Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,913
Mfalme wa Udachi (Netherlands) ameomba radhi kutokana na nchi hiyo kupata faida kubwa iliyotokana na biashara ya kuuza watu mnamo karne ya 17.
Katika hotuba yake kwa taifa kuadhimisha miaka 160 tangu kupigwa marufuku kwa biashara hiyo, mfalme Willem-Alexander akiambatana na mkewe bi Maxima amesema nchi yake ilisafirisha na kuuza watu duniani kote kabla ya marufuku hiyo
Katika mapitio ya kumbukumbu za biashara hiyo imejulikana kuwa Udachi ilipata jumla ya dola milioni 595 baina ya mwaka 1675 na 1770 kwa kusafirisha waumwa wasiopungua 600,000.
Maelfu ya waafrika walinunuliwa na kusafirishwa kwenda makoloni ya Udachi yaliyokuwa visiwa vya Carribean na Amerika ya kusini, hata hivyo hiyo ilikuwa ni asilimia 5 ya biashara yote ya utumwa..Sehemu kubwa ilikuwa ni biashara ya Uiengereza na Marekani ambapo meli iliyokuwa ikibeba watumwa ya ufalme wa Uiengereza iliyoitwa Jesus ilipewa nishani kwa kuleta faida kubwa iliyotokana na biashara hiyo ya utumwa duniani.
Waiengereza walinunua watumwa wengi kutoka Afrika ya magharibi huku wachache wakiwatoa kutoka Afrika Mashariki.
Biashara ya utumwa Afrika mashariki ilifanyika katika muda wa karibu na kupigwa marufuku kwa biashara hiyo mwaka 1863 wakati wa utawala wa ufalme wa Zanzibar ulioanza mwaka 1832.
.Waiengereza waliamua kusitisha biashara hiyo baada ya uvumbuzi mkubwa wa mitambo iliyofanya kazi zilizofanywa na watumwa kwenye makoloni yao na kupelekea kusafirisha watumwa na kuwatunza kuwa ni ghali zaidi