Mfahamu Double Agent wa CIA na EIJ aliyemfundisha OSAMA mbinu za kigaidi na vita

wachilamu utawajua tu jinchi wanavyopenda kuchifia ugaidi.
bhaaa.!
Wewee Y-N acha ujinga wewe hapa tunachambua UKWELI,UNAFIKI,UJASUSI,UHAINI,nk.. ilitupate taswira kamili ya majngaa ya yanyojirii Duniani na hata kizingitini hapa nchini! Chukuwa fursa hii ujifunze uhakika yasijekukuta by surprise!! Acha kushadidia chuki za kidini... JUST BE FAIR.
Take care and Good luck.
 
ukisoma paragraph mbili za mwisho utaona, yupo marekani lakini alipo haijulikani na inasemekana hajahukumiwa huku akitoa ushirikiano kwa marekani, kwa ninavyoona mimi huyu ni mtu wao so amepumzishwa fulani tu. kuna kipindi wananchi wa marekani walilalamika kwa nini hajahukumiwa lakini mengi zaidi wanajua wao

Umri wake je?!
 
Ukiangalia kwa nje nikama alikuwa kastaafu vile ila amini ilikuwa ni port of entry!!!!!

That might be the case

Kuna mfano mwingine wa huyo Alexander Lebedev,ex-kgb and filthy rich

Mlolongo ni mrefu wa ex-kgb operatives ambao sasa ni wafanyabiashara wa kubwa Russia
 
That might be the case

Kuna mfano mwingine wa huyo Alexander Lebedev,ex-kgb and filthy rich

Mlolongo ni mrefu wa ex-kgb operatives ambao sasa ni wafanyabiashara wa kubwa Russia

Ni watu muhimu na hatari hawa sasa huwezi muacha tu akizurura na unajua ujuzi hauzeeki!!!!!

Sasa kama sio madaraka ni kutengenezewa kampuni na yeye ukiendesha huku akiwa on and off duty au permanent silencing!!!!!

Kwa wanaobaki na nidhamu na kuzingatia viapo ni aidha madaraka au "biashara" na waliokuwa imani nusu basi option ya tatu ni lazima how and when ndio task ya wengine wenye specialization hiyo!!!!!
 
Katika tasnia ya ujasusi miaka ya nyuma KGB walikuwa juu sana,waliweza kuweka watu wao MI6 na CIA na wakawa na nafasi za juu katika taasis hizo,kwa sasa sijui kama bado wananguvu kama enzi hizo,pia wapakstan nao wako vizuri kwa upande wa asia
 
niliwahi kutazama a full documentary video ya huyu jamaa ( Ali Abdoul Saoud Mohamed)kule youtube,ikimzungumzia yeye na ushirika kama jasusi na agent wa CIA.nilibaki mdomo wazi.
 
Katika tasnia ya ujasusi miaka ya nyuma KGB walikuwa juu sana,waliweza kuweka watu wao MI6 na CIA na wakawa na nafasi za juu katika taasis hizo,kwa sasa sijui kama bado wananguvu kama enzi hizo,pia wapakstan nao wako vizuri kwa upande wa asia

KGB ambao sasa ni FSB wako vizuri sana.walibadilisha jina tu maana hadi jengo la HQ ni lile lile.Angalia link hiyo

http://rt.com/news/fsb-detain-cia-agent-253/
 

View attachment 129168
View attachment 129169

Ni Ali Abdoul Saoud Mohamed alikuwa double agent wa CIA na EIJ( Egyptian islamic jihad) ambayo ndio ilipelekea kuundwa kwa ALQAEDA huku yeye akiwa mwendesha mafunzo wa mbinu za kivita na kijasusi wa kwanza kwenye kambi zao kwa ajili ya kuwaandaa na mapambano dhidi ya utawala wa kisovieti nchini Afghanistan miaka ya 90. yeye ndiye mwalimu wa kwanza wa Osama bin Laden na Ayman Zawahiri( kiongozi wa sasa wa Alqaeda)

Ali anaelezwa kuwa mtu mwenye uzito wa kilo 90, urefu futi 6 huku akielezwa mtu aliye fiti kimwili, aliyebobea kwenye sanaa za mapigano( martial art),mwenye ufahasa mzuri wa lugha za kiingereza,kifaransa,kiyunani na kiarabu. alikuwa mwenye nidhamu ya juu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye kujichanganya na watu na uwezo wa kupata marafiki kwa urahisi.


