Mfahamu Jaili: Chinja chinja aliyevuma Mbeya na Mama yake aliyekufa na kufufuka mara tatu

Mbeya kwa matukio hatari sana

Mara Jombi, Jaili , wachuna ngozi ,wapiga nondo hatari sana

Nakumbuka marehemu shemu wangu Kuna siku nilikuwa kwake mitaa ya block T karibu kabisa na Uwanja wa ndege

Jamaa alikuwa dereva wa mabasi ya St Mary pale Forest

Sasa anatoka saa 11.30 kuchukua Basi awafate watoto mbalizi

Akafika mitaa ya karibu na SIDO wapiga nondo wakaanza kumkimbiza

Tuko ndani tunasikia sauti mtu anapiga kelele"fungua mlango " hapo yuko mbio

Daaah Mbeya nuksi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
nacheka hadi najishtukia

na hii swaumu mguno hautoki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku kova alipokoswakoswa na risasi kwenye ile supermarket nilikuwepo.

Siku mwanjelwa ilipoungua nilikuwepo.

Siku ndege ya yule waziri ilipodondoka nilikuwepo.

Siku wezi walipomfungia mwizi mwenzao kwenye box mwanjelwa dukani nilikuwepo.

Siku JK alipopoigwa mawe na alipochochola kule kilimo kwenda tukuyu nilikuwepo.

Siku Malawi walipoleta nyenyenye kule ziwani nilikuwepo.

Na nilinusurika kumezwa na chatu hapo pia nilikuwepo Mimi na chatu.

Sitaisahau mbeya has maeneo ya said mama John ilomba CCM rrm nilikuwa nakunywa Sana ulanzi na ile pombe inachemshwa kwanza kwenye Moto kwenye vilabu vya mamajohn sai na kule karibu na shule moja wanavaa wasichana suruali nyeusi na mashati ya marindarinda Kama unaelekea polisi ffu mbeya noma Sana niliwahi kudondosha pochi pale njia panda wanapaita mafiati Kama unaelekea mjini Kama unatoka uyole Kama unaenda mbalizi karibu na chuo Cha Tia airport kilikuwa na club moja inajaa Sana usiku ilikuwa pembeni ya ukuta wa Tia mkono wa kushoto Kama unaelekea mbalizi opozit na mbeya carnival Kama sikosei basi nikadondosha pochi iliyokuwa na he'll Kama laki tatu nanusu aisee ilikanyagwa na semi kama tatu huwezi amini niliambulia elfu sabini nyingine zote zilisagwasagwa kwa hasira nikaenda kuilewea yote nikarudi home kwa mguu sikufika nikalala njiani pembeni ya hoteli ipo Soweto inaitwa paradise sitaisahau mbeyaaaaaaaaa
Hizo hela ungepeleka BOT pale forest, hata ukipeleka hela imechomwa moto ila ina namba zile zilizolala na zile za kulia zilizosimama huwa wanakupa not I mpya bila gharama yoyote
 
Nimecheka balaa!!😂😂😂😂😂

Ukifika Mbeya Mjini kuna eneo linaitwa Forest Mpya.

Siku za nyuma eneo hilo lilijulikana tu kama Forest kwa kuwa kulikuwa na msitu mkubwa sana wa miti ya milingoti ambayo Kama huijui ni miti inayozalisha nguzo za umeme na za TTCL.

Huu msitu ndio Jaili aliutumia kuchinja watu ambao alikuwa akiwapiga kwanza na nyundo, Kisha huwapakia kwenye gari na kwenda kuwachinja Forest.

Mama yake Jaili alikuwa ni mchawi sana na alikufa na kufufuka Mara tatu kwenye uhai wake. Na alipokuja Mara ya nne haraka haraka wakaenda kumzika kwenye makaburi ya Nonde.

