MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Wazo zuri. Ina maana kwa style hiyo, basi kubwa au lori,inaweza kufikisha 5M,kwa mwaka
Tuna kiu kubwa sana ya mapato.

Kama tunakusudia road license iwe 250000 kisha tukakubaliana tuihamishie kwenye mafuta basi hesabu zizingatie lengo (250000)

Unaweza kuta ni sh. 1.50 kwa lita na maisha yakasongo kiulainiiii.
 
Msingi wa kutoza kodi unategemea na elasticity ya kodi inayotozwa namna itakavyopokelewa au itakavyoathiri ukusanyaji wa kodi hiyo. Kwa kawaida watoza kodi wanajitahidi kubuni kodi ambazo ni inelastic (mlipa kodi kutobadilisha means zinazotozwa kodi) pamoja na kodi hiyo kutoathiri sana uzalishaji (distortions). Bahati mbaya sana yaonyesha kuna tatizo katika "national Tax committee" kama ipo. Matokeo yake, kodi zetu huwa mtu anaamka anaiwaza kisha anaitoza. Yaani hazizingatii elasticity wala economic distortions.

Juzi nilikuwa namsikia Mheshimiwa Rais akipendekeza kodi ya kitambulisho kwa machinga. Hii ni aibu. Serikali isikwepe wajibu wake. Biashara ya kuzunguka na bidhaa ni sawa tu na kilimo au ufugaji wa kuhamahama uliokuwepo miaka 2000 na zaidi huko nyuma. Kumtoza mtu kodi bila kujua unachomtoza ni kitu ambacho hakieleweki, mbali ya kuwa hakikubaliki katika ulimwengu wa watu waliostaarabika.

Serikali ikitaka kuchukua kodi kwa wafanyabiashara wadogo ianzishe projects kwanza za kuboresha masoko yetu yaliyopo ili yaweze ku-accomodate wafanyabiashara. Sidhani kama "Dar es Salaam Markets Rehabilitation Programme" iingehitaji mabilioni kama ya Terrible teens. Masoko yalioko Dar es Salaam yangejengwa kwa kiwango cha ghorofa 3-5 kwa kila soko na kuweka miundombinu ya kisasa yangeweza ku-accomodate machinga wote. Halikadhalika hiyo hali ingekuwa extended mikoani kote. Hili nijukumu la Serikali lazima walitekeleze. Nikipata muda nirachangia kwenye road lincense na pendekezo la mtoa mada.... no time now.
 
Hii ni fikra ya ajabu kbs, wewe unadhani kila anayetumia petrol/diesel anagari? wengine wanabodaboda,wengine bajaji,wengine majenereta.

Na ukumbuke wenye vibaby walker wanalipa kidogo kuliko haya magari yetu. utawaonea buree wenye magari madogo

utakuwa ni unyonyaji shahiri dhahir kbs

Vipi kuhusu waliopaki magari?
 
Wewe ni miongoni mwa wale wavaa tai wanaosemwa hapa na wadau.

Hoja sio kuondoa road license bali ni kutafuta an alternative way that could be viable & comprehensive katika kukusanya kodi hiyo na sio kuwa na mfumo mgumu ambao unawafanya wengi wafikilie kuikwepa na hivyo serikali kuwa na takwimu hewa za makusanyo wakati magari meengi yapo garage au yashachinjwa tayari kama skrepa. Angalia LUKU ya TANESCO ilivyo simpo

Kupandisha bei ya mafuta kuna madhara makubwa kiuchumi kuliko unavyodhani, hivyo sio njia sahihi kuingiza road licence kwenye mafuta. Mpaka sasa karibu asilimia 50 au zaidi ya bei ni kodi. Vile vile mafuta ni nishati ambayo inatumiwa na viwanda, majumbani na katika uzalishaji mwingine usiohisisha matumizi ya barabara, kwa msingi huo road licence lazima iendelee kuwapo na huu ni mfumo wa dunia nzima.
 
Wewe ni miongoni mwa wale wavaa tai wanaosemwa hapa na wadau.

Hoja sio kuondoa road license bali ni kutafuta an alternative way that could be viable & comprehensive katika kukusanya kodi hiyo na sio kuwa na mfumo mgumu ambao unawafanya wengi wafikilie kuikwepa na hivyo serikali kuwa na takwimu hewa za makusanyo wakati magari meengi yapo garage au yashachinjwa tayari kama skrepa. Angalia LUKU ya TANESCO ilivyo simpo
Luku sio simpo, 'yuniti' ni ghali sana ukilinganisha na kipato cha mtanzania wa kawaida.
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Point
 
hatutaki tena kodi kwemye mafuta,,,,zaidi ya nusu ya bei ya mafuta ni kodi
 
Vipi kuhusu waliopaki magari?

Kuna mzee mmoja katumiwa gari na mwanae Kama zawadi alitumie akistaafu . Kwa sasa ana usafiri wa kazini hivyo amelipaki akisubiri atakapostaafu aanze kulitumia . Mwaka wa nne sasa analipia road licence gari likiwa limepaki .
 
Road licence ni jina tu lakini ni Adhabu ya kumiliki Gari
Kwa kuwa hutozwa kwa kila anayemiliki gari hata ikiwa mbovu. Na njia pekee ya kuikwepa ni kuifuta gari yako kwenye mtandao wa TRA
Maana ingekuwa ni kodi kama jina linavyoitwa ingekuwa gari mbovu inatolewa taarifa na kusitisha utozaji lakini sivyo kabisa
Naomba nisaidie kujua jinsi ya kufuta gari ambalo halitumiki TRA
 
Sio road licence tu,hata bima za magari zingewekwa kwenye mafuta na zingeliwekwa kwa staili ya compressive.
Stickers zibandikwe tu ili kuonesha kuwa insurer ni fulani,lakini kila kitu tayari kiko kwenye petrol/diseli.
Ni jambo la kutumia Tehama
cc. Ewura/Tra & co.
Note:Mbona makato mengine kwenye malipo yanalipwa na mlaji mfano Ewura .....% kwenye Maji na Umeme n.k
Sio hivyo tu mikokoteni,guta,machinga,baiskeli & like kama wanatumia barabara/maeneo kando ya, nao pia wawe na leseni/vibali maalumu.
Kila kitu kwenye mafuta, kila kitu kwenye mafuta. Mwisho itapendekezwa kuwa hata gharama ya kuwalipa DADA POA na KAKA POA na yenyewe iwekwe kwenye mafuta
 
Hayo sasa ni yako Mkuu.
Ukipinga toa mbadala kuliko kunajisi hoja.
Kila kitu kwenye mafuta, kila kitu kwenye mafuta. Mwisho itapendekezwa kuwa hata gharama ya kuwalipa DADA POA na KAKA POA na yenyewe iwekwe kwenye mafuta
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!
You must be genius haya ndio mawazo ya kutoa kwa serikali yetu. Nakupa kongole.
 
We kweli ni thinker mzuri
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Hapo chacha
 
Back
Top Bottom