Mfahamu Camilo Cienfuegos wa Cuba!!

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
Camilo-1.jpg

Camilo akiwa na Che Guevara

images

Hapa akiwa na Castro
Camilo_Cienfuegos.jpg


Jina lake kamili ni Camilo Cienfuegos Gorriaran alizaliwa February 6, 1932 huko Havana, Cuba.
Alikuwa ni Mwanamapinduzi aliyepambana mstari wa mbele katika Mapinduzi ya Cuba ya mwaka 1959 chini ya Makamanda Fidel Castro, Che Guevara, Huber Matos na Raul Castro. Alikuwa ni mmoja wa makamanda wa 26 of July Movement ambao ndio waliongoza Mapinduzi ya Cuba ya Mwaka 1959.

Baada ya Mapinduzi ya Cuba ya mwaka 1959, Camilo Cienfuegos alichaguliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Cuba, hii ni kutokana na uhodari na ushupavu wake wakati wa harakati za Mapinduzi. Siku chache kabla ya kifo chake Camilo Cienfuegos alienda Mjini Camaguey kumkamata rafiki yake na mwanamapinduzi mwenzake Huber Matos kwa amri ya Fidel Castro. Hiyo ni baada ya Huber Matos kumkosoa Fidel Castro na uongozi wake.

Oktoba 28, 1959 Camilo akitokea Camaguey akielekea Havana majira ya Usiku alipotoka kumkamata Mwanapinduzi mwenzake Huber Matos, Ndege aliyokuwa amepanda ilipotea angani bila kujulikana ilipo. Msako wa kuitafuta ndege hiyo ulianza mara moja lakini baada ya siku kadhaa za msako huo, Ndege hiyo haikupatikana tena na ikatangazwa rasmi kifo cha shujaa huyo wa taifa la Cuba.

Maswali mengi yameulizwa bila kupata majibu kuhusiana na Kifo cha Camilo Cienfuegos, wengi wakimtuhumu Fidel Castro kuwa nyuma ya kifo cha Camilo japo ilionekana kama wawili hao walikuwa ni marafiki wa karibu sana, hata Camilo kukubali kumkamata rafiki yake Huber Matos.

Madai ya kuhusika kwa Fidel Castro kwenye kifo cha Camilo yalizimwa vikali na Mwanamipinduzi Ernest Che Guevara baada ya kumsafisha Castro kuwa hakuhusika na kifo cha Mwanapinduzi Camilo.
Camilo alifariki akiwa na miaka 27 tu, hivyo kumfanya Mwanamapinduzi mdogo zaidi kufariki kati ya Wanamapinduzi waliohusika katika Mapinduzi ya Cuba ya 1959.
 
Mkuu haya mapinduzi ya cuba yalilenga nini hasa??na mchango wake duniani hasa kwa sisi weusi wa africa Ilikuwa ni nini???
 
Back
Top Bottom