Mfahamu Pete Felix O'neal

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
Pete Felix O'neal

Alizaliwa tarehe 27-07-1940 huko Kansas City siku kama ya leo, anayotimiza miaka 83. Ni mwanamapinduzi mwenye asili ya kimarekani akiwa menyekiti wa Black Panther Party- for self defence . Chama cha wapigania na kulinda haki za watu weusi wa kimarekani kama majimbo yao zidi ya sheria kandamizi na za kibaguzi za Jim Crow.

Pete akiwa menyekiti mkuu wa Kansas City Chapter, wakakumbwa na kadhia ya mpango mkakati na madhubuti uitwao COINTELPRO ( Counter Intelligence Program ) ulioanzishwa na mkurugenzi wa kwanza wa FBI , bwana Edgar J. Hoover . Mkakati wa kuzima na kudhoofisha vuguvugu na harakati za " civil rights movements "zilizochagizwa na wanamapinduzi mbalimbali wa miaka hiyo ya 1960s vinara wao wakiwa Dr. Martin Luther King & Malcolm X.

Kadhia zilizoambatana na hila chonganishi, mashambulio ya kushtukiza, mauaji, vifungo vya maisha jela kwa wahusika wakuu wa harakati hizo, Black Panther Party kikiwa chama kinacholengwa zaidi na mpango huo wa FBI.

Pete na mkewe Charlotte Hill O'neal akiwa binti asiyezidi miaka 20, ikawaladhimu waikimbie nchi yao kusalimisha maisha yao zidi ya njama hizo.

Wakafikia Algeria, kisha Tanzania miaka 1970 kutokana na sera wezeshi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwakaribisha wapigania Uhuru kutoka popote duniani kuja Tanzania , kusaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika kupata Uhuru wao.

Akapata political asylum, na kuishi kizuizini hapa Tanzania kwa muda wote toka mwaka 1972,akiwa hana nia wala dhamira ya kurudi tena Marekani baada ya kuishi umeruni kijiji cha Imbaseni na kuwa moja ya kabila la Wameru. Kwa msaada wa bega kwa bega na mkewe mama C wamefanikiwa kuanzisha shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama " United African Alliance Community Center " wamewezesha jamii ya kimeru na majirani kupata kunufaika na shirika hilo toka miaka ya 90 kwa kozi mbalimbali za vijana na elimu bure toka shirikani kuanzia madarasa ya kujifunza lugha , kompyuta, uigizaji, utengenezaji muziki, ufundi uashi, ujenzi nk, kwa zaidi ya mihongo mitatu .

Kupitia program yake ya kuwasili kimalezi, kuwalea watoto wenye uhitaji kimalezi na kielimu . Pete O'neal amefanikiwa, kuwalea watoto thelathini na tatu kuanzia wakiwa na miaka chini ya saba, mpaka kufikia ngazi ya kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu mwaka huu 2023. Wengi wao sasa wanaingia mwaka wa pili mavyuoni, wamepata kulelewa nae wakiwa nursery schools.

Mchango wao kwa jamii umewezesha mahusiano bora ya kiutamaduni baina ya waafrika wenye asili ya kimarekani na watanzania kuwa rafiki sababu ya kuwa daraja baina yao.

Jamii ya kijiji cha Imbaseni ni mnufaika wa mradi wa maji ya bure kwa miaka zaidi ya ishirini kupitia mradi wa Kuji Foundation ,taasisi iliyoanzishwa na rafiki yake wa karibu. Mwanaharakati mwenzie aliyekua mhanga wa mpango mkakati wa FBI wa COINTELPRO, ndugu Geronimo Elmer Pratt au kwa jina lake sahihi Geronimo Jijaga kiongozi aliyekuwa na ngazi juu ktk chama cha Black Panther, akiwa maarufu kama baba mlezi wa mwanamuziki maarufu wa hiphop Tupac Shakur . Kupitia documentary yake ya A panther in Africa - Pete na Geronimo walionekana pamoja wakifurahia harakati zao kusaidia jamiii nufaika ya kimeru mara baada ya kutenganishwa na matokeo hasi ya COINTELPRO kwa Black Panther Party miaka ya sabini.

Tunasherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa na shujaa huyu wa Kimeru leo tukimuombea heri na fanaka . United African Alliance Community Center imekuwa moja ya taasisi kubwa inayoleta wanafunzi wengi kutoka majimbo mbalimbali Marekani na nchi nyingine kufanya study tours ,na baadhi ya international schools za Kenya & Tanzania kuhusu kujifunza black history studies .

