Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,262
- 18,251
Naombeni tofauti kati ya
Shetani,
Ibilisi,
Jini,
Mchawi,
Mwanga,
Na
Malaika.
Shetani,
Ibilisi,
Jini,
Mchawi,
Mwanga,
Na
Malaika.
Ha ha ha! Shetani awe na ubavu wa kuzuia mawasiliano na Mungu? Labda si mungu tunayemjua, ukweli ni kwamba shetani hana uwezo wa kuingilia mawasiliano na Mungu, maana Mungu anajua hata nia yako tu ya kumwomba na nini utakachoomba hata kabla! Shetani huteseka na kuumia mno na kamwe hawezi kuhimili hata jina la Mungu linapotajwa kwa ibada!Dunia inateswa na mambo mengi Sana ambayo wengi wetu huwa tunadhani yanatokana na akili zetu na mawazo yetu ama pengine ni uamuzi wetu binafsi.
La hasha, kila jambo linalotokea huwa limepangwa ktk ulimwengu wa roho tusioweza kuuona Kwa macho ya damu na nyama.
Kiongozi mkuu au mfalme wa maovu na shida zote duniani ni shetani ,kuzimu wanamwita Lucifer.
Huyu ni kiongozi mkubwa Sana ambaye makazi yake ni chini ya maji, bahari na maziwa. (kuzimu)
Lucifer huwa hafanyi kazi yoyote ngumu, yeye hupokea Taarifa na kutoa amri Kwa pepo mkuu Belzebur, ambaye naye huwaagiza mapepo wengine watatu ambao nao ni wakuu.
Kwa Sababu maalumu, nitamtaja pepo mmoja tu Kati ya hao watatu wengine na kazi zake hapa duniani.
Kwa kawaida, Lucifer ana serikali yake kuzimu yenye dola kamili, na waziri mkuu wake ni Belzebur.
Lucifer huwapa kazi za kufanya hawa hao mapepo, kila Siku.
Na wote hukaa angani, kila mmoja akikaa pande moja ya dunia ,yaani mashariki, kaskazini, magharibi na kusini, na kazi yao ni moja tu ni kuzuia Maombi ya watu Wa Mungu, Na wote wanakuwa chini ya Belzebur.
Huzuia Maombi, ndo maana unaweza kuomba Mungu miaka kibao bila majibu, Soma Daniel 10:13.
Malkia wao anaitwa Kilenzi, hili ni pepo hatari la kike ambalo ndo limeshikilia anasa na pesa zote za dunia hii.
Kilenzi linavunja ndoa za watu na kuharibu maisha ya vijana na mabinti.
Ni pepo haribifu la maisha ya watu, wote wanaotafuta Mali kishirikina, kilenzi ndo mgawaji wa hizo mali endapo tu utafuata masharti yao.
Kilenzi ndo waziri wa fedha na uchumi huko kuzimu.
Kati ya mapepo makuu yote, ni yeye tu ndo jike peke yake.
Mtu yoyote, akitaka chochote, iwe utajiri, Urais, Umaarufu, hata Kama hana elimu Lucifer humpatia kupitia kilenzi endapo tu, atatimiza masharti yao ambayo ni magumu mno.
Kila Siku saa 8 usiku ktk majira ya nchi zote duniani, mapepo hawa hushuka kutoka angani na kwenda kuzimu Kwa ajili ya kufanya sherehe na mikutano maalumu ya kuiangamiza dunia.
Inapotimia saa9:55 alfajiri, yanakuwa tayari yamemaliza kazi zao kuzimu na kurudi angani.
Watu wengi hawajui kuwa muda mzuri wa kuomba Mungu ni kuanzia saa 8:00 usiku hadi mwisho saa 9:55 alfajiri.
Maana kilenzi na wenzake wanakuwa kuzimu na hivyo kuliacha anga likiwa safi.
Kilenzi ndo pepo aliyeshikilia hadi serikali nyingi duniani. Soma ,Ufunuo wa Yohana. 17:1-8.
Jamani tukaeni jaribu na Mungu, Kwa leo naishia hapa, Siku nyingine nitafafanua zaidi.
Mmoja Wa mabinti aliye chini ya miliki ya kilenzi, Kama upo Kama huyu haha kwenye picha, basi wewe ni wa kilenzi, Nitafafanua zaidi.
