Mfalme wa Uholanzi aomba radhi kwa biashara ya utumwa

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander ameomba msamaha wa kihistoria kwa Uholanzi kuhusika katika utumwa na ukoloni akisema ameathirika yeye binafsi tena kwa kiasi kikubwa kwakuwa Familia ya kifalme haikufanya chochoe kuzuia utumwa.

Maelfu ya vizazi vya Watumwa kutoka Taifa la Amerika Kusini la Suriname na Visiwa vya Karibea vya Aruba, Bonaire na Curacao walihudhuria sherehe hiyo Amsterdam jana Jumamosi ambapo ilifanyika kwa lengo la kuvunja minyororo katika Surinamese na kuadhimisha miaka 150 tangu desturi hiyo kusitishwa.

“Leo nimesimama hapa mbele yenu kama Mfalme wenu na kama sehemu ya Serikali, leo naomba msamaha binafsi, ninayasema haya kwa moyo na roho yangu”

Itakumbukwa Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte tayari aliomba msamaha rasmi mwezi Desemba kwa niaba ya Serikali kuhusu utumwa, tangu vuguvugu la Black Lives Matter lilipoibuka nchini Marekani, Uholanzi imeanzisha mjadala mgumu mara kwa mara kuhusu ukoloni na biashara ya Watumwa ambayo iliigeuza kuwa moja ya Nchi tajiri zaidi duniani.

Waholanzi walifadhili "Enzi ya Dhahabu" yao ya himaya na utamaduni katika karne ya 16 na 17 kwa kusafirisha karibu Waafrika 600,000 kama sehemu ya biashara ya Watumwa, wengi wao wakiwa Amerika Kusini na Karibea.
images%20(6).jpg
 
Lini waarabu nao wataomba radhi kwa kuwauza binadamu wenzao kama bidhaa? Ni wazungu tu wamekuwa wakiomba radhi, ikumbukwe wao ndio walikomesha ushenzi huo kwa mikataba moresby treaty
 
Siyo warabu tu hata machifu wa kiafrika. Machifu walikuwa wanufaika pia wa biashara hii ya utumwa. Kuna huyo Mbano Songea yeye alidriki hadi kupigana na wajerumani akilazimisha biashara ya utumwa iendelee. Machifu wote wakiongozwa na chifu mkuu wao wa sasa, waombe radhi na wafute mentality zao za kitumwa kuwa watu wetu hawawezi kujisimamia.
 
😆😂🤣 Chief wa sasa! Na sijui kwanini walimsimika Uchifu? Itakuwa walijua ni Mangungo wa kizazi kipya.
 
Lini waarabu nao wataomba radhi kwa kuwauza binadamu wenzao kama bidhaa? Ni wazungu tu wamekuwa wakiomba radhi, ikumbukwe wao ndio walikomesha ushenzi huo kwa mikataba moresby treaty
Katika watu wanaotamani utumwa uanze hata kesho ni mwarabu. Mwarabu akikusaidia sana, atakujengea msikiti na kukuchimbia kisima cha kujitawazia.
 
Warabu wanachokifanya sasa kwa mabinti wa kazi kutoka afrika haina tofauti na biashara ya utumwa. Kwa hiyo hadi sasa biashara ya utumwa inaendelea uarabuni.
 
Back
Top Bottom