Mfadhili mkuu wa REDET ajitoa

Ng'wamagigisi

Member
Jan 3, 2011
35
1
Katika pitapitaa ndani ya magazeti yasiyo na mlengo wowote bali kuelisha jamii nimekuta na newz kuwa wafadhili wakuu wa REDET ambayo imekua ikishutumiwa kwa kuchakachua matokeo ya tafiti zake ili kuridhisha matakwa ya mkuu wa kaya na chama chake wamejitoa. Hawa jamaa wamekua wakifadhiliwa na Denmark kupitia shirika lake la DANIDA.

Mdau mkuu wa REDET anadai DANIDA wamejitoa sababu ya mabadiliko yao ya sera. Sera zao mpya zapingana na majukumu na malengo ya REDET.

Tafadhali wana-jf wenye newz kamili kuhusu hawa REDET atujuze. Tafiti zao zina utata sana, zaidi kuna tetesi kuwa laenda kufumuliwa lote ingawa wenyewe wajisifu sana katika utendaji. Nikweli kuwa kizuri huwa chafumuliwa?!
 
Kwanza mbona hamna polls zinazochukuliwa sasa kuhusu uungwaji mkono wa serikali ya JK? Hawa Redet na wengine ni mizigo ya ccm mwanzo mwisho.
 
Bila shaka watafadhiliwa na ccm sasa. Sidhani kama Kikwete atavumilia kutoiona REDET barabarani maana imekuwa ikimpa maujiko.
 
Sina uhakika na hili lakini nahisi ni kawaida kwa wafadhili kujitoa hasa kwa sababu kuu mbili:

1. Kama wanaofadhiliwa wamekwisha fikia ule muda waliokubaliana kuwa taasisi inayofadhiliwa itakuwa imekwisha komaa kiasi cha kujitegemea yenyewe........ Kwa hili sina uhakika kama REDET imekomaa kiasi hicho
2. Iwapo sera za funder zimebadilika na hivyo kubadili mwelekeo wa shughuli za Funders - kama wanavyodai REDET.

All in all REDET imefika wakati wa wao kujitegemea ingawa ni wazi kuwa kwa sasa watahaha kutafuta wafadhili wengine, which to me is rediculous........ Iwaachie nafasi taasisi nyingine changa ziweze pata ufadhili kama wao.
 
Kwa hiyo ni jukumu la CCM na serikali yake kufadhi REDET kwa sasa!!
 
Bora wamejitoa maana hao jamaa wangeibuka na utafiti wenye utata tena!

Kuna tetesi kwamba walikuwa wanafanya utafiti nchi nzima kuangalia ni kiasi gani watanzania tunaiunga mkono Serikali iliyopo madarakani, matokeo ya awali yanaonyesha 92.3% ya Watanzania tumefarijika sana Kikkwete kuchaguliwa na tunampenda sana.
 
Mtegemea cha nduguye hufa angali maskini, nadhani ni muda mwafaka kwa redet kusimama kwa miguu yao wenyewe!
 
Sina uhakika na hili lakini nahisi ni kawaida kwa wafadhili kujitoa hasa kwa sababu kuu mbili:

1. Kama wanaofadhiliwa wamekwisha fikia ule muda waliokubaliana kuwa taasisi inayofadhiliwa itakuwa imekwisha komaa kiasi cha kujitegemea yenyewe........ Kwa hili sina uhakika kama REDET imekomaa kiasi hicho
2. Iwapo sera za funder zimebadilika na hivyo kubadili mwelekeo wa shughuli za Funders - kama wanavyodai REDET.

All in all REDET imefika wakati wa wao kujitegemea ingawa ni wazi kuwa kwa sasa watahaha kutafuta wafadhili wengine, which to me is rediculous........ Iwaachie nafasi taasisi nyingine changa ziweze pata ufadhili kama wao.