Heri ya sikukuu yako ya kuzaliwa Mzee Pete Felix O'neal a.k.a Babu

Toka Arusha Poetry Club

P . O'neal.jpeg
Pete O'neal.jpeg
Pete Felix O'neal.jpeg
 
Pete Felix O'neal
Alizaliwa tarehe 27-07-1940 huko Kansas City siku kama ya leo, anayotimiza miaka 83. Ni mwanamapinduzi mwenye asili ya kimarekani akiwa menyekiti wa Black Panther Party- for self defence . Chama cha wapigania na kulinda haki za watu weusi wa kimarekani kama majimbo yao zidi ya sheria kandamizi na za kibaguzi za Jim Crow.
Pete akiwa menyekiti mkuu wa Kansas City Chapter, wakakumbwa na kadhia ya mpango mkakati na madhubuti uitwao COINTELPRO ( Counter Intelligence Program ) ulioanzishwa na mkurugenzi wa kwanza wa FBI , bwana Edgar J. Hoover . Mkakati wa kuzima na kudhoofisha vuguvugu na harakati za " civil rights movements "zilizochagizwa na wanamapinduzi mbalimbali wa miaka hiyo ya 1960s vinara wao wakiwa Dr. Martin Luther King & Malcolm X.
Kadhia zilizoambatana na hila chonganishi, mashambulio ya kushtukiza, mauaji, vifungo vya maisha jela kwa wahusika wakuu wa harakati hizo, Black Panther Party kikiwa chama kinacholengwa zaidi na mpango huo wa FBI
Pete na mkewe Charlotte Hill O'neal akiwa binti asiyezidi miaka 20, ikawaladhimu waikimbie nchi yao kusalimisha maisha yao zidi ya njama hizo.

Wakafikia Algeria, kisha Tanzania miaka 1970 kutokana na sera wezeshi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwakaribisha wapigania Uhuru kutoka popote duniani kuja Tanzania , kusaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika kupata Uhuru wao.
Akapata political asylum, na kuishi kizuizini hapa Tanzania kwa muda wote toka mwaka 1972,akiwa hana nia wala dhamira ya kurudi tena Marekani baada ya kuishi umeruni kijiji cha Imbaseni na kuwa moja ya kabila la Wameru. Kwa msaada wa bega kwa bega na mkewe mama C wamefanikiwa kuanzisha shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama " United African Alliance Community Center " wamewezesha jamii ya kimeru na majirani kupata kunufaika na shirika hilo toka miaka ya 90 kwa kozi mbalimbali za vijana na elimu bure toka shirikani kuanzia madarasa ya kujifunza lugha , kompyuta, uigizaji, utengenezaji muziki, ufundi uashi, ujenzi nk, kwa zaidi ya mihongo mitatu .

Kupitia program yake ya kuwasili kimalezi, kuwalea watoto wenye uhitaji kimalezi na kielimu . Pete O'neal amefanikiwa, kuwalea watoto thelathini na tatu kuanzia wakiwa na miaka chini ya saba, mpaka kufikia ngazi ya kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu mwaka huu 2023. Wengi wao sasa wanaingia mwaka wa pili mavyuoni, wamepata kulelewa nae wakiwa nursery schools.

Mchango wao kwa jamii umewezesha mahusiano bora ya kiutamaduni baina ya waafrika wenye asili ya kimarekani na watanzania kuwa rafiki sababu ya kuwa daraja baina yao.

Jamii ya kijiji cha Imbaseni ni mnufaika wa mradi wa maji ya bure kwa miaka zaidi ya ishirini kupitia mradi wa Kuji Foundation ,taasisi iliyoanzishwa na rafiki yake wa karibu. Mwanaharakati mwenzie aliyekua mhanga wa mpango mkakati wa FBI wa COINTELPRO, ndugu Geronimo Elmer Pratt au kwa jina lake sahihi Geronimo Jijaga kiongozi aliyekuwa na ngazi juu ktk chama cha Black Panther, akiwa maarufu kama baba mlezi wa mwanamuziki maarufu wa hiphop Tupac Shakur . Kupitia documentary yake ya A panther in Africa - Pete na Geronimo walionekana pamoja wakifurahia harakati zao kusaidia jamiii nufaika ya kimeru mara baada ya kutenganishwa na matokeo hasi ya COINTELPRO kwa Black Panther Party miaka ya sabini.

Tunasherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa na shujaa huyu wa Kimeru leo tukimuombea heri na fanaka . United African Alliance Community Center imekuwa moja ya taasisi kubwa inayoleta wanafunzi wengi kutoka majimbo mbalimbali Marekani na nchi nyingine kufanya study tours ,na baadhi ya international schools za Kenya & Tanzania kuhusu kujifunza black history studies .
Heri ya sikukuu yako ya kuzaliwa Mzee Pete Felix O'neal a.k.a Babu

Toka Arusha Poetry Club

View attachment 2707133View attachment 2707132View attachment 2707131
Hongera nyingi kwao...👏👏
 
Back
Top Bottom