Mfahamu malkia wa kuzimu

Mfahamu malkia wa kuzimu

Malkia wa kuzimu ni Lilith ambaye ndo alikuwa mke wa kwanza wa adamu na ndo aliumbwa kama adamu.... hakuumbwa kutoka katka ubavu wa adamu.... hivyo nae alikuwa anataka mamlaka kama adamu....

Ndipo alipofukuzwa kutoka edeni na akaenda nyikani na kuanza kuzini na wale fallen angels na kuzaa nao .....
mh!! hii mbn sikuwahi kuiskia asee?!
 
mh!! hii mbn sikuwahi kuiskia asee?!
Lilith kwa mujibu wa mtandao wa kigirik na na kiebrania ni mke wa kwanza wa Adam aliye mbwa naye (Roth hashanah )
a9e28d674bbd7882ae91d36898294689.jpg
afe83d18a262b6ac681a5f3a72ade7f7.jpg

Nami ningependa kufahamu kuhusu hili
 
Ni hivi kipindi adamu ameumbwa na Mungu akamuona kuwa ni mpweke na inabidi amfanyie mtu wakufanana nae kuwa mke wake ni baada ya adamu kulalamika kuwa kipindi anapitishiwa wanyama ambao wapo paired alimuomba Mungu apate mwenzi wake....
Ndipo Mungu akamuumba Lilith kutoka mavumbini. Ila kulichomfanya Lilith kutokaa Edeni ni kuwa kipindi cha kufanya mapenzi alikuwa hataki kuwa chini ya adamu akidai kuwa ni submissive act, kuonekana ni mtumwa wakati wote ni sawa kwakuwa wote wametoka mavumbini na wako sawa...

Adamu alizidi kumlazimisha ndipo lilith akaamua kulitaka jina la Mungu na kupaa kutoka edeni na kuelekea katika bahari ya damu "Red Sea" ... Ndipo adamu akamwambia Mungu yaliyotokea na Mungu akawatuma malaika waende kum fetch Lilith huko red sea ili arudi bustanini.... Ila lilith alikataa....

Kuna mengi kuhusu lilith....ila ana sifa moja ya kuwafata wanaume katka ndoto na kuzini nao....
Yupo katika kila dini ila ana majina tofauti tofauti
Mkuu haujatuambia story yake inapatikana kwenye kitabu cha Mwanzo ngapi?
 
Nnaona Mshana nae katujibu kwenye mtandao wa kigiriki wanadai alikuwa mke wa Adam wa kwanza
iJamii vitu vingine ni rahisi sana hata mimi nilikuwa sijui kuhusu hili ona post yangu ya kwanza lakini sikusubiri niambiwe nikaingia Google nikakutana na hiki nilicholeta
Na ndio maana nikatumia maneno ya 'Kwa mujibu wa....'
 
Wadau kwa mujibu wa maandiko ya Biblia kimtindo yawezekana story ya Lilith ikawa na ukweli wake kimtindo. Nitaatach maandiko hapa ya biblia... Tujaribu kubrain storm wote hapa
[
fea8a0c784965412e95b7a8bf2130894.jpg

3fb763b840ae2ea1dbc2c99f984b06fe.jpg

Angalieni hapo kwenye genesis 1:27 na genesis 2:22
 
Sasa Tanzania ukiwa SAA nane usiku na marekani labda saa 12 jioni na UK labda SAA tano usiku hao mashetani wanatumia muda upi kwenda kuzimu??? Maana wanaweza kuwa wanatumia masaa ya Israel Mimi huku nikajisumbua tu kusali SAA nane kumbe wao wapo active
 
Nnaona Mshana nae katujibu kwenye mtandao wa kigiriki wanadai alikuwa mke wa Adam wa kwanza
Kwenye kitabu cha Quran au Bible hizo website hata wewe kuanzisha yako ukawa unawadanganya watu pia na kwakuwa watanzania wanapenda filamu za kutisha basi lazima uwavute ubongo...
 
Sasa Tanzania ukiwa SAA nane usiku na marekani labda saa 12 jioni na UK labda SAA tano usiku hao mashetani wanatumia muda upi kwenda kuzimu??? Maana wanaweza kuwa wanatumia masaa ya Israel Mimi huku nikajisumbua tu kusali SAA nane kumbe wao wapo active
Muda na wakati wa mwanadamu si wa Mungu
 
Kwenye kitabu cha Quran au Bible hizo website hata wewe kuanzisha yako ukawa unawadanganya watu pia na kwakuwa watanzania wanapenda filamu za kutisha basi lazima uwavute ubongo...
Pitia vizuri comments zangu angalia na attachment nilizoambatanisha
 