Ali alikuwa major katika kitengo cha ujasusi katika jeshi la misri kabla ya kuachishwa kazi mwaka 1984 kwa tuhuma za kusika katika harakati udini dhidi ya utawala wa Anwar Saadat wa misri, harakati zilizopelekea kuuawa kwa Saadat


Uhusiano wake na CIA
kwa mara ya kwanza aliingia marekani kama mkalimani wa Ayman Zawahiri( kiongozi wa sasa wa alqaeda) wakati alipoenda kuchangisha michango kusaidia wana mgambo katika harakati za kuutoa utawala wa wasovieti Aghanistan.kwa maelezo inasemekana Zawahiri almshauri a-infiltrate marekani, mwaka 1984. Ali anaelezwa aliweza kuingia kwenya kituo cha CIA Cairo,Egypt kwa urahisi na kuweza kuongea na mkuu wa kituo kuhusu ofa yake ya kufanya nao kazi. akawa recruited kama junior intelligence officer. kazi ya kwanza alipewa ni kupenya ndani ya msikiti mmoja mjini hamburg ujerumani uliosemekana kuwa na mahusiano na wanamgambo wa Hizbollah wa nchini Lebanon lakini cha ajabu akawataarifu viongozi kuwa yeye ni jasusi wa CIA ametumwa kuchukua taarifa, kwa kuwa katika ule mkusanyiko alikuwepo jasusi mwingine wa CIA, taarifa juu ya alichokifanya Ali zikawafikia mabosi CIA. Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa jarida la New Yorkers na mshirika wa kituo cha sheria na usalama New York University of Law Lawrence Wright ni kwamba ulitumwa ujumbe wa limawasiliano kutoka CIA ukitaarifu kuwa Ali sio mtiifu na ameshadhibitiwa, lakini mda huo taarifa inatumwa tayari Ali mohamed alikuwa mjini Carlifonia kushiriki program maalum ya kuwapatia ruhusa ya kuingia marekani bila kuwa na visa kwa 'Valuable assets' waliolifanyia taifa la Marekani utumishi wa hali ya juu, program ambayo yenyewe pia ilikuwa ikifadhiliwa na CIA. Ali akafanikiwa kuoa mmarekani Linda Sanchez na akachukuliwa kwenye special forces na akapangwa katika kambi kubwa ya Fort bragg kama drill commander( sijui kwa kiswahili wanaitwaje, yani wale ambao wanawapokea makuruta na kuwafundisha maisha ya jeshini, taratibu na nidhamu) pia alishawishiwa na CIA kusomea masomo ya dini ya kiislamu ili akafundishe mashariki ya kati


mnamo mwaka 1988 Ali aliwataarifu wakuu wake jeshini kuwa anachukua likizo fupi kwa ijili ya kwenda afghanistan kupambana na wasovieti( huko ndio akawa anatoa mafunzo kwa wanamgambo waanzilishi wa Alqaaeda). Huku nyuma afisa mwandamizi wa Ali, Lt. Col Robert Anderson aliandika ripoti ya kina ikilenga kutaka idara ya ujasusi ya jeshi kumchunguza Ali na kumfungulia mashtaka lakini taarifa yake hiyo ilipuuzwa. anaeleza kuwa '' Kuwa na mwanajeshi mmisri, aliyehusika na mauji ya rais wa zamani wa misri Saadat, alafu akapata visa ya kuja kuishi marekani na akachukuliwa kwenye vikosi maalum vya jeshi(special forces) inashangaza, haya mambo hayatokei tu hivi hivi" anaendelea kueleza kuwa ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa mwanajeshi wa kawaida wa Marekani kupigana vita katika jeshi la nje bila kuadhibiwa. akaendelea kusema anaamini atakuwa anafadhiliwa na shirika la kijasusi la kimarekani.



Ali aliendelea kutoa mafunzo kwa wana mgambo wa kiislamu wa Maktab al-Khidamat (iliyoanzishwa na Abdullah Azzam ambayo baadae alijiunga Osama, wakagombana hatimae Osama akaigeuza kuwa ALQAEDA baada ya ku-win popularity over Azzam)nchini marekani kupitia Kambi ya Al Kifah iliyokuwepo mjini brooklyn iliyokuwa akisapotiwa na Marekani kwa ajili ya kuwawaezesha kuutoa utawala wa kisovieti nchini Afghanistan


miaka ya 90 akarudi tena Afganistani ambako alitoa mafunzo ya kijasusi ikiwemo, kuteka watu, kuteka ndege, jinsi ya kuua n.k na inasemekana katika wanafunzi wake wa kwanza kabisa ni Osama bin laden, Ayman Zawahiry(kiongaozi wa sasa wa Alqaeda) na viongozi wengine wa Alqaeda kwa mijibu wa FBI special agent Jack Cloonan


mwaka 1993 akiwa ndani ya Alqaeda akawa informant wa FBI, na mmoja wa wapigaji wa ALQAEDA Mohamed Atyf aliyepewa jukumu la kufanya survey katika ubalozi wa marekani nchini kenya(uliolipuliwa mwaka 1998) alikataa kumtajia Ali passport namba yake kwa kuwa alikuwa na mashaka kuwa Ali alikuwa ni mshirika wa Marekani


wiki mbili baada ya balozi za marekani nchini Kenya na Tanzania kulipuliwa, FBI walisachi makao ya Ali na kukuta nyaraka mbalimbali zenye ushahidi juu ya kuhusika kwa na milipuko nchini Kenya na Tanzania na kukamatwa. Ali alikubali makosa ya kigaidi na akaeleza mwanza mwisho kuhusu ushiriki wake katika kundi la Al qaeda, akakiri makosa ili apate kifungo cha maisha jela bila msamaha wowote ule