Inawekana anadanganya lkn hadi ujue kuwa anadanganya Manake unaujua ukweli so kwakuwa hapa nikama Darasa kama MTU amedanganya ikiwa unaujua ukweli unaweka watu tunapima.....Wanasema hoja inapingwa kwa Hoja
Ni mambo mengi yanayo zuia pia mtu kutokupokea majibu ya maombi yake pindi aombapo na sio hayo mapepo, shetani na majeshi yake hao wote ni powerless katika new covenant. Hakuna kitu kinachoweza kuzuia maombi ya mtu kumfikia Mungu, na hakuna kinacho zuia mtu kupokea majibu ya maombi yake kutoka kwa Mungu katika hili agano jipya kama mtu huyo akifata kanuni za maombi na kuzishika
Kama aiwahusu wapite kulee!Mkuu chukua ujasiri wa mshana jr wakati anaweka mabandiko yake kuna watu walikuwa wakimpinga aidha aliendelea kukomaa Mwisho wa siku watu wamekuwa wakimuomba aweke Topic so kiongoz kama unania yakufundisha lete vitu Wengine sisi hatupitwi na jambo tunasoma kila kinachoandikwa tunachanganya na zetu so mkuu karibu uendelee ulipobakisha
Tuambie ukweli wako na sio kuukanusha uongo bila kutufafanulia ametoa mada anayoijua nawe tuambie unacho jua ili tujuzane tusiojua tujue tofautiHatukatazwi kujua, isipokua mleta mada anajuza watu kwa taarifa zisizo sahihi. Yaani namaanisha ni mwongo muanzisha mada
Kwenye ulimwengu wa Roho kuna....wa GIZA na NURU nivizuri kuzijua pande zote vzr Humu duniani huwezi kujua kila kitu unaweza kusema unaujua zaidi ulimwengu wa NURU unaweza ukakutana na MTU anajua mengi kuliko ww so maisha hayataki kukariri
Nami natakakujua zaidiNaombeni tofauti kati ya
Shetani,
Ibilisi,
Jini,
Mchawi,
Mwanga,
Na
Malaika.
Hatukatazwi kujua, isipokua mleta mada anajuza watu kwa taarifa zisizo sahihi. Yaani namaanisha ni mwongo muanzisha mada
Wewe ndo unajiita mcha Mungu? unawezaje kunizulia kuwa mimi ni muongo?
Wewe ni mhuni Kama wahuni wengine wanaojifanya wanamjua Mungu kumbe hakuna kitu.
Unaniita muongo nimemtapeli Nani kupitia mada yangu?
Kama huamini pita kimya, wanaoamini wanajua ni nini nimeandika.
Ndo maana nilitoa angalizo mapema Sana.
kuwa nyie ni wajuaji na hamjui kitu.
Kama ishu ni agano jipya kwanini Yesu alifunga siku 40? alikuwa anataka nguvu gani ya ziada Kama kuna tofauti ya zamani na sasa?
Ujuaji mwingi mbele giza.
Mmekuwa mkidanganya waumini wenu na kuwapotezea muda.
Hamfai kabisa, mmevunja ndoa nyingi za watu, hili nitalieleza Kwa kina Siku nyingine.
Na mnatoa unabii wa uongo, ole wenu Mathayo 22:7
Hakukuwa na Roho Mtakatifu na Yesu anasema utukufu wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo hivyo kwa sasa Tuna Neema zaidi ya akina Daniel ila kwa Imani ukijiona huna upako wa agano wa jipya utabaki hivyo hivyoEndelea kujidanganya na siku zinasonga mbele.
Na sijui Kama una usafi wa kumzidi Daniel mtu wa Mungu ambaye majibu ya Maombi yake yalizuiwa Kwa Siku 21,na mkuu wa uajemi (Belzebur). hadi Mungu akamtuma malaika wa Vita Mikael, akapigana na pepo Belzebur na kulishinda na ndipo Daniel akapata majibu yake.
Tatizo lenu ndugu zangu walokole mna ubishi wa ajabu Sana ambao mara nyingi hauwasaidii Daniel 10:13.
Hakukuwa na Roho Mtakatifu na Yesu anasema utukufu wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo hivyo kwa sasa Tuna Neema zaidi ya akina Daniel ila kwa Imani ukijiona huna upako wa agano wa jipya utabaki hivyo hivyo
Hawa Vijana Walosoma Hizi Siku Za Karibuni Huwa Wanaamini Sana Elimu Zao Kuliko Ukweli Halisi.Kama hujui mambo usiwe mbishi, ni vema ukaomba ufundishwe.
Sijakurupuka kuandika ujue, kuna mazito ninayoyajua siwezi kuyaweka hapa maana watu wengi ni wabishi halafu hawajui kitu.
Nimeona jinsi wanavyombishia mshana jr.
Usikimbilie kuniita muongo bila kufanya utafiti, ukiwa na akili hiyo, dunia itakupiga chenga Sana.
malaika na mapepo, wote ni roho, ila wana jinsia ktk ulimwengu wa roho.
Kwa mfano. malaika Mikael naye ni roho ila ni dume.
Hii strictly, kuna Mapepo jike na madume na yanaoana na kuzaana, wewe huwezi kuwaona Kwa macho, ni mambo ya kiroho.
Na Lucifer ni roho ila ni dume.
Usipende kuwa mbishi, penda kuwa mdadisi.
Lqkn Ni Vyema Ukaweka Hizo Tofauti Za Maandiko Ya Quran Dhidi Ya Haya Ya Bible Ilikuweka Mjadala Sawa, Nje Ya Hapo Hujui Kama Mtoa Uzi Anaijua Quran Kwa Kiasi Gani.Umeandika kutokana na kitabu chako kilivyokufunza ila Quran haikusema hivyo baadhi ya vitu ni tofauti sana kwa maana hiyo ingekuwa vizuri pia kusoma na upande wa pili ili kuweza kujibu baadhi ya hoja kwani ht nikiijenga hoja nitakuacha badala yke utajibu kutokana na mihemko nawasilisha