Mfahamu Double Agent wa CIA na EIJ aliyemfundisha OSAMA mbinu za kigaidi na vita

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,565
2,000
ali2.jpg
628x471.jpgNi Ali Abdoul Saoud Mohamed alikuwa double agent wa CIA na EIJ( Egyptian islamic jihad) ambayo ndio ilipelekea kuundwa kwa ALQAEDA huku yeye akiwa mwendesha mafunzo wa mbinu za kivita na kijasusi wa kwanza kwenye kambi zao kwa ajili ya kuwaandaa na mapambano dhidi ya utawala wa kisovieti nchini Afghanistan miaka ya 90. yeye ndiye mwalimu wa kwanza wa Osama bin Laden na Ayman Zawahiri( kiongozi wa sasa wa Alqaeda)

Ali anaelezwa kuwa mtu mwenye uzito wa kilo 90, urefu futi 6 huku akielezwa mtu aliye fiti kimwili, aliyebobea kwenye sanaa za mapigano( martial art),mwenye ufahasa mzuri wa lugha za kiingereza,kifaransa,kiyunani na kiarabu. alikuwa mwenye nidhamu ya juu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye kujichanganya na watu na uwezo wa kupata marafiki kwa urahisi.

Ali alikuwa Major katika kitengo cha ujasusi katika jeshi la misri kabla ya kuachishwa kazi mwaka 1984 kwa tuhuma za kusika katika harakati za kidini dhidi ya utawala wa Anwar Saadat wa misri, harakati zilizopelekea kuuawa kwa Saadat

Uhusiano wake na CIA
Kwa mara ya kwanza aliingia marekani kama mkalimani wa Ayman Zawahiri( kiongozi wa sasa wa alqaeda) wakati alipoenda kuchangisha michango kusaidia wana mgambo katika harakati za kuutoa utawala wa wasovieti Aghanistan.kwa maelezo inasemekana Zawahiri alimshauri ajipenyeze kwenye mifumo na vyombo vya Marekani. Ali anaelezwa aliweza kuingia kwenya kituo cha CIA Cairo,Egypt kwa urahisi na kuweza kuongea na mkuu wa kituo kuhusu ofa yake ya kufanya nao kazi. hatimaye akawa recruited kama junior intelligence officer. Kazi ya kwanza aliyopewa ni kupenya ndani ya msikiti mmoja mjini Hamburg Ujerumani uliosemekana kuwa na mahusiano na wanamgambo wa Hizbollah wa nchini Lebanon, lakini cha ajabu akawataarifu viongozi wa msikiti kuwa yeye ni jasusi wa CIA na ametumwa kuchukua taarifa. Kwa kuwa katika ule mkusanyiko alikuwepo jasusi mwingine wa CIA, taarifa juu ya alichokifanya Ali zikawafikia mabosi CIA. Kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa jarida la New Yorkers na mshirika wa kituo cha sheria na usalama New York University of Law bwana Lawrence Wright ni kwamba ulitumwa ujumbe kupitia mawasiliano kutoka CIA ukitaarifu kuwa Ali sio mtiifu tena na ameshadhibitiwa, lakini mda huo taarifa inatumwa tayari Ali Mohamed alikuwa mjini Carlifonia kushiriki program maalum ya kuwapatia ruhusa ya kuingia Marekani bila kuwa na visa kwa 'Valuable assets' waliolitumikia taifa la Marekani utumishi wa hali ya juu, program ambayo yenyewe pia ilikuwa ikifadhiliwa na CIA. Ali akafanikiwa kuoa mmarekani Linda Sanchez na baadae kidogo akachukuliwa kwenye na Special Forces na kupangwa katika kambi kubwa ya Fort bragg kama drill commander. Pia alishawishiwa na CIA kusomea masomo ya dini ya kiislamu ili akafundishe mashariki ya kati

Mnamo mwaka 1988 Ali aliwataarifu wakuu wake jeshini kuwa anachukua likizo fupi kwa ajili ya kwenda nchini Afghanistan kupambana na wasovieti( huko ndio akawa anatoa mafunzo kwa wanamgambo waanzilishi wa Alqaeda). Huku nyuma afisa mwandamizi wa Ali, Lt. Col Robert Anderson aliandika ripoti ya kina ikilenga kutaka idara ya ujasusi ya jeshi kumchunguza Ali na kumfungulia mashtaka lakini taarifa yake hiyo ilipuuzwa. anaeleza kuwa '' Kuwa na mwanajeshi mmisri, aliyehusika na mauji ya rais wa zamani wa misri , halafu akapata visa ya kuja kuishi Marekani na kuchukuliwa kwenye vikosi maalum vya jeshi(special forces) inashangaza, haya mambo hayatokei tu hivi hivi" anaendelea kueleza kuwa ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa mwanajeshi wa kawaida wa Marekani kupigana vita katika jeshi la nje bila kuadhibiwa. Akaendelea kusema anaamini atakuwa anafadhiliwa na shirika la kijasusi la kimarekani CIA.