mwaka 2001 gazeti la Raleigh News and Observer lilitaarifu kuwa Ali anatoa ushirikiano kwa serikali ya marekani, naeleza kamanda mstaafu wa Delta force katika kitabu chake cha The Mission,The Men and Me:Lessons from former Delta Force Commander Pete Blaber ''Mawakili wa utetezi wanaamini kuwa Ali hajahukumiwa na anasirikiana na serikali japo serikali haijathibitisha hilo,akihukumiwa anaweza akahukumia kidogo, kama miaka 25 kwa mujibu wa makubaliano yao"

mwaka 2006, mke wa Ali Linda Sanchez alisema kuwa mumwe bado hajahukumiwa na haruhusiwi kuzungumza na yeyote "yani wamemshikilia kiusiri sana ni kama vile amepotelea kwenye hewa"






yaliyotokea 1998 tunaomba yasitokee tena ilikuwa noma

Tanzania tulikuwa hatuna hili wala lile masikini
 
Hakuna chances huko mkuu umesikia ya South Africa leo? ?!!!!!
Umesikia Snowden anavyohitajika???!!!!

Kama angesaliti "kweli" saa hizi ingekuwa historia hakuna litmus ya msaliti kwenye ujasusi "before a man there is a man and after a man there is a man"!!!!!!!
kweli kabisa mkuu
 
Wewee Y-N acha ujinga wewe hapa tunachambua UKWELI,UNAFIKI,UJASUSI,UHAINI,nk.. ilitupate taswira kamili ya majngaa ya yanyojirii Duniani na hata kizingitini hapa nchini! Chukuwa fursa hii ujifunze uhakika yasijekukuta by surprise!! Acha kushadidia chuki za kidini... JUST BE FAIR.
Take care and Good luck.

watu km hawa wasiopenda kufikiri ndio hupelekwa hovyo
 
yaliyotokea 1998 tunaomba yasitokee tena ilikuwa noma

Tanzania tulikuwa hatuna hili wala lile masikini

tuombe mungu kwa kweli, sasa sijajua huu ukaribu uliomarika na marekani utatuweka mbali au karibu na matukio haya?
 
Katika tasnia ya ujasusi miaka ya nyuma KGB walikuwa juu sana,waliweza kuweka watu wao MI6 na CIA na wakawa na nafasi za juu katika taasis hizo,kwa sasa sijui kama bado wananguvu kama enzi hizo,pia wapakstan nao wako vizuri kwa upande wa asia

kilichowapaisha wapakistani ni ushirikiano wao na CIA, ulianza mda mrefu sana tangu zama hizo za huyu jamaa
 
Mkuu nimependa andiko lako.


donkey.gif
 
Reborn !! kwa hali iliyokuwepo sasa kundi linajizaa upya na kurudi kwa mfumo wa kisasa!!
 
kweli, hawa CIA ni noma sana.. i do believe ndio wanaendesha Al-qaeda


Mbona hata former US Secretary of State, Hillary Clinton alishakili kuwa Al Qaeda wanafadhiliwa na CIA. Until then, ndipo akili yamgu ilifunguka na kuona kila kitu hapa duniani ni planned, mambo hayatokei yenyewe tu...
 
Mbona hata former US Secretary of State, Hillary Clinton alishakili kuwa Al Qaeda wanafadhiliwa na CIA. Until then, ndipo akili yamgu ilifunguka na kuona kila kitu hapa duniani ni planned, mambo hayatokei yenyewe tu...

sasa kuna watu hawataki hata kufikiria mkuu, kweli kabisa mambo kama haya hayatokei tu hivi hivi
 
mmeisahau mossad ya Israel? Hiyo ndo noma sasa,majasusi wa mossad wametapakaa dunia nzima na huwezi kuwajua hata kidogo,kuna wengine wanajifanya ma padre ma sister,wapo ktk taasisi za kimataifa kama UNHCR,UNICEF,UN na nk,tena wengi wao wakitumia paspot za mataifa mengine,ili kuficha utaifa wao,hata hapa TZ tunao wengi,mwaka 2007 nikiwa nafanya bulyanhulu gold mine,nilishangaa kumuona mzungu mmoja akiwa anajua kiswahili vyema ana uraia wa canada ila cha ajabu anaijua mno israel na kuizungumzia mara nyingi kuliko canada,nataka niwaeleze kuwa,hawa mabalozi wa marekani ktk nchi mbalimbali ni majasusi namba 1 wa CIA,nyie huwa mnadhani hao ni diplomats,marekani na Israel si mataifa ya kawaida ktk medani za kijasusi,ni hatari sana.

Kweli kabisa, inabidi tubadilike nasi kwani miaka hii siyo ya kipindi kile cha 60's na 70's.
 
Back
Top Bottom