Mara ya kwanza alifia katika Hospital ya Rufaa Mbeya, enzi hizo ikiitwa Gredi Wani. Alipokufa wakampeleka mortuary, sasa Kuna watu walikuwa na maiti ya ndugu yao kafa kwa ajali, wakati mhudumu anavutavuta mafriji, mama yake Jaili akanyanyuka, na kutembea kwa miguu hadi kwa mwanae mitaa ya Ghana.

Mara ya pili alifia nyumbani kwa mwanae, na akapelekwa mortuary ambako alikaa, na siku walipoenda kumuandaa kwa ajili ya maziko, aliamka na kurudi kuwa hai, watu wakatoka nduki vibaya Sana.

Baada ya siku chache huyu Bibi mwenye mauzauza ambayo USER=98741]Mshana Jr[/USER] hajawahi kuyaona maishani mwake, alifariki Tena, ila Safari hii nimesahau alifufukaje.

Sasa alipokuja kufa Mara ya nne, hawakumchelewesha, Wananzengo fasta wakakimbilia kwenye makaburi ya Nonde, wakachimba kaburi refu sana, ngazi ya zimamoto inazama, wakaandaa na trip ya mawe, jiwe la chuma sio mamoma.

Maiti fasta ikawekwa kwenye jeneza lililotengenezwa kwa mti wa Mkambokambo, ile miti ambayo zamani wakati wa Christmas ilikuwa inauzwa Namanga na Kariakoo Cyprus tree.

Fasta wakaitwa Mchungaji Mwamlima na Mwinjilisti Mwaibofu wa wa kanisa la Moravian. Mwili wa marehemu hakuingizwa kanisani kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya mwisho. Moja kwa moja ikapelekwa Nonde, Mwamimwa akaendesha ibada huko. Ibada ilikuwa fupi Sana kuokoa muda ili asifufuke Tena.

Jeneza likashushwa huko kaburini, kwa namna ya kuvurumushwa.
Lile tipper ambalo lilikuwa na trip ya mawe, likabenua mawe yote Ndani ya kaburi.
Baada ya hapo vijana wakapiga posolo /chepe za kutosha kumfukia marehemu.

Huu msiba ulisisimua sana, watu wa Ghana, Mbata, Majengo, Nonde, Mabatini na hata Mwanjelwa walifika kuona mazishi hayo ya kigagula. Huyu Mama ndiye aliyekuwa anafanya mwanawe Jaili asikamatwe, na hata akikamatwa alikuwa anatoroka jela. Jaili alikufa miaka ya 1998/99 na kuzikwa Nonde.

Jaili ameishi maisha ya uzee kwa mateso makubwa, alikuwa anashinda Uhindini kwa Wahindi akiwaomba hela, wakimnyima anatishia kutoa Siri zao.

Mtoto wake aitwaye Manyenye alikuwa tishio Sana, naye alikufa siku chache baada ya kifo Cha baba Yake.
 
Loli lelo alendosi umwanike ujho..
 
Alikuwa ni Mmanyafu, kabila dogo sana linalopatikana kwenye mpaka wa wilaya ya Rungwe na Ileje Kijiji Cha Ikuti.

Kijijini hapo unapita mto Songwe/Kiwira. Kijiji chote ni wachawi sana na mto huu mkubwa ukifika kijijini hapo, huwa mdogo kabisa, kiasi cha kuweza kuruka kwa miguu.

Ukiruka mto hupanuka na wewe kudumbukia Ndani na kupoteza maisha. Kitendo hicho huitwa na wenyeji ATINYELITE BUKOMU kwamba hajaruka vizuri.

Jubha!
 
Asante kikolo, ule msitu ulikuwa unaonekana vema ukiwa maeneo ya juu pale Simike nyuma ya hospitali ya Wazazi! Nowadays msitu is gone watu wametia mijengo like a Disney land!
Hivi ni Simike au Isimike mkuu ?? Huwa nachanganya !!
 
Back
Top Bottom