Ali aliendelea kutoa mafunzo kwa wana mgambo wa kiislamu wa Maktab al-Khidamat (iliyoanzishwa na Abdullah Azzam ambayo baadae alijiunga Osama, wakagombana hatimae Osama akaigeuza kuwa ALQAEDA baada ya ku-win popularity over Azzam)nchini marekani kupitia Kambi ya Al Kifah iliyokuwepo mjini brooklyn iliyokuwa akisapotiwa na Marekani kwa ajili ya kuwawaezesha kuutoa utawala wa kisovieti nchini Afghanistan

Miaka ya 90 akarudi tena Afghanistan ambako alitoa mafunzo ya kijasusi ikiwemo, kuteka watu, kuteka ndege, jinsi ya kuua n.k na inasemekana katika wanafunzi wake wa kwanza kabisa ni Osama bin laden, Ayman Zawahiri(kiongaozi wa sasa wa Alqaeda) na viongozi wengine wa Alqaeda kwa mujibu wa FBI special agent Jack Cloonan

Mwaka 1993 akiwa ndani ya Alqaeda akawa informant wa FBI, na mmoja wa wapigaji wa ALQAEDA Mohamed Atyf aliyepewa jukumu la kufanya survey katika ubalozi wa marekani nchini kenya(uliolipuliwa mwaka 1998) alikataa kumtajia Ali passport namba yake kwa kuwa alikuwa na mashaka kuwa Ali alikuwa ni mshirika wa Marekani

Wiki mbili baada ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania kulipuliwa, FBI walisachi makao ya Ali na kukuta nyaraka mbalimbali zenye ushahidi juu ya kuhusika kwa na milipuko nchini Kenya na Tanzania na akakamatwa. Ali alikubali makosa ya kigaidi na akaeleza mwanzo mwisho kuhusu ushiriki wake katika kundi la Al qaeda, akakiri makosa ili apate kifungo cha maisha jela bila msamaha wowote ule

Mwaka 2001 gazeti la Raleigh News and Observer lilitaarifu kuwa Ali anatoa ushirikiano kwa serikali ya marekani, anaeleza kamanda mstaafu wa Delta force katika kitabu chake cha The Mission,The Men and Me:Lessons from former Delta Force Commander,bwana Peter Blaber ''Mawakili wa utetezi wanaamini kuwa Ali hajahukumiwa na anasirikiana na serikali japo serikali haijathibitisha hilo,akihukumiwa anaweza akahukumia kifungo kidogo, kama miaka 25 kwa mujibu wa makubaliano yao"

Mwaka 2006, mke wa Ali Linda Sanchez alisema kuwa mumewe bado hajahukumiwa na haruhusiwi kuzungumza na yeyote. "wamemshikilia kwa usiri mkubwa, ni kama vile amepotelea kwenye hewa" alieleza mke Ali
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,565
2,000
wachilamu utawajua tu jinchi wanavyopenda kuchifia ugaidi.
bhaaa.!
hapana sio kusifia ni kuweka mambo wazi, nadhani umewahi kusikia conspiracies kuwa Osama anaushirika n maekani, na pia alikuwa akimiliki hisa katika makampuni mbalimbali nchini marekani, tena sehemu zingine aki-share na rais bush, pia amewahi kupata mafunzo CIA and was their man. nadhani ukisoma huu uzi kuna vitu utagundua kuhusu tetesi hizo na maswali mengi utajiuliza
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,565
2,000
nadhani wamarekani tayari watakuwa wameshatengeneza movie, huwa hawachelewi
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,835
2,000
Ujasusi ni kitu kingine ndio maana hata hapa bongo wanasiasa wanaodhani wameweka mfukoni idara za ujasusi hawajui kuwa wao ndio wamewekwa mfukoni!!
Ukiona jinsi FBI na CIA wanavyoshiriki kwenye uchafu lakini wakiwa na projection za matunda bora baadae kwa Marekani ndio hapo unapoheshimu movement za kijasusi kama nguzo za taifa lolote.
Tuwape TISS mradi wa gesi bana wakue kama CIA (msinitoe macho).
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,565
2,000
Ujasusi ni kitu kingine ndio maana hata hapa bongo wanasiasa wanaodhani wameweka mfukoni idara za ujasusi hawajui kuwa wao ndio wamewekwa mfukoni!!
Ukiona jinsi FBI na CIA wanavyoshiriki kwenye uchafu lakini wakiwa na projection za matunda bora baadae kwa Marekani ndio hapo unapoheshimu movement za kijasusi kama nguzo za taifa lolote.
Tuwape TISS mradi wa gesi bana wakue kama CIA (msinitoe macho).

kweli, hawa CIA ni noma sana.. i do believe ndio wanaendesha Al-qaeda
 

mcmalck

Senior Member
May 25, 2012
134
195
mngony Asante sana kwa taarifa ila ujaimalizia vizur mana tumebak na mawazo currently yuko wap ana fanya nn?
 
Last edited by a moderator:

bysange

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
4,442
2,000
Hili bandiko ni zuri na linamaswali mengi sana au pia Osama wanaye wanaatudhihaki
maana hapa huu muunganiko unanipa mashaka CIA,FBI NA EIJ?mmmh
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,565
2,000
Asante sana kwa taarifa ila ujaimalizia vizur mana tumebak na mawazo currently yuko wap ana fanya nn?
ukisoma paragraph mbili za mwisho utaona, yupo marekani lakini alipo haijulikani na inasemekana hajahukumiwa huku akitoa ushirikiano kwa marekani, kwa ninavyoona mimi huyu ni mtu wao so amepumzishwa fulani tu. kuna kipindi wananchi wa marekani walilalamika kwa nini hajahukumiwa lakini mengi zaidi wanajua wao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom