmelogwa? Kwa nini hapo kituoni alivyokuwa anaendeleza jeuri yake ya ki- barbarian hamjampa kibondo? Sasa tunaiomba serikali yetu imfukuze nchini kwa notes ya saa 24 na kabla ya kuondoka atiwe ndani ya tenga la nyanya pale airport kwa zoezi la kutemewa mate na kila raia.
   
 19. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hakuna sheria ya Jinsi hiyo Tanzania ,Punguza makali , Police wanaweza kukufanyia wewe hivyo lakini si kwa mzungu.. Kuna jamaa juu ka kwamba mbia "THIS IS BONGO LAND" !!!!!!
   
 20. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka mkuu ...Punguza chuki !! Subiri kwanza rufaa zidi ya Zombe, wakishinda tena ndipo tutatoa hukumu kwa Mzungu !!! Jibu lipo kwenye Mabano !!!!!
   
Loading...