MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Ni vyema nao watozwe. Hata hivyo,rate itakuwa kidogo sana kulingana na matumizi madogo ya mafuta. Pia itafidia madhara ya uharibifu wa mazingira kutokana na "greenhouse emission".
Hoja ya msingi.
 
Kupandisha bei ya mafuta kuna madhara makubwa kiuchumi kuliko unavyodhani, hivyo sio njia sahihi kuingiza road licence kwenye mafuta. Mpaka sasa karibu asilimia 50 au zaidi ya bei ni kodi. Vile vile mafuta ni nishati ambayo inatumiwa na viwanda, majumbani na katika uzalishaji mwingine usiohisisha matumizi ya barabara, kwa msingi huo road licence lazima iendelee kuwapo na huu ni mfumo wa dunia nzima.
Mkuu fanya utafiti wa kina kuhusu road license, ulizia hata kwa jirani zetu. Utakuja kugundua kuwa tatizo lipo kwa watendaji hazina na TRA. Hawataki kuumiza vichwa kupata mfumo mzuri usio gandamizi na utakaoiongezea serikali mapato. Serikali inahitaji mapato!

Mfano, katika vituo vyote vya mafuta wanapaswa kutumia mashine za EFD. Mashine hii inauwezo mkubwa sana wa kutenganisha bidhaa inayopaswa kulipiwa kodi au kutolipiwa kodi. Sasa ukianzia hapo hapo, kama kweli tumeajiri watu wenye weledi katika taaluma zao, mbona rahisi kukusanya hiyo kodi pasipo kumuathiri mtumiaji mwingine wa mafuta asiyemiliki gari.

Nini maana ya kuwa na TIN kama walioitoa hawawezi kuitumia kubainisha nani anapaswa kulipa kodi stahiki na nani hapaswi. Vichwa maji hawa.

Lakini kwakuwa watu wamerithishwa kazi na wajomba zao, hawawezi kuumiza vichwa, bora serikali ikose mapato lakini wao waendelee na mfumo rahisi kwa akili yao.
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!
Hata mm siipendi hii tozo, bora wangeweka kwenye mafuta tuu, hawa wanaojiita wasomi sijui wanafikiria kwa kutumia kiungo gani mwilini, eti wasomi, ha ha haaa amkeni "wasomi" wa TRA
 
Road licence ni jina tu lakini ni Adhabu ya kumiliki Gari
Kwa kuwa hutozwa kwa kila anayemiliki gari hata ikiwa mbovu. Na njia pekee ya kuikwepa ni kuifuta gari yako kwenye mtandao wa TRA
Maana ingekuwa ni kodi kama jina linavyoitwa ingekuwa gari mbovu inatolewa taarifa na kusitisha utozaji lakini sivyo kabisa
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!
petrol inatumika kwenye magari tu? kwa hiyo 50 ni bei kubwa sana mkuu, ila ni hja nzuri inahitajika kuwa polished tu
 
Hata mm siipendi hii tozo, bora wangeweka kwenye mafuta tuu, hawa wanaojiita wasomi sijui wanafikiria kwa kutumia kiungo gani mwilini, eti wasomi, ha ha haaa amkeni "wasomi" wa TRA
Mkuu hatuna wasomi! Wanakila aina ya teknolojia inayweza kuwasaidia kukusanya kodi pasipo kuumiza watu, lakini akili zao mgando wanazidi kiikosesha serikali yetu mapato. Wakati umefika mkuu wa kaya ajaribu kumulika katika hizo ofisi, nadhani kuna vilaza wengi sana wamejificha humo.
 
petrol inatumika kwenye magari tu? kwa hiyo 50 ni bei kubwa sana mkuu, ila ni hja nzuri inahitajika kuwa polished tu
Hiyo 50 nimejaribu kutolea mfano katika namna ya kukokotoa tozo la road license. Inapaswa kuwa chinyi ya hapo.
 
Juzi ilizungumziwa bungeni. Ikajibiwa kuwa iko kisheria. Wanaufanya sheria kuwa korani au biblia. Wakishauriwa hawakubali mpaka waamue wenyewe. Ni kweli kuna mbadala wa kukusanya road lisence. Ikusanywe kulingana na gari linavyotumika barabarani. Wabadili sheria iwekwe kwenye mafuta.
 
Sio road licence tu,hata bima za magari zingewekwa kwenye mafuta na zingeliwekwa kwa staili ya compressive.
Stickers zibandikwe tu ili kuonesha kuwa insurer ni fulani,lakini kila kitu tayari kiko kwenye petrol/diseli.
Ni jambo la kutumia Tehama
cc. Ewura/Tra & co.
Note:Mbona makato mengine kwenye malipo yanalipwa na mlaji mfano Ewura .....% kwenye Maji na Umeme n.k
Sio hivyo tu mikokoteni,guta,machinga,baiskeli & like kama wanatumia barabara/maeneo kando ya, nao pia wawe na leseni/vibali maalumu.
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Ukisema hivyo unakosea maana kwenye importation magari pia huchajiwa rail levy japo hayatumii rail. Majenerata ni minor case can be ignored
 
Wananchi wengi wameanza kuelewa, lakini na walio bado gizani kujua nani analipa kodi bado ni wengi zaidi. Pote duniani mlipa kodi ni mlaji wa mwisho. Kupandisha bei ya petrol kufidia road licence utapata urahisi wa kukusanya kodi, lakini utavilipisha vyombo vingine vinavyotumia mafuta lakini havijui barabara, kama vile generator na boat za uvuvi na meli.
Ni kwa asilimia ngapi ya mafuta yanatumika kwenye vyombo hivyo? Mpaka sasa road toll inatozwa kwenye mafuta na vyombo hivyo vinadunda tu.
 
bei ya mafuta hata sasa tayari ina tozo ya barabara

hii ni moja ya kodi zilizokuwa double taxed
 
Kupandisha bei ya mafuta kuna madhara makubwa kiuchumi kuliko unavyodhani, hivyo sio njia sahihi kuingiza road licence kwenye mafuta. Mpaka sasa karibu asilimia 50 au zaidi ya bei ni kodi. Vile vile mafuta ni nishati ambayo inatumiwa na viwanda, majumbani na katika uzalishaji mwingine usiohisisha matumizi ya barabara, kwa msingi huo road licence lazima iendelee kuwapo na huu ni mfumo wa dunia nzima.

better u tell.....happy with ur comments
we need to think big on this as the impact is more that we talk or analys here
 
bei ya mafuta hata sasa tayari ina tozo ya barabara

hii ni moja ya kodi zilizokuwa double taxed
Kama mafuta yana kodi ya barabara why road licence?
Kama issue ni leseni ya mtumiaji wa barabara kwa maana ya road lecense ,why don't you include in its expenditures (fuel usage).kwa maana ya kuwa kadri anavyoitumia barabara ndivyo anavyolipa kodi/anavyoilipia.
 
Mimi nilikuwa na pick up miaka kumi iliyopita nikampa mwanangu aitumie imsaidie kimaisha . Lakini ghafla ikafa gear box . Aliacha pale garage na kuisahau . Mwishoni mwa Mwaka Jana tin yangu ikasoma Nina deni la road licence ya miaka kumi natakiwa niilipie . Kujitetea kwangu haikusaidia . Kutaka kuleta ushahidii toka garage wadhibitishe gari haikutembea na picha za kuonyesha ilivyopaki muda wote haikusaidia . Nilitakiwa nilipe road licence ya miaka kumi nikalipa kwa uchungu sana . Hatua iliyofuata ni process ya kwenda kuliondoa kwenye usajili ambapo nako kuna usumbufu sana hata baada ya kulipia .
 
idea nzuri sana lakini hawa TRA na wakulu wao wanawazaga ndani ya box tuuu, yani their not creative mshajua watu hawapendi kutoa hela nyingi Mara moja why wasitafute plan B. so stupid utasikia eti TRA wanaemploy First class tu idiots izo fake first class ndo zimepelekea kuwa maskini ivi mijitu inakazi yakucrem tu
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Mafuta ya jenereta yako unacho kisima nyumbani? Hutumii barabara kwenda kununua mafuta kituoni?
 
Hii ni fikra ya ajabu kbs, wewe unadhani kila anayetumia petrol/diesel anagari? wengine wanabodaboda,wengine bajaji,wengine majenereta.

Na ukumbuke wenye vibaby walker wanalipa kidogo kuliko haya magari yetu. utawaonea buree wenye magari madogo

utakuwa ni unyonyaji shahiri dhahir kbs
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Hoja yako nzuri sana, umeona mbali,
 
Back
Top Bottom