Uko sahihi kwa 101% ... hoja zako zote mbili naona zina ukweli kuhusu REDET. Ukisoma hii habari kwenye Raia Mwema utapaa ukweli wote, japo kuna mambo yanafichwa na Dr. Bana: Kilio cha Dk. Slaa chaiponza REDET

REDET ilikuwa haijakomaa na inaonekana hawakuwa wamejiandaa na hili la DANIDA kujitoa na ndio maana wameamua kufumua muundo wake pamoja na kubadilisha majukumu ili waweze kusaka wafadhili wengine.

Utetezi kwamba mikataba ya kazi ilikuwa inaisha mwezi Dec 2010, hauna mashiko kwa kuwa hata kama mfadhili angeendelea kuwepo kwa miaka 10 ijayo, bado mikataba ya kazi huwa ina ukomo. Kama mikataba ya kazi ilikuwa inaishia mwezi Dec mwaka jana, kwanini wanafumua muundo, hao wanaohusika na kufumua muundo ina maana hawahusiki na mikataba? Je, hizo kazi za viporo zitafanywa na nani na ilihali anasema mikataba ya kazi imeisha?

Kusifia kwamba REDET imekuwa ikifadhiliwa kwa miaka 18 na haijawahi kutokea Afrika, huo ni uongo wa wazi. REPOA wamekuwa wakifadhiliwa na serikali ya Uholanzi tangu walipoanza na mpaka sasa bado wanaendelea na ufadhili na ninadhani REPOA walianza miaka hiyo hiyo ya mwanzoni mwa 90.

Pamoja na kwamba Dr. Bana anakanusha kwamba polls za uchaguzi wa mwaka jana hazikuchangia DANIDA kujitoa, nina mashaka sana na hilo na hawezi kuwa mkweli kwa kuwa alishiriki kutenda dhambi ya kudanganya na wakaja kuumbuliwa na matokeo halisi. Kama NEC wasingechakachua REDET ingeumbuka sana. Hilo pia linaweza kuwa limepunguza credibility ya REDET na sasa wanahaha kuifumua ili wapate wafadhili wapya. Kama wako credible kwanini wanabadilisha madhumuni na majukumu yao?
 
bora wafadhili wamejitoa mana hata sielewi REDET walikua wanatafiti nini..................
 
Hata wafumue miundo na hata wabadili na jina haisaidii. Wafadhili wanateta wao kwa wao. Kama wamekuona ufahi kuaminiwa DANIDA wakikutosa hata uende CIDA sijuhi SIDA USAID utagonga mwamba. These people are communicating. Waliona raha kujikomba kwa CCM. Waende wapewe kazi zaidi maana nasikia huyo Banna ni mshauri wa rais masuala ya siasa then ndo researcher, how can he be objective??
 
Kuna tetesi kwamba walikuwa wanafanya utafiti nchi nzima kuangalia ni kiasi gani watanzania tunaiunga mkono Serikali iliyopo madarakani, matokeo ya awali yanaonyesha 92.3% ya Watanzania tumefarijika sana Kikkwete kuchaguliwa na tunampenda sana.

Bora walivyojitoa hao DANIDA kabla ya hayo matokeo ya utafiti wa kipuuzi kwani na hayo mabomu ya Mbagala lazima yamepunguza asilimia nyingi sana bado kwenye malipo najua hapo ndiyo itakuwa ni wizi mtupu
Watu wamerudi majumbani wamekuta mabomu wanawaita askari mpaka sasa hawajafika huo ndo utendaje wa Kikwete na serikali yake ambao wananchi wanaoufurahia?:blah::blah::blah:
 
Kuna tetesi kwamba walikuwa wanafanya utafiti nchi nzima kuangalia ni kiasi gani watanzania tunaiunga mkono Serikali iliyopo madarakani, matokeo ya awali yanaonyesha 92.3% ya Watanzania tumefarijika sana Kikkwete kuchaguliwa na tunampenda sana.

hahaa hii research niliifanya pia..niligharamiwa tiketi ya ndege kwenda Bukoba na kurudi na hela ya kutosha tu
sidhani kama nitakuja kufanya research niliyolipwa pesa nyingi sana kama ile....
 
Back
Top Bottom