Huu ni ufedhuli mkubwa. Ni nani hapa angependa siku anapata stroke ama hata inatokea ajali na yeye kupoteza viungo kisha mkewe afungue milango kwa whatsoever called Serengeti boys? Kama yupo ajitokeze hadharani tumjue.
Ni vema kutambua ya kwamba hata kama jamaa kweli kapoteza nyezi zake kwa sababu yoyote ila, mkewe atabaki kuwa mkewe na wala hatakuwa "shamba la bibi" kila mjukuu kujichunia chochote apendacho na wakati apendao.
Ni busara isiiyo aghali kuzingatia mahusiano yenye maadili na heshima, kuliko tukianza kuhubiri ukosefu wa nidhamu, uasherati na kushabikia uzinzi.
Pia ni muhimu kutambua kuwa, ikiwa ni kweli yamemkuta jamaa, yeye, mkewe na ndugu, jamaa na marafiki wa kweli watakuwa katika wakati wa majonzi na simanzi kwa kilichotokea. Kuwakebehi ni kukosa utu.
Katika akili ya binadamu wa kawaida sidhani kuwa wote waliofanyiwa vitendo hivi hawakushirikisha uamuzi, hisia na matakwa yao binafsi. Vinginevyo tayari kungekuwa na kesi lukuki za ubakaji juu ya jamaa.
Ninaloweza kuliona hapa, kama kweli wamewahi kufanyiwa hivyo na mtu yeyote yule, hayo ni matokeo ya uamuzi wao binafsi, iwe kwa kukidhi tamaa zao za kifedha au za kimwili.
Kisha ningependa kuwalaumu wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamejua kuwa wake zao, dada zao au wadogo zao wametumika visivyo halali, kisha wakabaki kumlaumu aliyewafanyia hivyo badala ya wao binafsi ambao waliamua kujitoa kiroho na kimwili katika hilo.
Natumaini umenipata mkuu.
Kuna taarifa kwamba mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam Ajulikanaye kwa jina la Mzamir hivi sasa hana tena uume baada ya kufanyiwa unyama wa kutisha huko China. Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mfanyabiashara huyo, Mzamir alitekwa na watu ambao inadaiwa aliwahi kuwatapeli madini huko Dar na baadaye wakamuwekea mtego ili aende China ambako alijikuta theatre akiwa hana uume. Aliokotwa akiwa hajitambui akakimbizwa hospitali ambako jamaa walichofanya ni kuzuia bleeding na kutibu kidonda. Naambiwa sasa hivi hana raha na nyodo zote zimemuishia.
Lyke...!..sidhani kama upo sawa kichwani la sivyo utakuwa mpambe wa pedejee Mzamir!..kama unaamini haya uliyoandika basi huwezi mtetea Mzamir kwa sababu hata yeye alivyokuwa ana dhulumu si alikuwa ana timiza matakwa yake ya kifedha sasa ameadhibiwa wewe una walaumu vipi waliomfanyia? Na wewe mlaumu yeye aliyeyataka basi!!! acha upambe nuksi!