MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Kama mafuta yana kodi ya barabara why road licence?
Kama issue ni leseni ya mtumiaji wa barabara kwa maana ya road lecense ,why don't you include in its expenditures (fuel usage).kwa maana ya kuwa kadri anavyoitumia barabara ndivyo anavyolipa kodi/anavyoilipia.
hoja hapa ni kuondoa double taxation
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Jamani hakuna sheria ya kodi ambayo inatekelezwa bila kuumiza wachache.Tanzania hii Hamna mtu asiyetumia barabara iwe kwa mguu au baiskeli.
1. Kuna watu wanalipa kodi ya aridhi ya mashamba wanayomiliki wakati kunawengine Wanamiliki na kutumiwa mashamba makubwa bure hasa huko vijijini.
2.Kuna watu wanalipa kodi ya pango la aridhi kila mwaka walipojenga nyumba zao wakati wengine hawalipi, hasa vijijini
3. Kuna watu wanalipa kodi ya majengo wakati wengine hawalipi. Tena unakuta centre huko vijijini kuna nyumba za thamani kubwa kuliko hata za mjini, kuna mfumo wa maji na umeme lakini hawalipi .
4.Kuna biashara nyingi ambazo hazitambuliwi n.a. mfumo wa kodi,watu wanapiga pesa bila shida, mfano Madini, Nafaka, Udarali na wale Benki bubu wanaokopesha watu pesa kwa riba nk.
Mimi naomba Serikali ikubali pendekezo hili la kutoza kwenye mafuta. Watapata pesa nyingi bila usumbufu na bila kukera watu.
 
Jamani hakuna sheria ya kodi ambayo inatekelezwa bila kuumiza wachache.Tanzania hii Hamna mtu asiyetumia barabara iwe kwa mguu au baiskeli.
1. Kuna watu wanalipa kodi aridhi ya mashamba wanayomiliki wakati kunawengine Waikiki n.a. kutumiwa mashamba makubwa bure hasa huko vijijini.
2.Kuna watu wanalipa kodi ya pango la aridhi kila mwaka walipojenga nyumba zao wakati wengine hawalipi, hasa vijijini
3. Kuna watu wanalipa kodi ya majengo wakati wengine hawalipi. Tena unakuta centre kuna nyumba za thamani kubwa kuliko hata za mjini, kuna mfumo wa maji na umeme lakini hawalipi .
4.Kuna biashara nyingi ambazo hazitambuliwi n.a. mfumo wa kodi,watu wanalipa pesa bila shida Madini, Nafaka, Udarali na wale Benki babu wanaokopesha pesa kwa riba nk.
Mimi naomba Serikali ikubali pendekezo hili la kutoza kwenye mafuta. Watapata pesa nyingi bila usumbufu.
 
Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta
Hata sh 20/- tu hilo daladala tayari ilishadouble hyo 2.5K ya sasa mkuu.
Hawa jamaa ukiwapa mfano wa 50 wao watakurupuka kwa kuweka sh 100 kwa sababu ya uvivu wa kufikiri.
 
kwa msingi huo road licence lazima iendelee kuwapo na huu ni mfumo wa dunia nzima.
Haikusemwa road licence ifutwe bali iingizwe kwenye mafuta.

Wanaosema mafuta yanatumika viwandani na majumbani: je ile iliyokuwa 'roditol' ilipoingizwa kwenye mafuta badala ya kulipia kwenye vibanda barabarani; je mafuta yaliacha kutumika viwandani?
 
Hawa jamaa hawashauliki pesa wangepiga sana shida wasomi wa kwetu hapa hawana msaada.
 
Ni wazo zuri sana, lakini kwa watu wa majenereta, mashine za kusukumia maji watakua wanaonewa
 
Wanatupiga mara mbili. Roadtoll ipo palepale na roadlicence ipo palelppale. Kaulize mchanganuo wa bei ya lita ya mafuta ya gari utakutana na road toll. Wizi
 
Hatuna utaratibu mzuri.wa kusikiliza mawazo mazuri ya wananchi.na kuyafanyia kazi.viongozi wengi na watawala Africa.ni miungu watu.tatizo.tutafika siku moja.umoja ni nguvu
 
Wananchi wengi wameanza kuelewa, lakini na walio bado gizani kujua nani analipa kodi bado ni wengi zaidi. Pote duniani mlipa kodi ni mlaji wa mwisho. Kupandisha bei ya petrol kufidia road licence utapata urahisi wa kukusanya kodi, lakini utavilipisha vyombo vingine vinavyotumia mafuta lakini havijui barabara, kama vile generator na boat za uvuvi na meli.

