Mfahamu Reinhard Bonnke: Mhubiri aliyetikisa dunia

Heri lee

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
981
528
Habari wana ndugu mnaendeleaje na vyuma kukaza

Moja kwa kwa moja kwenye pointi leo naomba tukumbashane kidogo mtu aliwahi kuvuma sana hapa duniani Enzi za miaka ya 1970 - 2003 miaka hiyo, Mtumishi kutoka Ujerumani bwana REINHARD BONKE.

Aliwazaliwa mwaka 1940-4-19. Alimpokea YESU akiwa na miaka 9 kwenye mkutano uliofanywa na huko MUNICH mwaka 1949 akiwa ndie mtoto pekee aliyenyoosha mkono anaitaji kuokoka. Baada ya kuokoka alikuwa na kipaji cha kipekee cha kuchambua vitabu vya dini hadi wazazi wake walitamani akasomee ukasisi aje kuwa papa lakini haikuwezekana.

Akiwa na miaka 17 aliandika kitabu cha “Time is running”. Alijunga na masomo ya bible school huko Swansea.

Bonke alioa mwaka 1964 akapata wototo 3 na wajukuu 8

Mwaka 1974 Bonke alianza huduma yake akiwa na watu 100 hivi alianzisha ya chama CHRIST FOR ALL NATION “CfaN” 1986

Bonke alizunguka zaidi ya nchi zote Africa ikiwemo Tanzania mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro

Nigeria
SOUTH AFRICA
UGANDA
KENYA
UGANDA
DRC
NIGER
ZAMBIA
MALAWI

Na nchi nyingi hapa na Duniani huku akishika nafasi ya juu kuliko wote kukusanya watu katika mikutano yake ambayo wahudhuriaji wa mikutano yake hawakuwa chini ya Laki 400,000.

Kwa sasa Bonke ana miaka 79; umri umeenda sana hafanyi tena huduma ya dunia nzima anatoa huduma ndogo ndogo huko vitongoji vya nchi za Ujerumani na Uingereza.

Anajulikana kama ''GREAT AFRICAN MISSIONARY'' Ameacha jina kubwa sana dunia tangu miaka ya ya 1990 hadi leo hakuibuka mtu wakujaza nafasi ya katika mikutano yake Africa na dunia kwa ujumla.

Kwa ufupi tumekumbushana tuu juu ya BWANA REIHHARD BONKE

''NASHUKURU''


boke.jpg
 
Nakumbuka nilihudhuria mkutano wake Kilimanjaro basi uwanja wa mashujaa pale palifungwa spika kuubwa ndeefu
 
Back
Top Bottom