Mkuu prosper nimepitia comments za watu zote, kuna mambo makuu mawili
1) Nguvu za Giza
2) Nguvu za Mungu
Ethical ameelezea vyema kabisa kuhusu agano la kale na agano jipya, rejea kwamba agano la kale watu walikuwa wanaadhibiwa directly kwa dhambi zao ila agano jipya hakuna hilo jambo
Mleta mada anaweza kuwa sahihi au pia asiwe sahihi, dunia ya sasa hivi imeharibiwa sana kwa ujuaji na ndio sababu maandiko yanasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Zimezuka stori nyingi zinazohusu kuzimu na kila mtu anajikuta anaijua kuzimu sana jambo ambalo ni nadharia tupu. Pili nasikitika sana ninaposoma comments za mtu anasema kama Mleta mada ni mwongo basi weka wewe tulinganishe nani ni mwongo, hii inaonesha ni kwa kiasi gani watu hawa wameaminishwa na sio wasomaji wazuri wa maandiko hivyo hata wakiletewa ushahidi roho zao zimeshafungwa.
Huwa naonaga watu wengi wanaoandika kuhusu mambo ya kuzimu na sijawahi changia kama kina mshana, jichawi, mzizimkavu na wengineo na masikitiko yangu watu wamesahau maandiko ya Quran na Biblia na kuwa interested na topic za namna hii...akili yako ukiijaza vitu hivi basi utaishia kuamini na kusahau ukweli upo wapi.
By the way siamini swala la sala kuzuiwa angani kama ozone layer inavyozuia miale mikali ya jua kuingia duniani...shetani hana Nguvu ya kuzuia maombi yako Bali Ana Nguvu ya ushawishi, mfano kama ulipanga usali saa saba mchana basi atakutia vishawishi na usisali ila ukishikilia msimamo wako unakuwa umemshinda. Pia tulipoambiwa tusali sana sio kwasababu ya maombi yetu kuzuiwa kama Mleta mada anavyodai la hasha Bali sababu ibilisi Ana Nguvu kubwa ya ushawishi hivyo kwa uwezo wetu hatuwezi kushinda ushawishi wake hivyo tunapaswa kujitakasa kila Mara ili roho mtakatifu atuongoze kushinda vishawishi hivyo. Adamu na Eva ukisoma kwa makini utaona mbinu anayoitumia ibilisi hakumshurutisha Eva ale lile tunda bali alimshawishi na ushawishi wake ukafanikiwa. Sasa tafakari kama Adamu na Eva hakukuwa na dhambi lakini alifanikiwa kumshawishi vizuri tu vipi kuhusu sisi tunaoishi kwenye ulimwengu uliojaa dhambi?!
Hivyo maombi hayazuiwi bali mapepo yana kazi kubwa ya kukushawishi na usipokuwa na imani dhabiti unashawishika na kuangamia kabisa...fact za kuzimu hazina ushahidi kwani kwangu nazifananisha na hadithi za Eric Shigongo kuuza vitabu na magazeti
Kuna Jambo Ambalo Nafikiri bado Hatujalielewa, Tunaposema Shetani Huzuia Maombi Ya Watu Kufika Kwa Mungu Ama Kufeli Haina Maana Tunazungumzia Kwa Upande Mmoja Tu Bali Kwa Pande Zote Bila Kujali Ni Ushawishi Au Lah.

Mtoa Uzi Anaeleza Anayoyajua Na Ninyi Mnaopinga Ni Vyema Mkafahamu Kwmb Linaloelezwa Lipo Hata Kwny Vitabu Vya Mungu Lipo.

Kumbukeni Kwmb Hata Yesu Alipoenda Kufunga Na Kusali Alikutana Na Shetani Na Shetani Alimwambia Yesu Amuabudu Lakn Yesu Alikataa. Bila Yesu Kuwa Na Imani Thabiti Yesu Asingeshinda.
So Ushawishi Pia Ni Chanzo Cha Kumkwamisha Muombaji Kujibiwa Maombi Yake.

Tujipange Kuelewa Na Si Kupinga, Kama Tunapinga Basi Tuje Na Hoja Badala Ya Kumuita Mtu Muongo Au Anaaminisha Mambo Yasiyo.
 
Mkuu angesema kuhusu kushawishi waaala nisingetia neno lakini hilo la kutanda angani kama ozone layer kuzuia maombi hilo nitapinga kabisa. Nadhani pia nilieleweka niliposema tuliambiwa tusali sana ili roho mtakatifu atujaze ujasiri wa kushinda vishawishi vya yule mwovu ibilisi na sio kushinda ozone layer ya mapepo angani...ndio maana mwisho nilimalizia kusema mambo ya kuzimu ni ya kusaidikika ila kwakuwa kizazi cha sasa kinapenda sana kusikia habari za kuzimu ndio kila mmoja anakuja na lake kama babu wa loliondo alivyooteshwa...ila zitabakia kuwa nadharia tupu hakuna ajuaye ya mbinguni wala kuzimu isipokuwa Yesu Kristo pekee ambaye alishinda mauti mengine ni hadithi za abunuasi ili kuuza vitabu
 
Back
Top Bottom