DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 8,598
- 17,735
Amani iwe nanyi
Angalizo: Kabla ya yote Enyi ndugu zangu napenda kutoa angalizo kwamba Yatakayoongelewa hapa ni kwa lengo la kujifunza na si katika muktadha wa maana yoyote nyingine..
Kama mada inavyojieleza Kuhusu Mafundisho ya hao watakatifu wawili..
watakatifu hao wamekuwa sio tu na mfanano wa Mafundisho hata mfanano wa maisha yao pia...
MFANANO WA BAADHI YA HAIBA..
Yesu anakadiriwa kuzaliwa mwaka 6 B.C.E ,japo kuna baadhi ya Nyaraka zinasema ni 7 BCE
na Krishna anakadiriwa kuzaliwa mwaka 400 B.C.E Japo kuna baadhi ya nyaraka zinasema ni mapema sana kabla ya hapo kama 1000 BCE kutokana na maandiko mengi kuandikwa kipindi cha vita ya kurukshetra ambayo wanahistoria wanakadiria ilikuwa kati ya mwaka 1000 BCE Na 400 BCE
kwa hiyo krishna alikuwepo duniani miaka 400 kabla ya kuwepo kwa Yesu...Au 1000 Kabla ya Yesu
MAFUNDISHO YAO..
YESU
Yesu alifundisha katika Yerusalem, Mji wa yuda Galilaya na Israel kwa ujumla, Mafundisho ya Yesu yanapatikana katika Biblia ,Quran na kitabu cha mormons..
Japo kitabu bora cha kupata Mafundisho yenye wingi wa Maelezo ni Biblia hasa agano Jipya..
Mafundisho mengi yamejikita kwenye Dialogue na maelezo aliyokuwa akiwaambia wanafunzi wake na baadhi ni yale aliyomfundisha Paulo kuyasema (Kwa mujibu wa paulo mwenyewe kupitia nyaraka)
KRISHNA
mafundisho ya krishna yanapatikana katika vitabu vitakatifu vya Hinduism kama Bhagavata Purana ,Garga Samhita ,Harivamsa,Vishnu Purana,Mahabharata (ambapo ndani kuna Bhagavad Gita), Brahma Vaivarta Purana..
katika vitabu vyote hivyo kitabu changu pendwa na nitakachokitumia ni Bhagavad Gita kwa sababu kimeeleza zaidi maneno mengi na kina mafundisho mengi sana.
Huenda kuliko hata vitabu vingine na kinatumika almost na wahindi wa madhehebu yote...
Mafundisho mengi ni aliyokuwa akiongea au kumwambia mwanafunzi wake mpendwa Arjun katika vita ya kurukshetra
INAENDELEA SOMA HAPA...MFANANO WA MAFUNDISHO YA YESU NA MAFUNDISHO YA KRISHNA UNAKUPA PICHA GANi 2

- kuzaliwa kwao wote walitabiriwa
- Wote walizaliwa kwenye mazingira mabaya Yesu alizaliwa Kwenye hori la ng'ombe na Krishna alizaliwa Gerezani..
- wote walizaliwa na baba fundi seremala..
- wote walizaliwa na mama Bikra..
- wote waliishi maisha matakatifu wakifundisha..
- wote walijinasibu ama kunasibiwa kuwa wana wa Mungu..
- wote walisema kuwa wao si wa ulimwengu huu na walikuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu...
- wote walihubiri upendo
- Sote walitabiriwa kwa kuonekana kwa nyota ya mashariki
- krishana alijitambulisha kama cowherd (Mchungaji wa ngombe), na yesu alijitambulisha kama Shephard (Mchungaji wa mifugo)
- wote kipindi wanazaliwa watoto katika mji wote waliuawa na kiongozi au watu waliohofia kuzaliwa kwao