Jinsi ya kuwa "mtumishi wa Mungu"

KatetiMQ

Senior Member
Sep 25, 2022
180
311
Hizi hapa njia za kuwa mtumishi wa mungu na kuukwaa utajiri

1. Jifunze kusema uwongo

2. Jifunze jinsi ya kuchezea akili za watu

3. Jifunze kuvaa suti au gauni jeupe

4. Craim biblia yote juu ya kichwa chako.

6. Tafta kamganga gwiji kakusaidie kufanya mazingaombwe kidogo.

7. Pata ukumbi mzuri usiweke fan wala AC (joto ufanya akili ya mtu isifanye kazi vyema)

8. Jifunze jinsi ya kuwapa maskini matumaini bandia

9. Pata sanduku kubwa la sadaka (muhimu sana)

10. Kuandaa mkesha wa usiku kila siku ili kuwachanganya(ukosefu wa usingizi ufanya mtu ashindwe kutumia akili)

11. Jifunze jinsi ya kuzungumza katika lugha zisizojulikana.

12. Jifunze ni nani wa kumfanya uponyaji na muujiza, (kuwa na watu maalumu)

BAADA YA HAPO ENJOY LIFE NA SAFARI MPYA YA MAFANIKIO YAKO ITAANZIA HAPO.
 
Pesa ikichanganya weka ma bus ya bure kuleta waumini kwenye ibada, na hii isiwe ya kudumu ila italeta motisha.

InShot_20240213_142429052.jpg
 
namuangalia mtu anaitwa Kuhani Musa, kila mdada anayeongea naye anamwambia ni mchawi na ni mtu wa pili toka kwa Lucifer, sasa sielewi huku kuwa wa pili kutoka kwa lucifer ni inawezekana vipi wadada kama watatu nilioona wanakuwa wote ni wa pili baada ya huyo lucifer
 
Andaaa semina mbali mbali plus maombi ndani yake mfano

Usiku wa kukomboa kizazi chako kilichoshikwa katika ulimwengu wa roho

Mkesha wa kukata minyororo na nira zilizofunga mafanikio yako
 
Andaaa semina mbali mbali plus maombi ndani yake mfano

Usiku wa kukomboa kizazi chako kilichoshikwa katika ulimwengu wa roho

Mkesha wa kukata minyororo na nira zilizofunga mafanikio yako
Tuchangamkie ajira hiyo vijana😂😂😂
 
Rabbon njoo
Kuna mtu hana imani na watumishi huku
Usihangaikie naye huyo,

Hao ni mbwa mwitu wanaojivika ngozi ya Kondoo Ili wadanganye watu,

Wanaofanya hivyo, Ni Waganga ambao wameacha kuvaa kaniki, wanavaa sauti na tai Ili kudanganya watu.

Kama ambavyo Pana manabii na watumishi wa uongo, wapo watumishi wa Mungu wa Kweli.

Watumishi wa Mungu wa Kweli hawana tamaa ya Fedha, hawajawahi kutumia sadaka Kwa mambo Yao binafsi zaidi ya kutumia kwenye INJILI, kuhudumia wajane na yatima kupitia sadaka hizo.

Njia ya Mbinguni ni nyembamba, tuwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli wapo kabisa, wasiouza miujiza, Wanapoza wagonjwa Bure. Wana Upendo, ni raia wa Mbinguni,wamepigwa CHAPA/MUHURI ya Mungu katika paji za nyuso zao.

Ubarikiwe.🙏
 
Hakuna mtumishi wa Mungu anayesema uongo, au kuchezea akili za watu na kufanya uhuni huo uliouandika, Usitumie jina la MUNGU hovyo! Jifunze kutofautisha mtumishi na Tapeli.
Admin1988 @activhuu uzi uondolewe au urekebishwe.

Alafu sio Craim ni cram
 
Back
Top Bottom