Mfahamu Jaili: Chinja chinja aliyevuma Mbeya na Mama yake aliyekufa na kufufuka mara tatu

Nilijua tu lazima Kuna mtu atajibu hivyo.

Hawa watu walitumia mizizi na majani tu kufanya yao.

Miti imeumbwa na Mungu alikuyekuumba wewe!!

Mzungu alivokuja alipuuza vitu vyetu vyote akasema vya kishenzi..Leo hi tunarudi kwenye ushenzi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tofautisha uchawi na tiba za miti shamba.
Mzungu aliviita vitu vyetu vya kishenzi ni kweli, badala ya ngoma za asili alileta dansi na disco, alileta utamaduni wake.
Lakini kabla ya ujio wa wazungu uchawi ulipingwa na jamii yote.
 
Ila natamani uwezo huu basi tu, mtu akinizingua namsulubu on the spoti. Kwanini watu hawakutaka huyo mama aishi? alikuwa anajifufua? alikuwa anauliwa? angekuwepo leo ninemtembelea anisimulie kwanini ana uwezo huo,nami nitumie kufufua ndugu, teh namini nikifa nifufuke.
Jifukize, kula malimao na tangawizi huku unaongeaongea maneno ya Kiarabu utashangaa unapata nguvu na uwezo wa ajabu, kiasi kwamba unaweza rudisha miaka nyuma.
 
Pia miaka ya mwanzoni mwa 80 kulikuwa na wachanjaji, wakikupiga chale zao unakufa. Vitanda vyumbani vikasogezwa katikati ya chumba, kitanda kikikaa ukutani wanakupiga chale zao za kichawi.

Chale ilichanjwa kwenye mgomba na aliye Ndani anaathirika, na kufa. Mfu huenda kuwekwa ndondocha
Duh.....basi ndo maana mwalimu alikuwa vile, sio kwa uchawi huu
 
Ni kweli inawezekana walikuwa wanaepusha madhara kwa watu. Tatizo la pale ni moja tu, lina kina kirefu sana katikati hivyo hata wenyeji wanafanyia shughuli zao pembeni kabisa mwa ziwa, ukisogea sana imekula kwako.
Ooh, ok nimeelewa sababu sasa, ngoja siku ntaenda kutembea ila sitakagi mazoea na maji, ntaishia kuangalia kwa mbalii😀😀
 
Tofautisha uchawi na tiba za miti shamba.
Mzungu aliviita vitu vyetu vya kishenzi ni kweli, badala ya ngoma za asili alileta dansi na disco, alileta utamaduni wake.
Lakini kabla ya ujio wa wazungu uchawi ulipingwa na jamii yote.
Kama mchawi anatumia majani na mizizi inatofauti gani na tiba asili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwe
Ukifika Mbeya Mjini kuna eneo linaitwa Forest Mpya.

Siku za nyuma eneo hilo lilijulikana tu kama Forest kwa kuwa kulikuwa na msitu mkubwa sana wa miti ya milingoti ambayo Kama huijui ni miti inayozalisha nguzo za umeme na za TTCL.

Huu msitu ndio Jaili aliutumia kuchinja watu ambao alikuwa akiwapiga kwanza na nyundo, Kisha huwapakia kwenye gari na kwenda kuwachinja Forest.

Mama yake Jaili alikuwa ni mchawi sana na alikufa na kufufuka Mara tatu kwenye uhai wake. Na alipokuja Mara ya nne haraka haraka wakaenda kumzika kwenye makaburi ya Nonde.

Mara ya kwanza alifia katika Hospital ya Rufaa Mbeya, enzi hizo ikiitwa Gredi Wani. Alipokufa wakampeleka mortuary, sasa Kuna watu walikuwa na maiti ya ndugu yao kafa kwa ajali, wakati mhudumu anavutavuta mafriji, mama yake Jaili akanyanyuka, na kutembea kwa miguu hadi kwa mwanae mitaa ya Ghana.

Mara ya pili alifia nyumbani kwa mwanae, na akapelekwa mortuary ambako alikaa, na siku walipoenda kumuandaa kwa ajili ya maziko, aliamka na kurudi kuwa hai, watu wakatoka nduki vibaya Sana.

Baada ya siku chache huyu Bibi mwenye mauzauza ambayo USER=98741]Mshana Jr[/USER] hajawahi kuyaona maishani mwake, alifariki Tena, ila Safari hii nimesahau alifufukaje.

Sasa alipokuja kufa Mara ya nne, hawakumchelewesha, Wananzengo fasta wakakimbilia kwenye makaburi ya Nonde, wakachimba kaburi refu sana, ngazi ya zimamoto inazama, wakaandaa na trip ya mawe, jiwe la chuma sio mamoma.

Maiti fasta ikawekwa kwenye jeneza lililotengenezwa kwa mti wa Mkambokambo, ile miti ambayo zamani wakati wa Christmas ilikuwa inauzwa Namanga na Kariakoo Cyprus tree.

Fasta wakaitwa Mchungaji Mwamlima na Mwinjilisti Mwaibofu wa wa kanisa la Moravian. Mwili wa marehemu hakuingizwa kanisani kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya mwisho. Moja kwa moja ikapelekwa Nonde, Mwamimwa akaendesha ibada huko. Ibada ilikuwa fupi Sana kuokoa muda ili asifufuke Tena.

Jeneza likashushwa huko kaburini, kwa namna ya kuvurumushwa.
Lile tipper ambalo lilikuwa na trip ya mawe, likabenua mawe yote Ndani ya kaburi.
Baada ya hapo vijana wakapiga posolo /chepe za kutosha kumfukia marehemu.

Huu msiba ulisisimua sana, watu wa Ghana, Mbata, Majengo, Nonde, Mabatini na hata Mwanjelwa walifika kuona mazishi hayo ya kigagula. Huyu Mama ndiye aliyekuwa anafanya mwanawe Jaili asikamatwe, na hata akikamatwa alikuwa anatoroka jela. Jaili alikufa miaka ya 1998/99 na kuzikwa Nonde.

Jaili ameishi maisha ya uzee kwa mateso makubwa, alikuwa anashinda Uhindini kwa Wahindi akiwaomba hela, wakimnyima anatishia kutoa Siri zao.

Mtoto wake aitwaye Manyenye alikuwa tishio Sana, naye alikufa siku chache baada ya kifo Cha baba Yake.
kweli maajabu hayaishi
 
Wanyakyusa tumewachia uwanja,leteni madini na siri za mkoa wenu
 
Back
Top Bottom