Mnapoleta hoja kama hizi nashindwa kuelewa nini maana yake. Hamkumbuki mafuta ya taa yalipandishwa kuliko diesel?? Hao wanavijiji ambao ndio watumiaji wakuu wa mafuta ya taa mbona waliridhia?? Kama ni nini, wawekewe utaratibu wa kupata vibali maalum vya kurudishiwa hiyo tozo. Naunga mkono hiyo kodi iwekwe kwenye mafuta waache unyanyasaji huu wanao ufanya
 
Wazo zuri mkuu....hawa wanang'ang'ania utaratibu wa kizamani.... ulicho shauri ni kama Tanesco wanavo pata pesa kwa Luku badala ya kug'ang'ana na mita za kizamani....
 
Mwaka 1997 wakati Jakaya anaianzisha Mamlaka ya mapato nadhani alikuwa na nia njema sana katika kukuza pato la taifa kupitia ukusanyaji wa kodi. Nina iman kubwa kabisa hata yeye alikuwa akisikitishwa na hawa jamaa kutegemea ulipwaji mkubwa wa kodi kutoka kwenye Sigara na Pombe. Mleta mada upo sawa kabisa pengine ningeenda mbali zaidi upande huo kwamba,
Sisi tunaojiajiri kungekuwa na mazingira rafiki ya hawa wakadiriaji kodi na wafanyabiashara wadogo sidhani kama kuna mtu angekwepa. Mtu umeanzisha biashara ndogo tu ila unataka itambulike kiutaratibu, pale kwa mkadiriaji anakukadiria kimazoea badala ya wao kutoka ofisini na kwenda eneo la biashara wakaangalie mazingira yalivyo ili ukadiriwe vizuri wao wanakukadiria watakavyo wao.
 
Napenda kukupongeza mtoa hoja hii kweli itawasaidia hata TRA garama za kuzitafuta gari ambazo hazijalipia, na pia usumbufu kwa wenye magari.Wananchi wengi wamekuwa pia wanauza magari bila badili miliki na mnunuzi anakuwa halipii matokeo deni linabaki kwa muuzaji.Hii niliwahi msikia jamaa yangu yalimkuta na nikamuambia mbona hakufanya kubadilisha jina kuepuka tatizo hilo.Pendekezo lako kama likimfikia Waziri wa fedha au kamati ya bajeti itasaidia maana kama hutumii gsri au bovu unakuwa huna deni kama vile LUKU
 
Akili za kijinga unafikiri ni sawa nauli zipande?
Mwenye bus Hana hasara watakao umia no maskini ujue hata mafuta ya taa yatapanda
 
Road licence ni jina tu lakini ni Adhabu ya kumiliki Gari
Kwa kuwa hutozwa kwa kila anayemiliki gari hata ikiwa mbovu. Na njia pekee ya kuikwepa ni kuifuta gari yako kwenye mtandao wa TRA
Maana ingekuwa ni kodi kama jina linavyoitwa ingekuwa gari mbovu inatolewa taarifa na kusitisha utozaji lakini sivyo kabisa
Kweli ni adhabu tena kubwa mnoo
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!
shilingi 50 kwa kila lita bado ni nyingi sana inaraliwe iwe kati ya 10 mpaka 30.
 
Nmekaa nkafkiria kwamba...hivi kama ungeenda pale magogoni na kumpa huu ushauri JPM, nna uhakika angekupa CHEO maana kuna wana uchumi wengi tu wameshindwa kuliona hili
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.

Mkuu:
Lakini Railway levy inatozwa hata kwa wasio husika.
 
Mkuu:
Lakini Railway levy inatozwa hata kwa wasio husika.
Railway Levy msingi wake ni kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga mtandao wa Reli. Baada ya kuona kuwa nchi (nadhani pia na nchi nyingine za Afrika Mashariki) zinakosa uwezo wa kibajeti wa kujenga Reli mpya kwa kiwango cha standard gauge, ikaonekana kuwa tukiamua kama nchi kutoza Kodi kwa bidhaa zote zinazoingizwa kutoka nje kwa ajili ya jambo hili tunaweza kufikia lengo. Bahati mbaya nayoiona ni kwamba huenda kod hii haina specific account na hivyo mapato yake kujumuishwa katika mapato ya jumla.

Nilitaraji kusikia waziri wa fedha akitoa updates za mara kwa mara Bungeni juu ya Railway Levy kwa maana ya kiwango kilichokusanywa, changamoto au mafanikio ya ukusanyaji wake ili kubaini kama italeta matokeo yaliyokusidiwa au hapana. Na hii ingeweza kuleta projections. Kwa msingi huo, Railway levy yapaswa kuwa temporary levy ambayo inatakiwa ife tu ikiwa urefu wa kilomita zilizokusudiwa kujengwa na kodi hiyo zimekamilika, nikitumai kwamba Reli ikiwepo, uendelezaji na upanuaji wa line nyingine za reli zinapaswa kufadhiliwa na mapato yatoknyo na Reli hiyo. Tatizo kubwa la mfumo wetu wa kodi ni kutokuwa specific na pia kutofanya evalution ya kutosha kuzibaini kodi zinazohitaji reforms. Bahati mbaya wataalam wetu ni "robots" katika kila kitu.
 
Back
Top Bottom