Mfahamu malkia wa kuzimu

Naombeni tofauti kati ya
Shetani,
Ibilisi,
Jini,
Mchawi,
Mwanga,

Na


Malaika.
 
Ha ha ha! Shetani awe na ubavu wa kuzuia mawasiliano na Mungu? Labda si mungu tunayemjua, ukweli ni kwamba shetani hana uwezo wa kuingilia mawasiliano na Mungu, maana Mungu anajua hata nia yako tu ya kumwomba na nini utakachoomba hata kabla! Shetani huteseka na kuumia mno na kamwe hawezi kuhimili hata jina la Mungu linapotajwa kwa ibada!
Nakubaliana nawe kwamba ana uwezo na anasa na mali za duniani lakini hili la kukatiza katikati ya Mungu na Binadamu kamwe haliwezi tokea. Anachoweza fanya ni kujaribu kuyahamishia mawazo yako mahala pengine (Distraction) na kukuhimiza ujishughulishe na masuala yasiyo na tija kwa roho yako lakini hufyata mkia utapolitaja (invoke) jina la Yesu maana jina hilo linapotajwa kwa ibada kuzimu hutetemeka na Luciferi na Majeshi yake hutawanyika!
Chezea na kingine lakini si jina la Mungu!
Kwa mtego wa mali na utajiri Luciferi amejitwalia wafuasi wengi kabisa. Utitiri wa dini na madhehebu yanayohubiri na kuahidi utajiri na ukwasi ni miongoni mwa makuwadi wa Luciferi, maana hata Yesu alisema itakuwa rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la shindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa mbingu; wewe unayehangaika dhehebu baada ya dhehebu kuusaka ukwasi unautarajia ukupeleke pepo ipi, ya mbinguni au kule aliko mmiliki wa utajiri wa duniani hapa Luciferi?
 
Jamani mazee! Hakuna kiumbe ama roho yoyote inayoweza kuzuia maombi ya mtu kumfikia Mungu. Pia hakuna kiumbe ama roho inayoweza kuzuia msjibu ya mtu kutoka kwa Mungu.
Kitu kinachoweza kuzuia maombi ya mtu ni mtu mwenyewe, pale anapo kiuka kanuni ama taratibu kila kitu kina sheria.
Kwa habari ya Daniel maombi yake kuzuiwa , note Daniel alikua agano la kale na shetani halikua haja pokwa mamlaka yake, but sasa shetani hana mamlaka tena kama wewe ni mtu wa sheria uzima, nyie ombeni popote pale hata ukiwa chooni ama bafuni we omba tu kwa imani na Mungu atakusikia na atakujibu kama umetimiza vigezo na masharti.

Njia nzuri ya kupokea majibu ya maombi ni kuacha dhambi na kuishi msisha ya upendo maana hiyo ndio kanuni. Maombi ya mtu mwenye haki yafaa sana
 
Inawekana anadanganya lkn hadi ujue kuwa anadanganya Manake unaujua ukweli so kwakuwa hapa nikama Darasa kama MTU amedanganya ikiwa unaujua ukweli unaweka watu tunapima.....Wanasema hoja inapingwa kwa Hoja

Mzee! Hii mada cha kwanza inahitaji ushahidi zaidi wa Biblia Takatifu, na sio maelezo matupu. na ukiangalia hili ni jukwaa sio mahala pake, kuna jukwaa na hayo mambo nafikiri ni la dini kama sijakosea ndio ingeenda huko ili ijadiliwe kwa mapana yake kwa msingi wa kiimani zaidi na sio porojo
 

Ndo maana nilitoa angalizo mapema Sana.
kuwa nyie ni wajuaji na hamjui kitu.
Kama ishu ni agano jipya kwanini Yesu alifunga siku 40? alikuwa anataka nguvu gani ya ziada Kama kuna tofauti ya zamani na sasa?
Ujuaji mwingi mbele giza.
Mmekuwa mkidanganya waumini wenu na kuwapotezea muda.
Hamfai kabisa, mmevunja ndoa nyingi za watu, hili nitalieleza Kwa kina Siku nyingine.
Na mnatoa unabii wa uongo, ole wenu Mathayo 22:7
 
Kama aiwahusu wapite kulee!
 
Haya mastori ya kufikirika haya.. cjui huwa mtu anapata wapi muda wa kuandika mambo kama haya...!
 
Kwenye ulimwengu wa Roho kuna....wa GIZA na NURU nivizuri kuzijua pande zote vzr Humu duniani huwezi kujua kila kitu unaweza kusema unaujua zaidi ulimwengu wa NURU unaweza ukakutana na MTU anajua mengi kuliko ww so maisha hayataki kukariri

Ni bora umemweleza ukweli mkuu, anajifanya kila kitu anajua, wakati mambo ya kiroho yana elimu pana Sana.
 
Asante Sana cipro, mid nmependa mafundisho yako name has a muda wa kuomba,
Uwe Unatoa mafunzo hya mazuri, waelewa tutaelewa na kunufaika, wabishi hawaishi
 
Hatukatazwi kujua, isipokua mleta mada anajuza watu kwa taarifa zisizo sahihi. Yaani namaanisha ni mwongo muanzisha mada

Wewe ndo unajiita mcha Mungu? unawezaje kunizulia kuwa mimi ni muongo?
Wewe ni mhuni Kama wahuni wengine wanaojifanya wanamjua Mungu kumbe hakuna kitu.
Unaniita muongo nimemtapeli Nani kupitia mada yangu?
Kama huamini pita kimya, wanaoamini wanajua ni nini nimeandika.
 

Mie sio muhuni, wewe ni mpotoshaji wa ukweli. Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa. So, najitahidi kwa neema yake kumcha sana ili maarifa yangu ya kumjua Mungu yaongezeke
 

Yesu Kristo, aliongozwa na Roho kwenda nyikani ( akiwa kajazwa Roho Mtakatiku yaani ujazo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu), na ilikua ni sehemu ya yeye kuomba kwa nguvu na kupitishwa katika majaribu ili aweze kupokea nguvu ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya huduma ( yaani Roho Mtakatifu juu yake) na ndipo unapo ona Yesu Kristo anatoka nyikani akiwa na nguvu za Roho Mtakatifu ( Roho Mtakatifu juu yake ) na sio kujazwa Roho Mtakatifu ( sio kujawa na Roho Mtakatifu ), ukitaka kuelewa nenda kasome Luka Mtakatifu kuanzia sura ya tatu na ya nne.
 
Hakukuwa na Roho Mtakatifu na Yesu anasema utukufu wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo hivyo kwa sasa Tuna Neema zaidi ya akina Daniel ila kwa Imani ukijiona huna upako wa agano wa jipya utabaki hivyo hivyo
 
Hakukuwa na Roho Mtakatifu na Yesu anasema utukufu wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo hivyo kwa sasa Tuna Neema zaidi ya akina Daniel ila kwa Imani ukijiona huna upako wa agano wa jipya utabaki hivyo hivyo

Muambie huyo! anataka kuaminisha watu kua shetani na majeshi kua wana nguvu ya kuzuia maombi hajui kua shetani ni powerless kwa wale walio na Roho Mtakatifu...
 
Yote haya umeyajuaje ndugu.
Na ninakushauri uache kumchukulia Mungu kama binadamu.
 
Hizi Mada Huwa Ni Nzuri Sana, Lakn Kujua Haya Mambo Yahitaji Usiwe Vuguvugu Bali Moto Au Baridi.

Neno Jema Mtoa Mada.
 
Hawa Vijana Walosoma Hizi Siku Za Karibuni Huwa Wanaamini Sana Elimu Zao Kuliko Ukweli Halisi.

Mtoa Uzi Anayajua Haya Lakn Pia Si Vyema Kumuita Mtu Muongo Wakat Hujui Hata Historia Yake.
Ni Vyema Tukajirekebisha.
 
Lqkn Ni Vyema Ukaweka Hizo Tofauti Za Maandiko Ya Quran Dhidi Ya Haya Ya Bible Ilikuweka Mjadala Sawa, Nje Ya Hapo Hujui Kama Mtoa Uzi Anaijua Quran Kwa Kiasi Gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…